Tetesi za Soka Ulaya Jumamosi 08.02.2020: Martinez, Dembele, Traore, Coutinho, Koulibaly

Chanzo cha picha, Getty Images
Chelsea inasemekana kwamba iko mbioni wasajili mshambuliaji wa Inter Milan na Argentina Lautaro Martinez, 22, na mshambuliji wa Lyon Moussa Dembele, 23. (Evening Standard)
Manchester United inataka kumsajili mlinzi wa timu ya Napoli na Senegal Kalidou Koulibaly, 28, msimu wa joto ujao. (Star)
Arsenal imejiunga na Leicester kumtafuta kumsajili winga wa timu ya Brentford raia wa Algeria Said Benrahma, 24. (Sun)

Chanzo cha picha, Getty Images
Southampton inatarajia kukubaliana kuhusu mkataba mpya na meneja Ralph Hasenhuttl kabla ya kumalizika kwa msimu huu. (Telegraph)
Liverpool haitarajiwi kusaini mkataba mpya na kiungo wa kati wa Uingereza Adam Lallana, 31, ambaye mkataba wake wa sasa unamalizika mwishoni mwa msimu huu. (Liverpool Echo)
Chelsea inakaribia kufikia makubaliano na kiungo wa kati wa Uingereza Tino Anjorin, 18, na mlinzi wa raia wa Uholanzi Ian Maatsen, 17.

Chanzo cha picha, Getty Images
Barcelona imeonyesha nia ya kumsajili tena raia wa Uhispania Adama Traore baada ya kuhofia kwamba huenda Real Madrid ikakimbilia kumsajili winga huyo mwenye umri wa miaka 24. (Mail)
Juventus inamwinda mshambuliaji wa Chelsea na Italia Emerson Palmieri, 25, kama mmoja wa wale wanaomlenga wakati wa usajili msimu wa joto. (Inside Futbol)
Tottenham, Burnley na Aston Villa zote zimeonesha nia ya kumsajili mshambuliajo wa Fenerbahce raia wa Uturuki Vedat Muriqi, 25. (Calciomercato - in Italian)






























