Uganda yakana kumsaidia rais Salva Kiir kijeshi

Serikali ya Uganda imekanusha madai ya upande wa makamu rais wa Sudan Kusini bwana Riek Machar kuwa Uganda ilimsaidia rais Salva Kiir kijeshi.
Maelezo ya picha, Serikali ya Uganda imekanusha madai ya upande wa makamu rais wa Sudan Kusini bwana Riek Machar kuwa Uganda ilimsaidia rais Salva Kiir kijeshi.
Iliyochapishwa

Serikali ya Uganda imekanusha madai ya upande wa makamu rais wa Sudan Kusini bwana Riek Machar kuwa Uganda ilimsaidia rais Salva Kiir kijeshi.

Taarifa zinamnukuu mmoja wa maafisa wa Sudan People’s Liberation Movement in Opposition-(SPLM-O) kuwa utawala wa Kampala umempa msaada wa kijeshi serikali ya Rais Salvar Kiir katika mapigano yaliyozuka juzi.

Utawala wa Kampala umekanusho hilo kupitia msemaji wake na waziri wa habari Frank Tumwebaze

''Mtu yeyote anaetoa madai kama hayo si makini. Hatujayasikia hayo sisi kama serikali ya Uganda lakini hayana msingi na yanafaa kuitwa ya kipuuzi. Kwanza kabisa vita gani vilivyokuwepo?

Waziri wa habari Frank Tumwebaze
Maelezo ya picha, Waziri wa habari Frank Tumwebaze

Ni kitu kilichotokea katika eneo lao na kwa hivyo tunawezaje kuwa tulikuwa huko ?''

Baada ya mapiagano ya wao kwa wao kutokea Julai saba mwaka huu,raia kadhaa, mkiwemo wa Uganda inasemekana walijikuta katika njia panda na mapigano hayo na hivyo kulazimisha Uganda kutuma askari wake Juba kuweza kuwaondoa.

Jeshi la Uganda kwa upande wake linasema liliomba serikali ya Juba kufanya hivyo kama anavyosema mkuu wa utawala katika jeshi la Uganda Brigadia Leopold Kyanda.

''Huenda hilo linaweza kuwa ndilo limechochea lawama hizo ambazo zimeonekana katika vyombo vya habari jambo ambalo msemaji wa serikali ya Uganda pia ametupilia mbali''.

uganda iliwatuma wanajeshi wake nchini Sudan Kusini kuwaokoa raia wake waliokuwa Juba
Maelezo ya picha, uganda iliwatuma wanajeshi wake nchini Sudan Kusini kuwaokoa raia wake waliokuwa Juba

''Mchango pekee wa jeshi la UPDF nchini Sudan Kusini ni kuwaokoa raia wetu ambao walikuwa walizingirwa na vita vyao visivyo na msingi''. alisema bwana Kyanda.

Waziri wa Uganda ameshangazwa na madai hayo ya upande wa Dr Machar na kuongeza kuwa ni rais Museveni ambae alipendekeza katika mkutano wa Muungano wa Afrika uliomalizika mjini Kigali njia ambazo zinamlinda Dr Machar.

 Brigadia Leopold Kyanda
Maelezo ya picha, Brigadia Leopold Kyanda

''Rais Museveni katika mkutano wa juzi wa Muungano wa Afrika ndio aliongoza pendekezo la kuundwa kwa kikosi cha kanda AU ambacho miongoni mwa mengine ni kumlinda Riak Machar.

Pia nilisikia taarifa kutoka upande wa Machar ukikaribisha pendekezo hilo.

Sasa inakuwaje tena kwa wakati mmoja tusikie ripoti kama hizo.''

Uhusiano katika utawala wa Kampala na Dr Machar umekuwa na walakini hasa kutokana na hatua ya majeshi ya Uganda kusaidia serikali ya rais Salvar Kiir katika mapigano ya kwanza kati ya vigogo hao wawili kabla ya juhudi za upatanishi zilizofanyika Ethiopia na kupelekea majeshi ya Uganda kuondolewa.