Tetesi za soka Ulaya Jumapili 21.06.2020:Jimenez, Mane, Walker, Cavani, Bailey, Fati, Henderson

Chanzo cha picha, Getty Images
Juventus imeingia kwenye kinyang'anyiro sambamba na Manchaster United na Real Madrid wakitaka kupata saini ya mshambuliaji wa Mexico anayekipiga Wolves ,Raul Jimenez,29. (Calcio Mercato, via Mail on Sunday)
Winga wa Liverpool, Msenegali Sadio Mane, 28, atahusika katika mpango wa kubadilishana na mchezaji wa Paris ST-Germain, mshambuliaji wa Kifaransa, Kylian Mbappe, 21, kwa kitita cha pauni milioni 200 (Sun on Sunday)
Inter Milan wanataka kumsajili mshambuliaji Kyle Walker, 30 anayeichezea Manchester City (Sun on Sunday)

Mshambuliaji wa Uruguay Edinson Cavani, 33, na mchezaji wa nafasi ya ulinzi Thomas Munier,28, hawataongeza mkataba wao na Paris St-Germain baada ya tarehe 30 mwezi Juni, hii ikimaanisha kuwa hawatakuwa kwenye Kampeni za ligi ya champions, inayoanza mwezi Agosti. (RMC, via Mail on Sunday)
Chelsea, Manchester City na Manchester United wanamtaka winger wa Bayer Leverkusen Leon Bailey, huku mchezaji huyo raia wa Jamaica akiwa na thamani ya pauni milioni 40. (Mail on Sunday)

Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester United wameambiwa wanapaswa kuweka mezani pauni milioni 355 kama wanataka kumchukua winga wa kikosi cha wachezaji wa umri wa chini ya miaka 21, Ansu Fati, 17 Mhispania anayeichezea Barcelona. ( Sunday Express)
Manchester United wanamtaka mlinda mlango wa Kiingereza Dean Henderson lakini Chelsea wanamhitaji mchezaji huyo, 23, ambaye yuko na kikosi cha Sheffield United kwa mkopo. (Sun on Sunday)

Chelsea wamekataa ofa ya Juventus kubadilishana wachezaji ambapo kiungo wa Italia Jorginho, 28, angeondoka Blues, huku kiungo Miralem Pjanic,30 angehamia Stamford Bridge kutoka kwenye klabu hiyo ya Serie A. ( Calcio Mercato, via Sunday Express)
Kiungo wa Uhispania Dani Ceballos, 23, atabaki kwa mkopo Arsenal akitoka Real Madrid mpaka mwishoni mwa msimu lakini amekubali kuwa anaweza kuondoka kwenye klabu hiyo iwapo Zinedine Zidane atasalia kuongkoza Bernabeu msimu ujao. (Marca)

Chanzo cha picha, Getty Images
Everton na Newcastle wanamtaka kiungo wa kati wa AC Milan Franck Kessie, 23. (Tuttosport)
Mshambuliaji wa zamani wa Newcastle na England Andy Carroll,31, atasalia St James'Park msimu mwingine (Sundaya Mirror)
Kocha wa Aston Villa Dean Smith amesema klabu yake iko kwenye mchakato wa kuongeza mkataba wa mkopo kwa mlinda mlango Pepe Reina, 37, aliyejiunga na klabu hiyo akitokea AC Milan, na kiungo wa Chelsea Danny Drinkwater. Mikataba ya sasa itamalizika tarehe 30 mwezi Juni. (Birmingham Mail)






























