Marekani na Uingereza zafanya mashambulizi mapya dhidi ya Wahouthi wa Yemen
Marekani inasema washirika hao walilenga maeneo 18, ikiwa ni pamoja na hifadhi ya makombora na ndege zisizo na rubani.
Moja kwa moja
Ambia Hirsi
Vita vya Ukraine: Zelensky asema wanajeshi 31,000 waliuawa

Chanzo cha picha, Getty Images
Rais wa Ukraine anasema wanajeshi 31,000 wameuawa tangu uvamizi kamili wa Urusi uanze.
Volodymyr Zelensky alisema hatatoa idadi ya waliojeruhiwa kwasababu hatua hiyo ingesaidia mipango ya kijeshi ya Urusi.
Kwa kawaida, maafisa wa Ukraine hawatangazi hadharani idadi ya wanajeshi waliouawa katika vita.
Haya yanajiri baada ya waziri wa ulinzi kusema nusu ya misaada yote ya Magharibi kwa Ukraine imecheleweshwa, hali inayogharimu maisha na maeneo yanayokaliwa na Warusi.
"Kwa sasa, ahadi inayotolewa haiendani na upokeaji wa vifaa," Rustam Umerov alisema katika hotuba ya televisheni siku ya Jumapili.
Ukraine kwa sasa inakabiliwa na vikwazo mbalimbali katika dhamira yake ya kuiondoa Urusi kutoka katika eneo lake.
Bw Umerov alisema kuwa ukosefu wa vifaa unaiweka Ukraine katika hasara zaidi "katika mikakati ya vita".
"Tunafanya kila linalowezekana na lisilowezekana lakini bila kupata msaada kwa wakati hatuwezi kuendelea na juhudi hizi," alisema.
Mnamo Januari, Umoja wa Ulaya (EU) ulisema zaidi ya nusu ya hizi zitafika Ukraine kufikia tarehe ya mwisho na kwamba kiasi kamili kilichoahidiwa hakipatikana hadi mwisho wa 2024.
Mkuu wa sera za kigeni wa EU, Josep Borrell, alilaumu ukosefu wa uwezo wa uzalishaji lakini Katibu Mkuu wa Nato Jens Stoltenberg alisema washirika wamekuwa wakiongeza hatua hii.
Vikosi vya Ukraine mara nyingi vimelalamikia uhaba katika vita vyao na Urusi.
Rais Volodymyr Zelensky alisema moja ya sababu za Ukraine kukabiliana na mashambulizi ambayo hayakutarajiwa kuanza mapema mwaka jana ni ukosefu wa silaha.
Maelezo zaidi:
Israel inafikiria mpango wa kusitisha mapigano - ripoti

Chanzo cha picha, Getty Images
Baraza la mawaziri la Israel limearifiwa kuhusu yanayojiri katika mazungumzo ya kusitisha mapigano mjini Gaza, kufuatia hatua iliyofikiwa katika mazungumzo mjini Paris siku ya Jumamosi.
Haya yanajiri huku polisi wakivunja maandamano ya kumtaka Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu ajiuzulu mjini Tel Aviv.
Polisi wa kukabiliana na ghasia wametumia farasi kuwatawanya waandamanaji waliokuwa wakijaribu kuelekea kwenye uwanja wa Demokrasia.
Mazungumzo hayo ya Paris ni sehemu ya mazungumzo yanayolenga kufikia usitishaji vita na kuachiwa kwa mateka.
Makubaliano hayo pia yatashuhudia kuachiliwa kwa wafungwa wa Kipalestina wanaoshikiliwa nchini Israel.
Jumamosi jioni, baraza la mawaziri la vita la Israel liliarifiwa kuhusu mazungumzo mjini Paris na wapatanishi kutoka Misri, Qatar na Marekani.
"Tunajitahidi kupata maelezo zaidi ya kuachiwa kwa mateka wetu," Bw Netanyahu aliandika kwenye mtandao wa X zamani Twitter.
"Ndio maana nilituma wajumbe Paris - na usiku wa leo tutajadili hatua zinazofuata katika mazungumzo."
Baadaye, iliripotiwa kuwa Israel itatuma wajumbe nchini Qatar kwa mazungumzo zaidi wiki hii.
CNN: Idadi kubwa ya raia wa Urusi wanaomba hifadhi nchini Korea

Chanzo cha picha, Getty Images
Idadi kubwa ya raia wa Urusi waliomba hifadhi ya kisiasa nchini Korea Kusini, imeandika CNN ikiashiria hati ya uhamiaji ya Korea Kusini.
Kulingana na hati hiyo, mnamo 2023, Warusi 5,750 walisajiliwa nchini Korea Kusini kuomba hifadhi ya kisiasa nchini humo.
Hii ni mara tano zaidi ya mwaka uliopita, wakati Warusi 1,038 waliomba hifadhi nchini Korea Kusini. Idadi hyo pia inazidi jumla ya watu walioomba hifadhi kati ya 1994 hadi 2019, CNN inabainisha.
Mwaka jana watu 18,838 waliomba hifadhi nchini Korea Kusini, idadi kubwa zaidi ikiwa ya raia wa Urusi wakifuatiwa na Kazakhstan (2,094), China (1,282), Malaysia (1,205), India (1,189), Mongolia (836) na Uturuki (564).
Idadi ya waomba hifadhi nchini Korea Kusini mwaka jana ilikuwa ya juu zaidi katika kipindi cha miaka minane, kulingana na huduma ya uhamiaji nchini humo.
Korea Kusini ina sheria kali za uhamiaji. Kulingana na Wizara ya Sheria ya nchi hiyo, kuanzia 1994 hadi mwisho wa 2023, watu 103,760 waliomba hadhi ya ukimbizi, na ni 4,052 tu kati yao walifaulu kupata hifadhi.
Rais wa Namibia Hage Geingob azikwa mjini Windhoek

Chanzo cha picha, Reuters
Umati mkubwa wa watu umehudhuria mazishi ya kitaifa ya Rais wa Namibia Hage Geingob aliyefariki kutokana na saratani akiwa na umri wa miaka 82.
Bw Geingob alizikwa katika kaburi la Mashujaa laAcre nje kidogo ya mji mkuu, Windhoek, huku waombolezaji wakitoa heshima kwa mtu waliyemsifu kama mjenzi wa taifa na shujaa wa Afrika nzima.
Mjane wake, Monica Geingob, alilia jeneza lake lilipokuwa likishushwa ndani ya kaburi lake.
Mazishi ya Bw Geingob yaliadhimisha kilele cha maombolezo ya wiki tatu.
Bw Geingob alifariki hospitalini tarehe 4 Februari, na naibu wake, Nangolo Mbumba, kuapishwa kama mrithi wake muda mfupi baadaye.
Kifo chake kiliibua hisia ya uzalendo, huku Wanamibia wakiweka kando tofauti zao za kisiasa kuomboleza kifo cha Rais Geingob.

Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Raia wa Namibia kutoka matabaka mbalimbali walikusanyika pamoja kuomboleza kifo cha rais wao Maelfu ya watu - wengi wakiwa wamebeba bendera ya Namibia na mavazi ya rangi ya kitaifa - walijipanga barabarani kumuaga katika mitaa ya Windhoek siku ya Ijumaa na Jumamosi
Mwili wake ulilazwa katika Uwanja wa Uhuru, kabla ya kuchukuliwa Jumapili, ukiwa kwenye gari maalum na kwenda kupumzishwa makaburi ya Mashujaa.
Hii ilikuwa mara ya kwanza kwa Namibia kumpoteza rais tangu uhuru wake kutoka Afrika Kusini, wakati huo chini ya utawala wa wazungu wachache, mwaka 1990.
Watangulizi wawili wa Bw Geingob, Sam Nujoma na Hifikepunye Pohamba, walihudhuria maziko yake, pamoja na takriban wakuu 20 wa nchi na serikali.
Raia wa Namibia kutoka matabaka mbalimbali walikusanyika pamoja kuomboleza kifo cha rais wao.
Jeshi la Somalia lashiriki mazoezi ya kijeshi nje ya nchi kwa mara ya kwanza

Chanzo cha picha, SNA
Makumi ya wanajeshi wa Somalia wamewasili nchini Kenya kwa mazoezi ya kijeshi yatakayoshirikisha nchi kadhaa za Afrika.
Makomando waliopewa mafunzo maalum ya Danab wa Somalia watakuwa wa kwanza kushiriki katika mazoezi ya kijeshi nje ya nchi hiyo tangu kuangushwa kwa serikali ya Mohamed Siad Barre mwaka 1991.
Kamanda wa jeshi la Somalia, Jenerali Ibrahim Sheikh Muhyiddin, amelitaka jeshi la Somalia linaloshiriki mazoezi hayo kuonyesha vipaji miongoni mwa mamia ya wanajeshi wanaoshiriki zoezi hilo, na kuleta sifa kwa taifa la Somalia.
Tanzania: Idadi ya waliofariki katika ajali ya Arusha yafikia 25
Idadi ya vifo vilivyotokana na ajali iliyohusisha magari manne katika Barabara Kuu ya Arusha-Namanga imeongezeka na kufikia 25 huku majeruhi wakiwa 21.
Ajali hiyo iliyotokea Jumamosi ilihusisha lori na magari mengine madogo matatu.Katika taarifa kwa vyombo vya habari jana usiku katika Hospitali ya Rufaa ya Mtakatifu Meru, Kamishna wa Polisi Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, CP Awadhi Juma Haji amesema miongoni mwa waliofariki ni wanawake 11 akiwemo mtoto wa kike mdogo, huku raia wa kigeni waliofariki wakifikia saba.
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameungana na Watanzania wengine kuwafariji waliofiwa na kuwatakia afueni ya haraka waliojeruhiwa.
Ruka X ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
ECOWAS yaiondolea vikwazo Niger

Chanzo cha picha, Getty Images
Jumuiya ya Kanda ya Afrika Magharibi (ECOWAS) imetangaza kuondolewa kwa vikwazo vilivyowekwa dhidi ya Niger.
Hayo yalifikiwa katika mkutano wa viongozi mjini Abuja, wakitaka kupitisha mkakati mpya wa kuzishawishi nchi zinazoongozwa na wanajeshi kusalia katika umoja huo.
Vikwazo vya awali vililenga shughuli za usafiri, biashara na uchumi nchini kwa lengo la kugeuza mapinduzi ya Julai 26 ya mwaka jana na baadhi ya maafisa wa kijeshi.
Rais wa Tume ya ECOWAS Omar Alieu Touray ambaye alisoma maamuzi yaliyofikiwa na viongozi wa ECOWAS, alisema kuwa kuondolewa kwa vikwazo dhidi ya Niger ni "kwa misingi ya kibinadamu" ili kupunguza mateso yaliyosababishwa na matokeo yake.
Viongozi wa kijeshi wa majirani watatu wa Sahel pamoja na Guinea sasa wako huru kushiriki katika masuala ya kiufundi na usalama ya umoja huo.
ECOWAS pia imetoa wito wa kuachiwa huru kwa rais aliyeondolewa madarakani Mohamed Bazoum, na kuzitaka nchi hizo nne kuwasilisha ratiba zao za mpito wa kidemokrasia.
Pia unaweza kusoma:
Trump ashinda uteuzi wa mgombea urais wa Republican Carolina Kusini

Chanzo cha picha, Getty Images
Donald Trump anakaribia kupata uteuzi wa mgombea wa urais wa chama cha Republican baada ya kupata ushindi mkubwa dhidi ya Nikki Haley huko South Carolina.
Rais huyo wa zamani alishinda jimbo la nyumbani la mpinzani wake mkuu kwa tofauti ya pointi 20, ushindi wake wa nne mfululizo.
Bw Trump hakumtaja mpinzani wake alipokuwa akisherehekea, akiweka mtazamo wake kwenye uchaguzi mkuu wa Novemba.
Akifanikiwa kushinda uteuzi huo atakutana tena na mrithi wake katika Ikulu ya White House.
"Tutamtazama Joe Biden machoni," aliwaambia wafuasi dakika chache baada ya vyombo vya habari vya Marekani kumkadiria kama mshindi Jumamosi usiku.
"Anaharibu nchi yetu - na tutasema 'toka Joe, umefukuzwa kazi'.
" Bw Trump alisifu "umoja" wa chama chake baada ya matokeo ya Jumamosi, akisema: "Hakujawahi kuwa na roho kama hii. Sijawahi kuona Chama cha Republican kikiwa na umoja hivyo."
Iliashiria mabadiliko kutoka kwa majibu yake kwa mchujo wa mwezi uliopita huko New Hampshire, ambapo alimkashifu Bi Haley kwa "kutoa hotuba kama alivyoshinda".
Bi Haley, ambaye aliwahi kuwa gavana maarufu wa Jimbo la South Carolina kwa mihula miwili , alimpongeza mpinzani wake kwa ushindi wake katika hotuba yake.
Aliapa kusalia katika kinyang'anyiro hicho, hata hivyo, akisema 40% ya kura alizopata "sio kidogo".
Soma:
Marekani na Uingereza zafanya mashambulizi mapya dhidi ya Wahouthi wa Yemen

Chanzo cha picha, ROYAL AIR FORCE HANDOUT/EPA-EFE/REX/Shutterstock
Pentagon inasema ndege za kivita za Marekani na Uingereza zimefanya mashambulizi katika maeneo 18 ya waasi wa Houthi nchini Yemen - operesheni ya pamoja ya nne ya washirika.
Marekani inasema mashambulizi ya Jumamosi yalilenga vituo vya kuhifadhia silaha, ndege zisizo na rubani, mifumo ya ulinzi wa anga, rada na helikopta za wanamgambo hao.
Uingereza inasema washirika hao walichukua hatua ya "kusambaratisha" uwezo wa Houthi.
Wahouthi wanaoungwa mkono na Iran wamekuwa wakifany amashambulizi dhidi ya meli katika njia muhimu ya biashara ya Bahari ya Shamu.
Wahouthi - ambao wanadhibiti maeneo makubwa ya Yemen ukiwemo mji mkuu Sanaa - wamekuwa wakilenga meli ambazo wanasema zina uhusiano na Israel na nataifa ya Magharibi katika hatua ya kukabiliana na vita vinavyoendelezwa na Israel mjini Gaza.
Njia ya usafirishaji wa bidhaa duniani kupitia majini sasa inakabiliwa na usumbufu mkubwa.
Hali hiyo imechangia kupanda kwa gharama kutokana na baadhi ya makampuni makubwa ya usafirishaji kugeuza safari mbali na Bahari ya Shamu - mojawapo ya njia za meli zenye shughuli nyingi zaidi duniani.
Maelezo zaidi:
Hujambo na karibu kwa matangazo ya moja kwa moja.
