Je Sudan Kusini imeporomoka?

Iliyochapishwa

Nchi changa zaidi duniani Sudan Kusini , imeorodheshwa kama nchi ya kwanza yenye hali tete zaidi duniani , kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa nchini Marekani.

Somalia ambayo daima ilikuwa ya kwanza kama nchi iliyoporomoka kwa miaka sita mfululizo, ilishikilia nafasi ya pili, ikifuatiwa na CAR, DRC, Sudan na Chad.

Mmoja wa watafiti wakuu wa utafiti huo, J.J. Messner, alisema kuwa matatizo yanayokumba Sudan Kusini yalikuwa ukosefu wa hali thabiti, uongozi duni na ukabila.

Hali ambazo zimechochea ghasia nchini humo.