Kenya yapiga moyo konde kuhusu miundombinu

Iliyochapishwa

Kenya inasisitiza itaendelea na miradi yake ya miundo mbinu itakayogharimu mabilioni ya dola licha ya mataifa jirani kujiondoa katika mipango hiyo.

Miaka minne iliyopita Kenya ilizindua mradi mkubwa wa ujenzi wa barabara kuu, reli, bandari na miji mikubwa ambao utagharimu zaidi ya dola bilioni ishirini.

Lakini nchi hiyo inakabiliwa na ushindani mkubwa kutoka kwa taifa jirani ya Tanzania ambalo pia linajenga bandari na reli mpya.

Katika miezi ya hivi karibuni Uganda na Rwanda zimechagua kufanya biashara na Tanzania licha ya awali kusaini mikataba mikubwa na kenya. Je ni kwa nini Kenya imejikuta katika hali hiyo?

Mwandishi wetu Emmanuel Igunza na mengi zaidi.