Polisi kufukua kaburi la halaiki Kenya

Polisi nchini Kenya wamepata idhini ya mahakama kufukua kaburi la halaiki
Maelezo ya picha, Polisi nchini Kenya wamepata idhini ya mahakama kufukua kaburi la halaiki
Iliyochapishwa

Polisi nchini Kenya wamepata idhini ya mahakama <bold><link type="page"><caption> kufukua kaburi la halaiki lililodaiwa kupatikana hapo jana mjini Mandera</caption><url href="http://www.bbc.com/swahili/habari/2015/12/151207_mandera_mass_graves.shtml" platform="highweb"/></link></bold> Kaskazini Mashariki mwa taifa hilo.

Hapo jana miili ya watu waliozikwa katika makaburi yasiojulikana katika eneo la Mandera

Mwili wa mwanamke mmoja ulipatikana ukiwa umezikwa katika eneo hilo hapo jana baada ya kutoweka katika mazingira ya kutatanisha.

Wakaazi wa eneo hilo wamehofia kuwa huenda kukawa na miili zaidi iliyozikwa katika eneo hilo.

Viongozi kutoka eneo hilo linalokaliwa na idadi kubwa ya watu wa jamii ya Wasomali wameshutumu vikosi vya usalama.

Viongozi hao wanadai polisi wanawauwa washukiwa wa ugaidi na kutupa miili yao katika makaburi ya pamoja.
Maelezo ya picha, Viongozi hao wanadai polisi wanawauwa washukiwa wa ugaidi na kutupa miili yao katika makaburi ya pamoja.

Viongozi hao wanadai polisi wanawauwa washukiwa wa ugaidi na kutupa miili yao katika makaburi ya pamoja.

Maafisa wakuu wa serikali, kiongozi wa uchunguzi wa maiti, mawakili na umma wote walikongamana katika makao makuu ya serikali ya mji wa Mandera ilikuishinikiza serikali kutoa idhini rasmi ya kufukua miili hiyo.

Wenyeji wanadai kuwa miili 12 ikiwemo moja ya mwanamke mmoja aliyeripotiwa kutoweka majuzi tu iligunduliwa katika kaburi la karibu viungani mwa mji wa Mandera.

Msemaji wa polisi Charles Owino alikanusha madai hayo akisema kuwa hiyo ni propaganda ya kundi la wapiganaji wa kiislamu la al-Shabab.