Wastaafu watabasamu Tanzania,kilio kwa watumiaji wa vileo Kenya na Uganda yaapa kupambana na deni la kitaifa

Nchi hizo zinakabiliwa na changamoto za kupanda kwa madeni ya umma, gharama ya juu ya mafuta, kushuka kwa mapato na hali ngumu ya kufanya biashara

Muhtasari

  • Mwanahabari wa Marekani kufikishwa mahakamani Urusi kwa tuhuma za ujasusi
  • Wanandoa wasafirishwa hadi Lithuania baada ya kuabiri ndege isiyofaa
  • Kenya: Afisa wa polisi auawa na wenzake baada ya kumpiga risasi hakimu
  • Zelensky atarajia 'maamuzi muhimu' kuhusu Ukraine katika mkutano wa G7
  • Hamas yakanusha lawama za Blinken kwa usitishaji mapigano ambao haukuafikiwa
  • Idadi ya watu wanaotoroka vurugu yaongezeka kwa kiasi cha kuvunja rekodi
  • G7 inapanga kutumia mali ya Urusi iliyokamatwa kufadhili Ukraine
  • Rais Tinubu wa Nigeria aanguka katika hafla ya kitaifa
  • Bajeti Afrika Mashariki: Hofu ya mikopo na mzigo wa madeni
  • Ajali ya boti DR Congo yaua takriban watu 80
  • Meli yajaa maji kufuatia mashambulizi ya Houthi katika bahari ya shamu
  • Meli za kivita za Urusi zawasili Cuba katika onyesho la ubabe
  • Mji wa Buenos Aires wakumbwa na ghasia kufuatia mabadiliko ya Milei
  • Mpango wa kusitisha mapigano Gaza wawekwa katika ratili huku Marekani ikisema Hamas ilipendekeza 'mabadiliko'

Moja kwa moja

Seif Abdalla

  1. Chama cha ANC Afrika Kusini chakaribia kuunda serikali ya Umoja

    .
    Maelezo ya picha, Wafusi wa Chama cha ANC nchini Afrika Kusini

    Chama tawala nchini Afrika Kusini cha African National Congress (ANC) kinasema kuwa kimepiga hatua katika juhudi za kuanzisha serikali ya umoja wa kitaifa baada ya kupoteza idadi kubwa ya wafuasi wake katika uchaguzi wa hivi majuzi.

    Lakini Katibu Mkuu wa chama hicho Fikile Mbalula alisema chama bado hakiko tayari kutangaza maelezo ya makubaliano hayo.

    ANC ilipoteza wingi wake wa wabunge kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 30 katika uchaguzi wa Mei 29, na kupata 40% ya kura.

    Hii ina maana ilihitaji kuungwa mkono na vyama vingine ili Rais Cyril Ramaphosa aweze kusalia madarakani.

    Bunge jipya linakutana kwa mara ya kwanza siku ya Ijumaa, wakati linapotarajiwa kumpigia kura rais. Bw Ramaphosa anatarajiwa kuhifadhi kiti chake."Tunazungumza na vyama vya kisiasa tunapozungumza hivi sasa," Bw Mbalula aliambia wanahabari baada ya mkutano wa maafisa wakuu wa chama hicho, akiongeza kuwa hawezi kutoa maelezo zaidi.

    Alisema itakuwa kuhamia kituo cha kisiasa, kwa sababu vyama vilivyojitenga na ANC vilivyo upande wa kushoto vimesema havitajiunga.

    Alisema vyama vikiwemo vinavyounga mkono biashara vya Democratic Alliance (DA) vimekubaliana kuunda serikali ya umoja wa kitaifa.Lakini ANC na DA hawajaafikiana kuhusu jinsi gani hasa watashirikiana, Bw Mbalula aliongeza.

    "Kama DA ingepata baadhi ya vitu hivi inavyotaka ina maana ANC itakuwa imekufa," alisema.DA ilishika nafasi ya pili katika uchaguzi huo kwa asilimia 22 ya kura.Rais Cyril Ramaphosa hapo awali ameshutumu DA - ambayo inaungwa mkono hasa na watu walio wachache na wa rangi - kwa "uhaini" na "wapinzani".

    Mpango wowote na DA hautakuwa maarufu miongoni mwa wanaharakati wengi wa ANC.Chama hicho ni mtetezi wa uchumi wa soko huria, ambapo kinakinzana na mila za mrengo wa kushoto za ANC, na kina sifa ya kuwakilisha maslahi ya wazungu walio wachache.

  2. Na kufikia hapo ndio tunamaliza matangazo yetu ya moja kwa moja. Kwaheri.

  3. Bajeti Afrika Mashariki: Wastaafu,watabasamu Tanzania,kilio kwa watumiaji wa vileo Kenya na Uganda yaapa kupambana na deni la kitaifa

      • Author, Yusuf Jumah
      • Nafasi, BBC Swahili
    th

    Mawaziri wa fedha wa Afrika Mashariki wamewasilisha mipango yao ya matumizi kwa mwaka wa kifedha wa 2024/2025 huku pakiwa na mazingira magumu ya kiuchumi na kero kubwa la kupanda kwa madeni ya umma, gharama ya juu ya mafuta, kushuka kwa mapato ,hali ngumu ya biashara na mivutano ya kimataifa ya kijiografia katika Mashariki ya Kati na Ulaya Mashariki mambo ambayo yanachangia kuzuia ukuaji wa uchumi katika kanda hii

    Kenya

    Waziri wa Fedha nchini Kenya Prof. Njuguna Ndung'u Alhamisi aliwasilisha makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2024/2025 bungeni akiangazia maeneo ya kipaumbele kwa serikali kufikia Ajenda ya Mabadiliko ya Kiuchumi ya kutoka Chini hadi Juu (BETA).

    Bajeti ya mwaka huu ilihusisha ongezeko la jumla ya matumizi ya serikali hadi Ksh.3.9 trilioni kutoka Ksh.3.6 trilioni katika mwaka wa kifedha wa 2023/24.

    Kati ya Ksh3.9 trilioni, Waziri huyo aliorodhesha maeneo makuu matano ya kipau mbele : Kilimo, Biashara Ndogo, Biashara Ndogo na za Kadri(MSME), Nyumba na Makazi, Huduma ya Afya na na Uboreshaji wa miundo ya Kidijitali na tasnia ya ubunifu.

    Mgao uliotengewa idara za Usalama wa Kitaifa ni jumla ya Sh377.5 bilioni. Kati ya hizo, Ulinzi ulitengewa Sh173 bilioni, Huduma ya Kitaifa ya Polisi Sh110.6 bilioni, Huduma ya Kitaifa ya Ujasusi Sh46.3 bilioni na Magereza ya Kenya Sh32.7 bilioni.

    Zaidi ya hayo, Sh13.9 bilioni zilitengwa kwa ajili ya kukodisha magari ya polisi na Sh918.4 milioni kwa ajili ya kuendeleza Maabara ya Taifa ya Uchunguzi wa Jinai.

    Alipendekeza kubadilisha Ushuru wa Bidhaa kwa vinywaji vikali kutoka viwango maalum kwa lita hadi Sh16 asilimia ya lita ya pombe tupu. "Tunataka kuanza kutoza ushuru kwa vinywaji vya pombe kwa msingi wa kiwango cha pombe," alisema.

    Waziri huyo pia alisema serikali katika mwaka ujao pia itasimamisha uajiri wowote wa wafanyikazi wanaojiunga na utumishi wa umma ili kudhibiti kiasi cha fedha kinacholipwa kwa watumishi kama mishahara .

    "Kutakuwa na ukomo kwa uajiri wote mpya katika sekta ya umma kwa mwaka mmoja ujao,''

    Wakati huo huo, waziri alitangaza kwamba wakati wa kipindi cha kuzuia ajira ya wafanyakazi wapya wa umma , serikali itafanya ukaguzi na kusafisha orodha zote za malipo ya umma.

    Tanzania

    Kwa upande wa Tanzania Waziri wa fedha wa nchi hiyo Mwigulu Nchemba amewasilisha makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2024/2025 ambayo ni shilingi trilioni 49.3 sawa na ongezeko la asilimia 11.2 ikilinganishwa na mwaka wa fedha uliopita.

    Akiwasilisha makadirio hayo bungeni Dodoma, Dr Mwigulu Nchemba ametaja vipaumbele ambavyo serikali imekusudia kuvishughulikia.

    Miongoni mwa masuala ambayo yamekuwa gumzo kubwa katika siku za karibuni ni malipo ya pensheni kwa wastaafu ambapo sasa Serikali imeongeza malipo ya mkupuo kwa asilimia 7 kutoka asilimia 33 ya sasa hadi asilimia 40.

    Aidha serikali ya Tanzania imelenga kuongeza wigo wa kodi na kuzingatia kanuni za usawa za utozaji kodi kwa kukusanya kodi ya zuio kwa kiwango cha asilimia 5 kwenye malipo yanayofanywa kwenda kwa mtengeneza maudhui ya mtan mkazi.

    Kwa mbolea za kilimo kodi itaondolewa kwa mwaka mmoja, kama itakavyokuwa kwa vifaa vya teknolojia ya michezo kama vile mfumo wa usaidizi wa waamuzi katika soka kwa kifupiVAR.

    Kadhalika katika sekta ya madini kodi imefutwa kwa wafanyabishara watakaoiuzia Benki Kuu ya Tanzania madini moja kwa moja.

    Hata hivyo, serikali imependeleza kuanza kwa tozo ya shilingi mia tatu kwa kila kilo moja ya gesi inayotumika katika magari.

    Kwa upande mwingine Waziri Mwigulu Nchemba ametetea deni la serikali ambalo linaongezeka kila kukicha na kufikia shilingi trilioni 91 na kuzua mjadala katika jamii.

    Waziri huyo amesema wanaoanzisha mjadala wa deni la serikali wanapaswa kutambua kuwa kukua kwa deni hilo kunatokana na sababu mbalimbali ikiwemo changamoto za kiuchumi duniani zilizosababisha sarafu ya Tanzania kushuka thamani yake dhidi ya Dola ya Marekani na kwamba fedha zinazokopwa zinatumika katika miradi muhimu ya maendeleo ya nchi

    Matarajio ya wengi yalikuwa ni kuona utitiri wa kodi unapungua na kuleta nafuu kwa watu wa kipato cha chini, jambo ambalo halijatekelezwa kikamilifu huku ikiwa ni bajeti itakayogharamia pia uchaguzi wa serikali za mitaa baadaye mwak huu, pamoja na ujenzi na ukarabati wa viwanja vya michezo kwa ajili ya fainali za mataifa ya Afrika zitakazochezwa Tanzania, Kenya na Uganda mwaka 2027.

    Uganda

    Uganda inatarajia kupunguza deni linaloongezeka kwa kuzingatia ukopaji wa masharti nafuu na kuzuia mikopo ya kibiashara mwaka ujao wa kifedha, waziri wake wa fedha Matia Kasaijaalisema Alhamisi, baada ya kushuka kwa kiwango cha mikopo mwezi uliopita.

    Deni la umma la nchi hiyo ya Afrika Mashariki limekuwa likiongezeka huku serikali ya Rais Yoweri Museveni ikisitisha miradi mikubwa ya miundombinu, jambo ambalo limezusha onyo kutoka kwa benki yake kuu.

    Waziri wa Fedha Matia Kasaija alisema katika makadirio ya bajeti kuwa jumla ya deni la umma lilifikia dola bilioni 24.7 mwishoni mwa mwaka jana na lilionekana kuongezeka hadi dola bilioni 25.7 mwishoni mwa mwezi huu.

    Gharama za huduma ya deni bila ukombozi wa deni la ndani zilitarajiwa kumeza 40.3% ya mapato ya ndani katika mwaka wa fedha unaoanza Julai, kutoka 33.4% katika mwaka huu.

    Serikali ya Uganda inasema kukopa kumetumika kukuza uchumi, ambao umekua kwa haraka kuliko nchi nyingine za Afrika tangu janga la COVID-19.

    Uchumi ulitarajiwa kukua kati ya 6.4% na 7% mwaka ujao wa fedha, Kasaija alisema, ukichochewa na shughuli za mafuta na gesi kabla ya uzalishaji wa mafuta ghafi uliopangwa kuanzia 2025/26.

    "Uchumi wa Uganda umeimarika kikamilifu kutokana na misukosuko mbalimbali ya nje na ya ndani ambayo iliathiri utendaji kazi katika miaka minne iliyopita," Kasaija alisema.

    Mchango wa ripoti kutoka kwa Florian Kaijage akiwa Dar es Salaam

  4. Tanzania: Polisi wamshikilia aliyekuwa mkuu wa mkoa kwa tuhuma za ulawiti

      • Author, Florian Kaijage
      • Nafasi, BBC Dar es Salaam
    th

    Polisi nchini Tanzania inamshikilia aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Simiyu, ulipo Kusini Mashariki mwa Ziwa Victoria, Dkt., Yahya Nawanda kwa tuhuma za kumlawiti mwanafunzi wa chuo kikuu kilichopo jijini Mwanza.

    Hatua ya polisi kumshikilia Dkt. Nawanda imetangazwa na kamanda wa polisi wa mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa alipozungumza na waadishi wa habari.

    Kamanda Mutafungwa amesema polisi inamhoji Dkt. Nawanda kuhusiana na tuhuma zinazomkabili huku uchunguzi wa kina ukiendelea kuhusiana nan tukio hilo.

    Nawanda alitenguliwa kwenye nafasi ya mkuu wa mkoa Jumanne Juni 11, 2024 baada ya kudumu kwenye nafasi hiyo kwa zaidi kidogo ya miaka miwili. Hata hivyo, taarifa ya Kurugenzi ya mawasiliano ya rais Ikulu haikutaja sababu za Dkt. Nawanda kutenguliwa katika wadhifa huo. Alinukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari akidai kuwa alikuwa ameundiwa kashfa ili aondolewe kwenye nafasi ya mkuu wa mkoa.

    Tanzania ina sheria kali dhidi ya makosa ya kulawiti. Mtu anayekutwa na kosa la kulawiti huklabiliwa na adhabu ikiwemo kifungo gerezani

  5. Mwanahabari wa Marekani kufikishwa mahakamani Urusi kwa tuhuma za ujasusi

    .

    Mwandishi wa habari wa Marekani Evan Gershkovich atashtakiwa nchini Urusi kwa mashtaka ya ujasusi, waendesha mashtaka wa Urusi wamesema.

    Ripota wa Wall Street Journal ameshutumiwa kwa kukusanya "taarifa za siri" kutoka kiwanda cha kutengeneza vifaru cha Urusi kwa niaba ya CIA.

    Waendesha mashtaka wanasema atasimama katika mahakama ya Yekaterinburg - mji aliokamatwa mwezi Machi mwaka jana akiangazia vita vya Ukraine.

    Bw Gershkovich, gazeti lake na Marekani zinakanusha mashtaka, huku Washington ikimtaja rasmi kama "aliyezuiliwa kimakosa".

    Waendesha mashtaka wa Urusi walisema siku ya Alhamisi kwamba uchunguzi ulibaini kwamba mwandishi huyo alikuwa amekusanya "taarifa za siri" kuhusu "uzalishaji na ukarabati wa vifaa vya kijeshi" kutoka kwa kiwanda cha kutengeneza vifaru cha Urusi.

    Katika taarifa, walimshutumu kwa kufanya "vitendo haramu kwa kutumia njia za kula njama".

    Hii, waendesha mashtaka walisema, ilikuwa "kwa maagizo ya CIA".

    Tangu kukamatwa kwake, Bw Gershkovich amesalia katika kizuizi kabla ya kesi yake kuanza ramsi mjini Moscow, maili 1000 (1609km) kutoka Yekaterinburg.

    Amekaa gerezani kwa zaidi ya mwaka mmoja na akipatikana na hatia anakabiliwa na kifungo cha miaka 20 jela.

    Kukamatwa kwake kulikua mara ya kwanza kwa Urusi kumshutumu mwandishi wa habari wa Marekani kwa ujasusi tangu enzi ya Usovieti.

    Ubalozi wa Marekani mjini Moscow umesema sababu za kuzuiliwa kwake hazina msingi.

    soma zaidi:

  6. Ryanair: Wanandoa wasafirishwa hadi Lithuania baada ya kuabiri ndege isiyofaa

    .

    Wanandoa wawekwa kwenye ndege isiyo sahihi walipokuwa wakielekea kwenye likizo ya familia, na badala yake waliishia umbali wa maili 1,500 kutoka mahali walipokusudia.

    Safari ya kwenda Costa Brava ilikuwa ya siku ya kuzaliwa ya Andrew Gore, lakini wakati wengine katika familia walikuwa wakiwasili katika uwanja wa ndege wa Barcelona, ​​Andrew na mkewe Victoria walijikuta katika jiji la Kaunas la Lithuania.

    Baada ya kugundua walikuwa wamewekwa kwenye ndege isiyo sahihi ya Ryanair, wanandoa kutoka Mountain Ash, Rhondda Cynon Taf, walisema waliachwa wakiwa na "mfadhaiko".

    Uwanja wa ndege wa Bristol ulisema ulikuwa ukifanya kazi ya kuchunguza kilichotokea na kufanya maboresho, huku Ryanair ilisema kwamba wafanyakazi hufanya matangazo kadhaa kabla ya kuondoka kuwafahamisha abiria maeneo ya wanakoelekea.

  7. Kenya: Afisa wa polisi auawa na wenzake baada ya kumpiga risasi hakimu

    .

    Afisa wa polisi ameripotiwa kumpiga risasi na kumjeruhi hakimu mwandamizi katika Mahakama ya Makadara jijini Nairobi, Ofisi ya msajili mkuu wa mahakama imesema.

    Polisi huyo anasemekana kumpiga risasi hakimu wakati akiwa anatoa uamuzi wa kesi inayomhusisha mke wake.

    ‘’Tunasikitika kuripoti tukio la kupigwa risas lenye kumhusisha afisa wa polisi na Hakimu katika Mahakama ya Makadara mnamo tarehe 13 Juni 2024,’’ Ofisi ya msajili mkuu wa mahakama ilisema.

    Wakati kikao cha wazi cha mahakama kinaendelea, hakimu alifuta dhamana kwa mshtakiwa ambaye alikosa kufika mahakamani baada ya kupewa dhamana na kushindwa kutoa maelezo ya kuridhisha kwanini alifanya hivyo.

    Ofisi ya msajili mkuu wa mahakama imesema, ‘mara baada ya uamuzi huo kutolewa mtu alimpiga risasi hakimu na kumjeruhi kwenye nyonga’.

    Maafisa wa polisi waliokuwepo eneo la tukio walijibu haraka kwa kumpiga risasi na kumuua huku hakimu akikimbizwa hospitali kwa matibabu.

  8. Zelensky atarajia 'maamuzi muhimu' kuhusu Ukraine katika mkutano wa G7

    .

    Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky anasema anatarajia "maamuzi muhimu" yatafanywa katika mkutano wa kilele wa G7 wa viongozi kutoka mataifa saba tajiri zaidi duniani.

    "Kiasi kikubwa kitatolewa kwa Ukraine, ulinzi wetu na uthabiti wa kiuchumi," alisema katika ujumbe kwenye Telegraph.

    Ikulu ya White House inasema G7 imepiga hatua nzuri katika mpango wa Marekani wa kutumia mali ya Urusi iliyokamatwa kukusanya $50bn (£39bn) kwa mwaka kwa nchi yake.

    Bw Zelensky, ambaye atahudhuria mkutano huo, anatarajiwa pia kutia saini mikataba mipya ya usalama na Japan na Marekani.

    Mataifa ya G7 ya Canada, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Japan, Uingereza na Marekani yamekuwa wafuasi muhimu wa kifedha na kijeshi wa Ukraine tangu uvamizi kamili wa Urusi mnamo 2022.

    Mali ya Urusi ambayo ilizuiliwa na kundi hilo, pamoja na EU, wakati Moscow ilipovamia Ukraine ni $325bn.

    Chini ya sheria za kimataifa, nchi haziwezi kutaifisha mali hizo kutoka kwa Urusi na kuzipa Ukraine.

    Lakini kima hicho kinazidi kuzalisha riba nyingi - karibu $3bn kwa mwaka - kwa hivyo wazo ni kutumia riba hiyo kwa njia ya ubunifu.

    Mpango ni kuchukua mkopo katika masoko ya kimataifa, kutoa takriban $50bn kwa Waukraine kila mwaka, na kutumia $3bn kulipa riba ya mkopo huo kila mwaka.

    Inaonekana kueleweka moja kwa moja, lakini ni vigumu sana. Bado kuna mengi yakutatuliwa.

    Soma zaidi:

  9. Hamas yakanusha lawama za Blinken kwa usitishaji mapigano ambao haukuafikiwa

    .

    Hamas imerudi nyuma baada ya kukosolewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken kwa kutokubali pendekezo la kusitisha mapigano, ikisema imeonyesha mtazama "chanya" katika mazungumzo hayo.

    Kundi hilo lilisema "limeshughulikia vyema... pendekezo la hivi karibuni na mapendekezo yote ya kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano".

    Ilisema, kinyume chake, "wakati Blinken anaendelea kuzungumza juu ya idhini ya 'Israel' ya pendekezo la hivi karibuni, hatujasikia afisa yeyote wa Israel akitoa idhini".

    Bw Blinken amesema mara kwa mara kwamba Israel imekubali pendekezo la kusitisha mapigano lililotolewa na Rais Biden tarehe 31 Mei. Serikali ya Israel haijasema hivyo rasmi, ingawa mpango wa Israel uliunda msingi wa tamko la Bw Biden.

    Akizungumza nchini Qatar siku ya Jumatano, Bw Blinken alionyesha kuchoshwa na jibu la Hamas kwa pendekezo la Israel la kusitisha mapigano, ambalo kundi hilo liliwasilisha Jumanne.

    Maelezo ya majibu hayajawekwa wazi, ingawa Bw Blinken alisema Hamas ilipendekeza mabadiliko, ambayo baadhi yake hayakuweza kutekelezeka.

    "Wakati fulani katika mazungumzo - na hii imejirudia kwa muda mrefu - inafika mahali ambapo ikiwa upande mmoja unaendelea kubadilisha matakwa yake, ikiwa ni pamoja na kutoa matakwa na kusisitiza mabadiliko ya mambo ambayo tayari yamekubalika lazima wahoji kama wanaendelea kwa nia njema au la."

    Lakini katika msururu wa taarifa siku ya Jumatano usiku, Hamas ilihoji iwapo Israel imekubali mpango huo au azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linaloidhinisha.

    Pia unaweza kusoma:

  10. Idadi ya watu wanaotoroka vurugu yaongezeka kwa kiasi cha kuvunja rekodi

    .
    Maelezo ya picha, Mwanamke aliyekimbia vita nchini Sudan ameketi katika nyumba ya familia moja huko Chad

    Watu milioni 120 wamelazimika kukimbia makazi yao kutokana na vita, ghasia na mateso na kuweka rekodi mpya - mwaka wa 12 mfululizo idadi hiyo imeongezeka, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi lilisema.

    Idadi ya watu waliolazimika kuhama makazi yao duniani sasa ni sawa na ile ya Japan, shirika hilo lilisema.

    Migogoro mipya nchini Sudan na Gaza ilichangia kuongezeka, ambayo mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi Filippo Grandi aliita "mashtaka mabaya juu ya hali ya dunia".

    Alitoa wito kwa serikali kushughulikia chanzo cha tatizo, badala ya kuwaingiza wakimbizi kisiasa na kugeukia masuluhisho ya haraka kama vile kufunga mipaka, jambo ambalo aliiambia BBC kuwa halitatatua tatizo hilo.

    Badala yake, alizitaka nchi kufanya kazi pamoja kwa ajili ya suluhu za kudumu zaidi.

    Migogoro mipya na ya zamani iliongeza idadi ya wakimbizi duniani kote kufikia Aprili 2024, kulingana na ripoti ya kila mwaka ya shirika hilo kuhusu suala hilo.

    Nchini Sudan, vita vilivyoanza kati ya majenerali wapinzani mnamo Aprili 2023 vililazimisha zaidi ya watu milioni tisa kuondoka kwa makazi yao.

    Huko Gaza, vita kati ya Israel na Hamas vimesababisha takriban 75% ya wakazi - watu milioni 1.7 - tangu Oktoba.

    Mgogoro mkubwa zaidi wa uhamaji wa watu duniani umesalia nchini Syria, ambapo mzozo ulioanza mwaka 2011 unawazuia karibu watu milioni 14 kutoka makwao.

    Mamilioni ya watu zaidi walifukuzwa kutoka makwao katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Myanmar kwa sababu ya mapigano mwaka jana.

    Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi limesema si kweli kwamba wakimbizi wote na wahamiaji wengine walikwenda katika nchi tajiri, likieleza kuwa idadi kubwa ya wakimbizi hao wako katika nchi jirani na zenye kipato cha chini na cha kati.

    Idadi ya watu waliokimbia makazi duniani kote imeongezeka karibu mara tatu tangu 2012 na huenda ikaongezeka, Bw Grandi alisema.

    Soma zaidi:

  11. G7 inapanga kutumia mali ya Urusi iliyokamatwa kufadhili Ukraine

    .
    Maelezo ya picha, Mashambulizi ya Urusi dhidi ya Ukraine yameiacha nchi hiyo ikiwa na njaa ya pesa na uchovu wa vita

    Viongozi kutoka mataifa saba tajiri zaidi duniani wanakutana nchini Italia kwa mkutano unaotarajiwa kukubaliana mpango wa kutumia mali ya Urusi iliyopigwa tanji ili kukusanya mabilioni ya dola kwa Ukraine.

    Pendekezo la Marekani linaweza kuongeza $50bn (£39bn) kwa mwaka kwa Ukraine, pamoja na kutumia shinikizo jipya la kiuchumi kwa Urusi.

    Vile vile vinavyotarajiwa kuwa ajenda katika mkutano wa G7 ni vita vya Gaza, uhamiaji, usalama wa kiuchumi na akili mnemba (AI).

    Mkutano huo unakuja wakati viongozi kadhaa - ikiwa ni pamoja na Rishi Sunak, Emmanuel Macron na Joe Biden - wakikabiliwa na changamoto za uchaguzi nyumbani.

    Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak alijitoa katika uchaguzi mkuu kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika mwezi ujao.

    Pia chama kinachowakabili wapiga kura katika kipindi cha wiki chache ni chama cha Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, ambaye aliitisha uchaguzi wa haraka wa bunge baada ya kushindwa kwa kura ya maoni ya Kitaifa ya mrengo mkali wa kulia katika uchaguzi wa mwishoni mwa juma lililopita kwa bunge la EU.

    Wakati huo huo, Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau na Rais wa Marekani Joe Biden wenyewe wanaweza kushindwa wakati ujao wapiga kura watakapopiga kura.

    Giorgia Meloni wa Italia amejigamba kuwa nchi yake ilikuwa inaelekea katika mkutano huu ikiwa na "serikali yenye nguvu kuliko zote", baada ya utendaji mzuri katika uchaguzi wa Ulaya mwishoni mwa juma lililopita.

    Soma zaidi:

  12. Rais Tinubu wa Nigeria aanguka katika hafla ya kitaifa

    .
    Maelezo ya picha, Rais Tinubu wa Nigeria

    Rais wa Nigeria Bola Tinubu ameteleza na kuanguka chini katika hafla rasmi ya kuadhimisha miaka 25 ya demokrasia nchini humo.

    Rais, 72, alianguka alipokuwa akipanda ngazi kwenye gari ambalo lilipaswa kumpeleka karibu na Bustani ya Eagle Square katika mji mkuu, Abuja. Ilibidi asaidiwe kusimama. Mmoja wa wasaidizi wake alielezea kama "hatua mbaya" na akasema rais ameweza kuendelea na programu iliyobaki.

    "Mara moja aliendelea na sherehe hiyo. Hakuna masuala," aliandika msaidizi wa rais Dada Olusegun kwenye X. Mpinzani wa karibu wa Bw Tinubu wakati wa uchaguzi wa mwaka jana, Atiku Abubakar, alionyesha huruma yake.

    “Ninamuhurumia kwa dhati Rais Bola Tinubu kuhusu tukio hili lisilo la kufurahisha alipokuwa amepangwa kukagua gwaride la Siku ya Demokrasia. Ninatumai kuwa kila kitu kiko sawa naye, "aliandika kwenye X.

    Mwanasiasa maarufu na mwanaharakati Shehu Sani alisema haikuwa jambo kubwa, na kwamba tukio hilo lilionyesha rais hana tofauti na mtu mwingine yeyote.“Si Rais Tinubu pekee, yeyote aliye hai anaweza kujikwaa na kuanguka; ilitokea kwa Rais Biden na Fidel Castro. Marais ni binadamu.

    ”Mtumiaji wa X Arinze Odira alisema kuanguka "kunatisha kutazama".Mnigeria mwingine Charles Awuzie alichapisha kwenye Facebook kwamba alipata hisia baada ya kuona klipu hiyo."Iwapo ni Rais Biden au Rais Tinubu, kwa kawaida mimi huhisi uchungu wakati mwanadamu anajeruhiwa mahali pa huduma.

    Namtakia heri rais.”Wakati Wanigeria wengi wameonyesha huruma na kumtakia heri, kwa baadhi imezua maswali mengi kuhusu afya yake, ambayo ilihojiwa na wapinzani wake wakati wa kampeni za uchaguzi uliokuwa na ushindani mkali mwaka jana.

  13. Bajeti Afrika Mashariki: Hofu ya mikopo na mzigo wa madeni

    Maelezo ya video, Kwanini serikali haichukui mapato yake kutoka vyanzo vingine vya ndani?

    Leo bajeti ya serikali za Kenya, Uganda na Tanzania zitasomwa.

    Nchini Tanzania, suala la deni la taifa ni kitu kinachofuatiliwa kwa ukaribu.

    Baadhi ya maswali ambayo wengi wanauliza ni pamoja na; je, deni ni kubwa kiasi gani? Serikali imekopa kutoka wapi? Kwanini isichukue mapato yake vyanzo vingine vya ndani.

    Mwandishi wa BBC Sammy Awami anajaribu kujibu baadhi ya maswali hayo.

  14. Ajali ya boti DR Congo yaua takriban watu 80

    .

    Takriban watu 80 wamefariki dunia baada ya boti kuzama katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, rais wa nchi hiyo amesema.

    Maafa hayo yalitokea Jumatano kwenye Mto, kilomita 70 kutoka mji wa Mushie katika jimbo la Maï-Ndombe karibu na mpaka na nchi jirani ya Kongo-Brazzaville.

    Katika taarifa kwenye mtandao wa kijamii, Rais Félix Tshisekedi alisema "amehuzunishwa".

    Rais alisema walioathiriwa watapata usaidizi na pia akaagiza uchunguzi ufanyike kubaini kilichosababisha.

    "Rais wa Jamhuri anatoa wito wa uchunguzi kuhusu sababu za kweli za tukio hili la kusikitisha, ili kuzuia maafa kama haya kutokea tena katika siku zijazo," ofisi ya rais ilisema kwenye X, ambayo zamani ilikuwa Twitter.

    Ajali mbaya za boti ni za kawaida nchini DR Congo, ambapo boti mara nyingi hujaa abiria ambao ni nadra kupewa jaketi za usalama na mara nyingi hawawezi kuogelea.

  15. Meli yajaa maji kufuatia mashambulizi ya Houthi katika bahari ya shamu

    .
    Maelezo ya picha, Waasi wa Houthi wametangaza kuwaunga mkono Wapalestina katika Ukanda wa Gaza

    Jeshi la Marekani limesema meli inayomilikiwa na Ugiriki katika Bahari ya Shamu imeshambuliwa na meli isiyo na rubani iliyotumwa na Wahouthi nchini Yemen, na kusababisha mafuriko makubwa na uharibifu wa chumba cha injini.

    Ofisi ya Jeshi la Wanamaji la Kifalme la Uingereza la Operesheni za Biashara ya Baharini (UKMTO) ilisema ilipokea ripoti za meli hiyo iliyoshambuliwa kwenye eneo la bahari takriban maili 66 kusini magharibi mwa bandari inayodhibitiwa na waasi ya Hodeida nchini Yemen siku ya Jumatano.

    Chombo hicho hakikuwa chini ya amri ya wafanyakazi wa UKMTO ilisema. Hakuna majeruhi walioripotiwa.Waasi wa Houthi wanaoungwa mkono na Iran walidai kuhusika na shambulio hilo, wakisema walilenga meli yenye bendera ya Liberia iitwayo Tutor kwa kutumia ndege isiyo na rubani ya baharini.

    Waasi wa Houthi wamekuwa wakishambulia meli katika Bahari ya Shamu kuwaunga mkono Wapalestina huko Gaza, na kusababisha usumbufu mkubwa wa biashara ya dunia.

    Katika taarifa, msemaji wa jeshi la Houthi alisema meli hiyo ilishambuliwa "kwa kutumia boti isiyo na rubanina makombora ya masafa marefu, na kuongeza kuwa meli hiyo "iliharibiwa vibaya, na inaweza kuzama".Meli hiyo ililengwa “kwa sababu kampuni inayomiliki meli hiyo imekiuka uamuzi wa kupiga marufuku kuingia katika bandari za Palestina inayokaliwa kwa mabavu”, ilisema taarifa hiyo.

    Kamandi Kuu ya Marekani (CentCom) iliripoti kwamba "meli ya Houthi inayoungwa mkono na Iran isiyo na rubani (USV)" ilishambulia meli hiyo iliokuwa imetia nanga hivi majuzi nchini Urusi.

    Athari "ilisababisha mafuriko makubwa na uharibifu wa chumba cha injini", ilichapishwa kwenye X.CentCom iliongeza kuwa vikosi vyake "vimefanikiwa kuangamiza" kurusha makombora matatu ya kuzuia meli katika eneo linalodhibitiwa na Wahouthi nchini Yemen katika muda wa saa 24 zilizopita, pamoja na ndege moja isiyo na rubani iliyorushwa kutoka eneo linalodhibitiwa na Wahouthi nchini Yemen juu ya Bahari ya Shamu.

    "Tabia hii ya chuki na uzembe inayoendelea kufanywa na Wahouthi wanaoungwa mkono na Iran inatishia uthabiti wa kikanda na kuhatarisha maisha ya mabaharia katika Bahari ya Shamu na Ghuba ya Aden," ilisema.

    Kundi la Houthi lenye silaha linajiona kama sehemu ya "mhimili wa upinzani" unaoongozwa na Irani dhidi ya Israeli, Marekani na Magharibi kwa upana, na limetangaza uungaji mkono wake kwa Wapalestina katika Ukanda wa Gaza.

  16. Meli za kivita za Urusi zawasili Cuba katika onyesho la ubabe

    .
    Maelezo ya picha, Umati wa watu ulishangilia wakati meli ya kijeshi ya Admiral Gorshkov ya Urusi na meli nyingine tatu zikiingia kwenye Ghuba ya Havana.

    Meli nne za jeshi la wanamaji la Urusi - ikiwa ni pamoja na manowari inayotumia nguvu za nyuklia na frigate - zimewasili Cuba, katika kile kinachoonekana kama kuonyesha ubabe huku kukiwa na mvutano na nchi za Magharibi kuhusu vita vya Ukraine.

    Meli hizo zimetia nanga kwenye Ghuba ya Havana - takriban maili 90 (km 145) kutoka jimbo la Marekani la Florida.

    Wizara ya ulinzi ya Urusi imesema meli ya Admiral Gorshkov na nyambizi ya Kazan zinabeba silaha za hali ya juu, ikiwa ni pamoja na makombora ya hypersonic Zircon.

    Hapo awali walifanya mazoezi ya makombora katika bahari ya Atlantiki.

    Lakini wizara ya mambo ya nje ya Cuba inasema hakuna meli yoyote inayobeba silaha za nyuklia, na ziara yao ya siku tano haileti tishio kwa eneo hilo.

    Maafisa wa Marekani wanasema wanafuatilia kwa karibu ziara hiyo.

    Jeshi la Wanamaji la Marekani pia lilitumia ndege zisizo na rubani za baharini kuzuia meli za Urusi zilipokuwa zikikaribia Cuba, mshirika wa BBC wa Marekani CBS anaripoti.

  17. Mji wa Buenos Aires wakumbwa na ghasia kufuatia mabadiliko ya Milei

    .
    Maelezo ya picha, Ghasia mjini Bueno aires nchini Argentina kufuatia mabadiliko ya kiuchumi

    Polisi wa kutuliza ghasia katika mji mkuu wa Argentina Buenos Aires walifyatua gesi ya kutoa machozi na maji ya kuwasha kuwatawanya waandamanaji nje ya Bunge la Congress, kabla ya wabunge kutoa kibali cha awali cha mageuzi ya kupunguza bajeti katika Seneti ya Brazil siku ya Jumatano.

    Waandamanaji - ambao wanasema hatua hizo zitaumiza mamilioni ya Waajentina - walirusha mabomu ya petroli na mawe, na kuchoma moto gari moja.Idadi kuu ya watu waliripotiwa kujeruhiwa, na vyombo vya habari vya ndani vikielezea tukio hilo Jumatano kama "uwanja wa vita".

    Mpango wa mageuzi, uliopendekezwa na Rais wa mrengo wa kulia Javier Milei ili kufufua uchumi unaokua wa nchi hiyo, ni pamoja na kutangaza hali ya hatari ya kiuchumi, kukata pensheni na kupunguza haki za wafanyikazi.

    Hatua hizo zinapingwa na vyama vya kisiasa vya mrengo wa kushoto, vyama vya wafanyakazi na mashirika ya kijamii.

    Lakini hoja hiyo, ambayo awali ilikuwa sare ya 36-36 katika bunge la Seneti, ilipitishwa awali Jumatano baada ya mkuu wa baraza hilo, Makamu wa Rais Victoria Villarruel, kuvunja sare.

    "Kwa wale Waajentina wanaoteseka, wanaosubiri, ambao hawataki kuona watoto wao wakiondoka nchini... kura yangu ni ya uthibitisho," makamu wa rais na kiongozi wa Seneti Bi Villaruel alisema baada ya matokeo ya kura kuwa sare.

    Mswada huo wa vifungu 328 sasa utachunguzwa hatua kwa hatua kabla ya kuidhinishwa kikamilifu siku ya Alhamisi.Kisha utarudi kwenye bunge la chini kwa ajili ya kuidhinishwa.

    .
  18. Mpango wa kusitisha mapigano Gaza wawekwa katika ratili huku Marekani ikisema Hamas ilipendekeza 'mabadiliko'

    .
    Maelezo ya picha, Waziri wa masuala ya kigeni nchini Marekani Anthony Blinken

    Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken ameiambia Hamas kwamba ni "wakati wa kukomesha malumbano", baada ya viongozi wake kupendekeza "mabadiliko mengi" kwenye mpango wa kusitisha mapigano Gaza na kuachiliwa kwa mateka.

    Aliwaambia waandishi wa habari mjini Doha kwamba baadhi ya mabadiliko "yanawezekana" na mengine hayafanyiki, lakini kwamba Marekani na wapatanishi Qatar na Misri "zitajaribu kuhakikisha mkataba huo umeafikiwa".

    Hamas ilisema Jumanne kwamba iko tayari "kushughulikia vyema" mchakato huo lakini ikasisitiza haja ya Israel kukubaliana na usitishaji vita wa kudumu na kujiondoa kikamilifu Gaza.

    Serikali ya Israel haikutoa maoni yoyote, lakini afisa mmoja ambaye jina lake halikutajwa alisema kuwa jibu la kundi la wapiganaji la Palestina lilikuwa ni kukataliwa.

    Waziri mkuu wa Israel bado hajaidhinisha hadharani pendekezo hilo, ambalo Rais wa Marekani Joe Biden alisema lilitolewa na nchi hiyo alipolieleza siku 12 zilizopita.

    Lakini Bw Blinken anasema Benjamin Netanyahu "amethibitisha ahadi yake" wakati wa mkutano mjini Jerusalem siku ya Jumatatu.

    Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa pia lilipitisha azimio linalounga mkono pendekezo hilo siku hiyo, na kuongeza shinikizo la kidiplomasia ambalo Washington inatoa.

  19. Natumai hujambo. Karibu katika matangazo ya moja kwa moja