Maelfu wanatoroka kaskazini mwa Gaza huku wanajeshi wa Israel wakiushambulia mji huo
Njia ya kusini ilifunguliwa kwa saa tano - lakini mamlaka inayoendeshwa na Hamas inasema mashambulizi ya anga yanaendelea.
Moja kwa moja
Mkuu wa Umoja wa Mataifa asema idadi ya raia waliouawa Gaza inaonyesha kitu 'kibaya'

Chanzo cha picha, Getty Images
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres anasema idadi ya raia waliouawa katika Ukanda wa Gaza inaonyesha kuwa kuna kitu "kibaya" katika operesheni za kijeshi za Israel dhidi ya Hamas katika eneo hilo.
Alisema wafanyakazi 92 wa Umoja wa Mataifa pia wameuawa katika mzozo wa Israel na Hamas.
"Kuna ukiukwaji haki za binadamu wa Hamas wanapowafanya binadamu zao," Guterres aliliambia shirika la habari la Reuters.
"Lakini mtu anapotazama idadi ya raia waliouawa katika operesheni za kijeshi, kuna jambo ambalo ni baya kabisa."

Chanzo cha picha, EPA
Maelezo ya picha, Watu wakiwasha mishumaa karibu na picha za mateka wa Israel na wahasiriwa walipokuwa wakiadhimisha mwezi mmoja tangu shambulio la Octoba 07 la Hamas kwenye mkutano wa kumbukumbu huko Jerusalem. Wakati huo huo katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, amesema Umoja wa Mataifa unahusika katika mazungumzo yenye lengo la kuachiliwa kwa mateka zaidi ya 200 waliochukuliwa wakati Hamas ilipoanzisha mashambulizi yake dhidi ya Israel kutoka Ukanda wa Gaza mwezi uliopita.
"Tuna wajibu wa kufanya kila linalowezekana ili kuwawezesha kuachiliwa kwa mateka," aliambia shirika la habari la Reuters.
"Hatuna nguvu dhidi ya Hamas kwa hilo lakini kuna baadhi ya nchi ambazo zina uwezo wa ushawishi." anasema.
"Misri imekuwa hai sana. Wengine wanafanya kila wawezalo. Tunawasiliana na mamlaka za Israel pia," anasema.
"Ni muhimu kabisa kwamba mateka wote waachiliwe mara moja na bila masharti," aliongeza.
Alisema malori 630 ya misaada yamepita Gaza kwa muda wa siku 18 zilizopita - ikilinganishwa na malori 500 tyaliyopita kila siku kabla ya vita - na "mazungumzo" yanaendelea ili kuhakikisha misaada inatolewa kwa njia inayofaa, lakini hadi sasa misaada "imechelewa sana, imechelewa".
Soma zaidi:
- 'Nilimwambia binti yangu kuwa simu ya baba imeharibika kwa hivyo hawezi kutupigia'
- Baba kutoka Israel na Palestina waungana kwa huzuni juu ya vifo vya binti zao
Mwanaume wa Nigeria auawa katika jaribio la hirizi ya kuzuia risasi

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Baadhi ya watu nchini Nigeria wanaamini kwamba hirizi huwalinda Mwanamume mmoja ameuawa kwa kupigwa risasi katika jimbo la kaskazini-mashariki la Bauchi nchini Nigeria wakati kile kinachojulikana kama hirizi ya kuzuia risasi - au "dawa ya bunduki" - kilikuwa kikifanyiwa majaribio na mganga wa kienyeji, msemaji wa polisi Ahmed Wakil amesema.
Mganga huyo - ambaye anadaiwa kufyatua risasi hiyo kwa bunduki iliyotengenezwa kienyeji - amekamatwa, pamoja na washukiwa wengine wawili, huku washukiwa wengine wakiwa hawajulikani walipo baada ya kutoroka, aliongeza.
Uchunguzi wa ufanisi wa "dawa ya bunduki" ulifanyika kwa mwanakijiji Muhammadu Ali mwenye umri wa miaka 43, Wakil alisema.
Polisi walikimbilia eneo la tukio mara tu waliposikia kuhusu ufyatuaji risasi, na kumpeleka Bw Ali hospitalini, lakini alitangazwa kuwa amefariki alipofika, msemaji wa polisi aliongeza.
Washukiwa hao watafikishwa mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika, Supt Wakil alisema.
Hirizi zinazoaminika kuwa na nguvu za uchawi hutumiwa sana nchini Nigeria, ambapo watu wengi huwasiliana na waganga wa kienyeji kuhusu masuala mbalimbali.
Lakini kumekuwa na ripoti kadhaa za watu kuuawa baada ya kupima kile kinachoitwa hirizi zisizozuia risasi na dawa.
Picha za satelaiti zinaonyesha Wapalestina wakielekea kusini
Wapalestina wanaendelea kuukimbia mji wa Gaza, wakielekea kusini kando ya Barabara ya Salah al-Din - barabara kuu ya Ukanda wa Gaza na njia kuu ya uokoaji.
Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) linasema kuwa barabara hiyo ni salama kutumiwa nyakati maalumu za za siku kwa kawaida kati ya nne asubuhi na saa nane kwa saa za Israeli – muda huo uliongezwa kwa saa moja leo.
Kitengo cha BBC uhakiki wa taarifa- BBC Verify kimetatahmini kijiografia video ya IDF, iliyochapishwa jana, takriban kilomita 3 (maili 1.9) kaskazini mwa Gaza - mpaka wa asil uliotambuliwa kama mpaka unaogawanya maeneo ya kati ya Kaskazini na Kusini.
Katika video hiyo, raia wanaweza kuonekana wakielekea kusini kando ya barabara.
Watu wanaotembea kwa njia sawa wanaweza pia kuonekana kwenye picha za satelaiti zilizopatikana jana.
Dalili za uharibifu zinaonekana, ikiwa ni pamoja na baadhi ya majengo na uchafu kwenye barabara kuu.
Picha ya pili, iliyopigwa karibu kilomita 1 (maili 0.6) kaskazini mwa mji wa Gaza, inaonyesha kundi kubwa la raia wakitembea kuelekea kusini mwa Gaza, ambako IDF inachukulia 'eneo salama'.


Makabiliano ya mabomu katika mpaka wa Lebanon na Israel yachacha

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Picha ya uzio wa mpaka baina ya Israel na Lebanon Mashambulizi ya Israel kusini mwa Lebanon yameanza tena leo, baada ya makombora kurushwa kutoka eneo la Lebanon kuelekea maeneo ya Israel karibu na eneo la mpakani.
Mapigano ya muda mrefu yanaendelea katika maeneo ya mpakani kati ya vikosi vya Israel na wapiganaji wa Hezbollah, huku kukiwa na hofu ya kuongezeka zaidi kwa mapigano na kuibuka kwa eneo jipya la vita kusini mwa Lebanon na kaskazini mwa Israel.
Soma zaidi:
- Hezbollah yaonya vita vya kikanda ikiwa mashambulizi Gaza yataendelea
Wanajeshi maalum wa Israel kati ya 32 waliouawa katika uvamizi wa ardhini Gaza

Chanzo cha picha, IDF
Jeshi la Israel limethibitisha kuwa mwanajeshi mmoja wa kikosi maalum ameuawa katika mapigano huko Gaza.
Kufikia sasa Israel imethibitisha kuwa wanajeshi 32 wa IDF wameuawa huko Gaza tangu uvamizi wa ardhini uanze tarehe 27 Oktoba.
Sgt Daraja la Kwanza Jonathan Chazor, mwanajeshi wa umri wa miaka 22 wa kitengo cha Shaldag cha Jeshi la Wanahewa la Israeli, aliuawa katika vita kaskazini mwa Gaza, IDF inasema kwenye orodha yake ya majeruhi.
IDF imechapisha majina ya wanajeshi 350 waliofariki tangu vita kuanza, wengi wao waliuawa katika mashambulizi ya Hamas tarehe 7 Oktoba.
Wakati huo huo Waziri wa Ulinzi wa Israel Yoav Gallant anasema kiongozi wa Hamas yuko kwenye chumba chake na hazungumzi na mtu yeyote - hajui hilo kwa uhakika.
Jeshi la Israel halikuweza kupata taarifa za kijasusi kwamba Hamas ilikuwa na mpango wa kufanya mauaji hayo tarehe 7 Oktoba.
''Kwa hivyo nadhani tunahitaji kutilia maanani madai yao ya ujuzi fulani. Israeli ni nchi yenye nguvu sana, yenye jeshi lenye nguvu sana, na wanapeleka kiasi kikubwa huko Gaza. Kwa hiyo ingawa Israel ina silaha zote nzito, swali ni iwapo wanaweza kuwashinda wapiganaji wa Hamas ambao wamekuwa wakitoa video zao wakikimbia huku na kule na kutoka nje ya vichuguu, na kurusha aina mbalimbali za makombora ya kukinga mizinga dhidi ya jeshi la Israel na magari yanayoenda mji wa Gaza.''
Wapalestina waomboleza kifo nje ya hospitali
Maafisa huko Gaza wanasema nyumba za kaskazini zilishambuliwa na mashambulio ya Israeli jana usiku.
Shirika la habari la Wafa liliripoti vifo katika mji wa Gaza na katika eneo lote.
Kama ukumbusho, jeshi la Israel kwa wiki kadhaa limewaambia watu kuondoka katika mji wa Gaza na kaskazini mwa ukanda huo, lakini maelfu wamesalia.

Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Kundi la Wapalestina katika Hospitali ya Indonesia, kaskazini mwa Gaza, waliinamisha vichwa vyao katika maombi Jumatano asubuhi. 
Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Moshi umetanda kaskazini mwa Ukanda wa Gaza baada ya kile maafisa wa Gaza wanasema ni mgomo wa Israel Mkulima wa Australia anusurika kushambuliwa na mamba baada ya kumg’ata

Chanzo cha picha, PA Media
Maelezo ya picha, Mamba wanafugwa chini ya Wilaya ya Kaskazini na sheria za Australia Mkulima wa Australia anasema ana bahati ya kuwa hai baada ya kuzuia shambulio la mamba kwa kumng'ata mnyama huyo.
Mfugaji wa ng'ombe Colin Deveraux amekuwa hospitalini kwa mwezi mmoja baada ya kuumwa na mamba wa maji ya chumvi mwenye urefu wa mita 3.2 (futi 10) katika eneo la Kaskazini.
Alikiambia chombo cha habari CBA News kuwa aliuma kope za mamba katika harakati zake za kuyanusuru maisha yake.
Bw Deveraux alisema masaibu yake yalianza baada ya kusimama katika ziwa la billabong alipokuwa akisafiri kujenga uzio karibu na Mto Finnis mwezi uliopita.
Alitulia kando ya ziwa baada ya kuona samaki wakiogelea katikati ya maji ya mawimbi. Baada ya kuondoka tena, mamba "aliushika " mguu wake wa kulia, akimtikisa kama "mwanasesere " na kumvuta ndani ya maji.
Bw Deveraux aliambia ABC kwamba alijaribu kwanza kumpiga teke mamba kwenye mbavu kwa mguu wake mwingine - kabla ya kumuuma.
"Nilikuwa katika hali isiyo ya kawaida ... lakini kwa bahati mbaya meno yangu yalishika kope zake. Zilikua nene sana, kama kushikilia ngozi, lakini nilirudisha kope zake na akaliachia.
"Niliruka na kupiga hatua kubwa hadi lilipo gari langu. Alinifukuza kwa muda,kwa mita kama nne, lakini akasimama."
Bw Deveraux alisema alitumia taulo na kamba kuzuia damu kuvuja kwenye mguu wake, kabla ya kaka yake kumchukua kilomita 130 (maili 80) kwa gari hadi kaskazini Hospitali ya Royal Darwin.
"Kama [mamba] angeniuma mahali pengine ingekuwa tofauti," alisema.
"Inamaanisha lazima nibadili kile ninachofanya. Nimekuwa nikizunguka eneo hilo lenye maji kwa muda mrefu nikitengeneza uzio na maisha ya kuishi, lakini tukio hili limenifungua macho yangu."
Kulingana na serikali ya mtaa mamba ndio msingi wa tasnia muhimu katika Wilaya ya Kaskazini na wanalindwa na sheria.
Wanachukuliwa kuwa wa kuvutia sana kisayansi na kibinadamu na vile vile kivutio muhimu cha watalii.
Kuwatoroka wapiganaji wa Hamas: Jaribio la familia ya Israeli kuwaokoa binti zao
Maelezo ya video, Kujaribu kuwatoroka wapiganaji wa Hamas: Jaribio la familia ya Israeli kuwaokoa binti zao Picha za CCTV zinaonyesha kwa undani jinsi familia ya Swissa ilijaribu kuukimbia mji wa Sderot karibu na mpaka wa Gaza wakati wapiganaji wa kundi la Hamas waliposhambulia tarehe 7 Oktoba, baada ya kwanza kurusha safu ya roketi.
Bi Eliana Swissa anamsimulia Michael Shuval wa BBC Idhaa ya Kiarabu kuhusu mateso ambayo mwanawe, binti-mkwe na wasichana wao wawili walivumilia.
Hamas waliua jumla ya watu 1,400 na kuwateka nyara zaidi ya watu 200.
DRC: Mapigano makali yanaendelea kati ya vikosi vya serikali na waasi wa M23

Chanzo cha picha, AF
Mapigano yamekuwa yakiendelea huko Masisi kati ya vikosi vya serikali na waasi wa M23 Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokeasia ya Kongo (DRC).
Madaktari Katika mji wa Bambo ulio Kilomita 60 karibu na mji wenye wakazi wengi wa Goma wamethibitisha vifo vya watu watano na wengine 30 kujeruhiwa katika mapigano hayo.
Mapigano hayo yamehusisha matumizi ya silaha nzito na nyepesi pamoja na kupeleka ndege za kivita aina ya Sukhoi 25.
Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, Stephane Dujarric amethibitisha kuwa wanajeshi wa Umoja wa Mataifa nchini Congo MONUSCO na wanajeshi wa DRC FARDC wameungana na kuanzisha operesheni, (Springbok).
Alisema "Wenzetu wa kulinda amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wanatuambia kwamba wameanzisha operesheni ya pamoja na wanajeshi wa Kongo huko Kivu Kaskazini ili kulinda miji muhimu ya kikanda ya Goma na Sake.
Operesheni Springbok - kama inavyoitwa - inafanywa ili kukabiliana na mapigano yanayoendelea kati ya wanamgambo wa M23 na makundi yenye silaha katika jimbo hilo pamoja na ghasia yaliyofanywa na M23 kuelekea Sake.
Walinda amani wa Umoja wa Mataifa na wanajeshi wa Kongo wanashika doria katika maeneo muhimu ili kulinda watu na kuzuia ghasia zinazofanywa na M23.
Ujumbe huo pia umeanzisha maeneo ya ulinzi karibu na kituo cha Kitchanga ili kusaidia kulinda watu 25,000 ambao wametafuta hifadhi katika kituo hicho na kuwezesha utoaji wa misaada ya kibinadamu.
Wakati huo huo Rais wa Rwanda Paul Kagame alizungumza na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres juu ya kuongezeka kwa ghasia za silaha na chuki za kikabila mashariki mwa DR Congo, ofisi ya rais ilitangaza.
Rais Kagame alisisitiza kwamba "suluhisho si la kijeshi bali ni la kisiasa".
Hapo awali Rais wa DRC Felix Tshisekedi alitoa wito wa kuondolewa kwa ujumbe wa Umoja wa Mataifa ya kulinda amani ifikapo Desemba 2023.
MONUSCO imekosolewa kwa kushindwa kuwalinda raia dhidi ya mashambulizi kutoka kwa makundi yenye silaha.
Wabunge 17 wa upinzani nchini Zambia watimuliwa kwa muda bungeni
Wabunge 17 wa upinzani nchini Zambia wamezuiliwa kuhudhuria vikao vya bunge kwa siku 30, kufuatia kuvurugu zilizokumba bunge hilo wiki iliyopita.
Wabunge hao walikaidi amri ya kuondoka kwenye kikao hicho baada ya kumshutumu Spika kwa kuwanyima fursa ya kuzungumza.
Akiwasimamisha kazi siku ya Jumanne, Spika Nelly Mutti alitaja mienendo ya wabunge hao kuwa isiyo ya kibunge na ukiukaji wa heshima na uadilifu wa Bunge.
Bi Mutti alisema kuwa uvunjaji wa sheria haupaswi kuchanganyikiwa na uhuru wa kujieleza na kumkaidi Spika ni sawa na kushambulia demokrasia ya kikatiba ya Zambia.
Mbunge Brian Mundubile, kiongozi wa upinzani bungeni, alikuwa miongoni mwa waliosimamishwa kazi.
Wabunge hao wanadai chama tawala kinataka kushinikiza baadhi ya mabadiliko ya katiba bila kuwepo.
Baadhi ya wabunge wa upinzani wameripotiwa kuwasilisha ombi la kuondolewa kwa Spika kwa madai ya usimamizi mbaya wa masuala ya bunge.
Blinken: Tunawezaje kuwa na usitishaji vita wakati Hamas inashikilia mateka?

Chanzo cha picha, Reuters
Blinken anasema Marekani na Israel zinakubaliana kuwa "hakuna kurudi nyuma hadi Oktoba 6 kabla ya mashambulizi ya kinyama ya Hamas".
"Sote tunataka kumaliza mzozo haraka iwezekanavyo na kupunguza mateso ya raia," anasema.
"[Lakini] Wale wanaotaka kusitishwa kwa mapigano mara moja wana wajibu wa kutoa suluhu ya kuzuia kile kilichoifanya - Hamas kuondoka na zaidi ya mateka 200, na uwezekano wa kurudiwa kwa azma yake ya 7 Oktoba tena na tena na tena."
Blinken anaongeza "njia pekee ya kuhakikisha mgogoro huu hautokei tena ni kuanza kuweka mazingira ya amani na usalama wa kudumu".
Raia wa Canada achagua kubaki Gaza ili kurekodi matukio ya vita

Chanzo cha picha, Mansour Shouman
Baba mmoja Mpalestina mwenye uraia wa Canada ameamua kusalia Gaza, licha ya kwamba hatimaye aliruhusiwa kuondoka katika eneo lenye vita.
Mansour Shouman aliambia BBC kwamba anahisi kuwajibika kubaki na kuandika matukio yanayomzunguka.
Alisema watoto wake watano na mkewe ni miongoni mwa raia wa Canada wa kwanza ambao walifanikiwa kuvuka salama hadi Misri siku ya Jumanne.
Kati ya Wakanada 80 walioidhinishwa kuondoka Gaza hadi sasa, 59 wametoka salama.
Global Affairs Canada imesema kuwa wanafahamu zaidi ya raia 400 wa Canada, wakaazi wa kudumu na wanafamilia wao wanaotaka kuondoka kupitia kivuko cha Rafah kuelekea Misri.
Bw Shouman, mshauri wa usimamizi, alisema kuwa kwake kubaki nyuma ni wajibu.
"Mradi watu milioni 2.3 wanateseka, ninaamini kuwa ni wajibu wangu wa kidini, wajibu wangu wa kibinadamu kukaa na kusimulia hadithi kuhusu kile kinachotokea," alisema.
"Naweza kuzungumza Kiingereza, nimeishi Magharibi," alisema Bw Shouman, ambaye tayari amezungumza na vyombo kadhaa vya habari vya kimataifa, ikiwa ni pamoja na BBC.
Bw Shouman ni mhitimu wa Chuo Kikuu cha Malkia huko Kingston, Ontario na Chuo Kikuu cha Calgary huko Alberta, na amefanya kazi kwa miaka kadhaa katika sekta ya mafuta na gesi ya Alberta.
Mwenye asili ya Jerusalem, Bw Shouman alisema kuwa yeye na familia yake walichagua kuhamia maeneo ya Palestina yaliyokaliwa kwa mabavu miaka miwili iliyopita ili watoto wake waishi katika nchi ya mababu zao.
Walichagua kuishi Gaza, alisema, kwa kuwa ni mji alikozaliwa mke wake.
"Tumekuwa tukiishi maisha mazuri sana hapa," Bw Shouman alisema, licha ya machafuko ya muda mrefu katika ukanda wa Gaza.
"Watoto wetu walikuwa wakienda shule za kimataifa," alisema. "Mimi na mke wangu tulikuwa tukifanya kazi. Tulikuwa na marafiki wengi. Msikiti wa eneo hilo ulikuwa mzuri."
Lakini aliongeza yeye na familia yake hawakutarajia kamwe kuwa katikati ya vita vya sasa.
Sasa, Bw Shouman amefanya hospitali katika Khan Younis kuwa nyumba yake, ambapo analala katika chumba kidogo karibu na wadi ya uzazi.
"Kila mtoto mchanga anapozaliwa, mimi husikia habari njema," alisema.
Kivuko cha mpaka cha Rafah kati ya Gaza na Misri kilifunguliwa Jumatano ili kuruhusu idadi ya raia kuondoka. Mamia ya wamiliki wa pasipoti za kigeni, wakiwemo zaidi ya Wamarekani 400, wamevuka mpaka kufikia sasa. Ilikuwa ni fursa yao ya kwanza kufanya hivyo tangu vita kuanza tarehe 7 Oktoba.
Orodha ya wanaoruhusiwa kuvuka imekubaliwa na Misri na Israeli. Kisha, nchi husika zinaarifiwa ili kuhakikisha ziko tayari kupokea raia wao.
Soma zaidi:
'Sasa ni hakika' kwamba 2023 utakuwa mwaka wa joto zaidi

Chanzo cha picha, Getty Images
Sasa ni "hakika" kwamba 2023 – mwaka wa mawimbi ya joto kali, mafuriko na moto - utakuwa wenye joto zaidi katika rekodi, data mpya inapendekeza.
Utabiri huo unafuata halijoto "ya kipekee" ya mwezi Oktoba.
Kiwango cha wastani cha joto cha hewa duniani kilikuwa 0.4C kuliko kiwango cha juu cha awali cha Oktoba 2019, kulingana na huduma ya mabadiliko ya hali ya hewa ya EU.
Ikiendeshwa na utoaji wa hewa ya ukaa na tukio la hali ya hewa la El Niño, huu ulikuwa mwezi wa tano mfululizo wa halijoto iliyorekodiwa.
Hali ya joto kali duniani huenda itaendelea hadi 2024, watafiti wanasema.
Inasemekana kuwa mwaka huu utakuwa wa joto zaidi kuwahi kurekodiwa: miezi miwili iliyopita ya 2023 haina uwezekano mkubwa sana wa kubadili mwelekeo na halijoto ya juu kote ulimwenguni imeendelea hadi Novemba.
Idadi ya siku zinazovuka kiwango muhimu cha ongezeko la joto la 1.5C tayari imefikia kiwango kipya cha juu, kabla ya mwisho wa mwaka.
Julai ilikuwa ya joto sana kwamba unaweza kuwa mwezi wa joto zaidi katika miaka 120,000 , wakati wastani wa joto wa Septemba ulivunja rekodi ya awali kwa "gobsmacking" 0.5C.
Oktoba haikuwa na joto la kawaida kama Septemba lakini bado inavunja rekodi ya mwezi huo kwa kiwango cha "kipekee", kulingana na Huduma ya Mabadiliko ya Tabianchi ya Copernicus.
Mwezi huo ulikuwa wa joto kwa 1.7C kuliko wastani wa kabla ya viwanda - ikimaanisha ikilinganishwa na kipindi kabla ya wanadamu kuanza kuchoma mafuta mengi.
Soma zaidi:
Uingereza, Marekani zatoa tahadhari mpya ya usalama kuhusu Uganda

Chanzo cha picha, Getty Images
Picha: Uganda imerekodi ongezeko la visa vya ukosefu wa usalama katika miezi ya hivi karibuni
Ubalozi wa Uingereza nchini Uganda umeonya kuhusu "tishio la ugaidi linaloongezeka nchini humo, ikiwa ni pamoja na kuwalenga wageni", saa chache baada ya ubalozi wa Marekani kutoa tahadhari kama hiyo.
Misheni zote mbili za kidiplomasia mnamo Jumanne zilionya raia wao dhidi ya kuhudhuria mikusanyiko mikubwa, pamoja na shughuli za ibada.
Pia walitahadharisha dhidi ya kushiriki katika tamasha za muziki na kitamaduni, kabla ya tamasha maarufu la Nyege Nyege mnamo Alhamisi.
Serikali ya Uingereza imewashauri raia wake dhidi ya kutembelea Mbuga ya Kitaifa ya Semuliki na Mbuga ya Kitaifa ya Queen Elizabeth, ambapo wanandoa wa Uingereza na Afrika Kusini na kiongozi wao wa Uganda waliuawa na kundi la wanamgambo wa Allied Democratic Forces (ADF) mwezi uliopita.
Kisha Uingereza ilionya raia wake dhidi ya kutembelea mbuga hiyo maarufu.
Uganda imekumbwa na hali ya ukosefu wa usalama katika miezi ya hivi karibuni.
Mamlaka zilisema zilikomesha mashambulizi mawili tofauti dhidi ya makanisa yaliyofanywa na ADF mnamo Septemba na Oktoba.
Mwezi Juni, wanamgambo wa ADF waliwaua watu 42 katika shule moja magharibi mwa Uganda, mojawapo ya mashambulizi mabaya zaidi ya ADF nchini humo.
Wanandoa wafariki baada ya hoteli yao kuwekwa dawa ya kuua kunguni - ripoti

Chanzo cha picha, Facebook
Wanandoa wa Uingereza wameaga dunia huko Misri walikokuwa wakikaa katika hoteli iliyowekwa dawa ili kuua kunguni – ripoti ya uchunguzi uliofanywa imesema.
John Cooper, 69, na mkewe Susan, 63, wa Burnley, Lancashire, walifariki mnamo 2018 wakiwa likizo huko Hurghada na binti yao na wajukuu watatu.
Uchunguzi uliofanywa ulionyesha kuwa wanandoa hao waliugua katika Hoteli ya Aqua Magic wakati wa masaa ya mapema na kufariki siku iliyofuata.
Uchunguzi huo ulisema kuna uwezekano walipata "maambukizi ya kibaolojia au kukumbana nakemikali zenye sumu".
Mahakama ya Blackburn Coroner ilisikiliza ripoti hiyo ikipendekeza si sumu ya kaboni monoksidi au sumu ya chakula iliyosababisha vifo vya wanandoa hao.
Mtalii kutoka Ujerumani alisema aliripoti kuvamiwa na kunguni katika chumba jirani na Cooper na kisha vyumba vyao vikawekwa dawa, inayojulikana kama Lambda.
Vyumba hivyo viwili vilikuwa na mlango unaoungana lakini ulikuwa umefungwa.
Binti yao, Kelly Ormerod, aliwaelezea wazazi wake kama waliokuwa wenye afya njema na walifurahia likizo yao vizuri.
Bw Cooper, mjenzi, na mke wake, Susan, keshia katika ofisi ya mabadiliko katika wakala wa usafiri wa Thomas Cook, walifurahia likizo kadhaa kwa mwaka.
Mke wa Cooper alikuwa kwenye hoteli hiyo hiyo mnamo Aprili mwaka huo, alielezea hoteli hiyo kuwa ya "kuvutia" na akaamua kurudi na familia yake.
Pia unaweza kusoma:
Maelfu wanatoroka mauaji mapya ya kikabila huko Darfur nchini Sudan

Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Wakimbizi hao hasa ni wanawake na watoto ambao wanatoroka ghasia bila chochote, MSF inasema (picha kutoka maktaba) Kumekuwa na ongezeko kubwa la idadi ya watu wanaotoroka ghasia mpya katika eneo la Darfur nchini Sudan, shirika la usaidizi la matibabu linasema.
Mashuhuda wameshutumu vikosi vya Rapid Support Forces washirika wake kwa kutekeleza mauaji ya kikabila dhidi ya watu wasio Waarabu huko Darfur Magharibi.
RSF haikutoa maoni yake mara moja kuhusu madai hayo lakini awali ilisema haikuhusika katika kile ilichokitaja kuwa "mgogoro wa kikabila".
Watu elfu saba wamevuka mpaka wa Sudan na kuingia Chad katika muda wa siku tatu, Médecins Sans Frontieres (MSF) inasema.
Miongoni mwao ni makumi ya watu waliojeruhiwa. MSF inasema wakimbizi hao ni hasa wanawake na watoto ambao wanatoroka ghasia bila chochote.
Shirika la habari la Reuters linaripoti msururu wa wanaume wamevuka kutoka Darfur kwenda Chad huko Adre, yapata kilomita 27 (maili 17) magharibi mwa mji mkuu wa jimbo, El Geneina.
Baadhi wamewaambia waandishi wa habari kuhusu ukatili unaofanywa katika maeneo ya Darfur Magharibi ambayo yametekwa na RSF.
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi linasema mgogoro wa kibinadamu "usiofikirika" unaendelea nchini Sudan.
Takriban watu milioni sita wamekimbia makazi yao tangu vita kati ya jeshi la Sudan na RSF kuanza katikati ya mwezi Aprili.
Zaidi ya watu 500,000 wamevuka na kuingia Chad, wengi wao kutoka Darfur Magharibi, Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) linasema.
Vikosi hasimu havijapiga hatua kuelekea kusitisha mapigano katika mazungumzo yao ya hivi punde, badala yake walikubali kuwezesha uwasilishaji wa misaada, mwenyeji wa Saudi Arabia alisema Jumanne.
Soma zaidi:
Hofu mamia ya watoto wametumika katika utengenezaji wa picha za uchi

Chanzo cha picha, Guy Hedgecoe/BBC
Mama wa msichana ambaye picha yake ilitumiwa katika utengenezaji wa picha za uchi zilizotengenezwa na Akili Mnemba (AI), anasema mamia ya wazazi wamemwambia watoto wao pia ni waathiriwa.
Binti ya Miriam Al Adib alikuwa mmoja wa watoto kadhaa kutoka kijiji cha Uhispania ambao walikuwa na picha chafu zilizoundwa kwa kutumia picha zao wakiwa wamevalia nadhifu.
Anasema wazazi kote ulimwenguni wanadai watoto wao pia wamelengwa.
Wakfu wa Internet Watch ulisema "haishangazi" kuona tabia hiyo imeenea sana.
Mji wa Almendralejo uligonga vichwa vya habari mwezi Septemba baada ya zaidi ya wasichana 20, wenye umri wa kati ya miaka 11-17 kuwa na picha chafu zilizotengenezwa kutokana na teknolojia ya AI zilizoshirikishwa mtandaoni bila wao kujua.
Bi Al Adib alikuwa miongoni mwa kundi la wazazi waliounda kikundi cha msaada kwa walioathiriwa, jambo ambalo alisema lilisababisha wazazi wengine wengi kuwasiliana naye wakiwa na wasiwasi wao.
"Mamia ya watu wameniandikia wakisema 'umekuwa na bahati gani [kupata usaidizi] kwa sababu kitu kama hiki kimetokea kwetu, kilimtokea binti yangu, au kwangu, na sijapata msaada wowote' ," aliiambia Wales Live.
"Ikiwa msichana yeyote ameathiriwa, tafadhali waambie wazazi wako."
Soma zaidi:
Mpishi wa Ireland amvua Mnigeria kama mpishi aliyeweka rekodi ya dunia

Mpishi mmoja kutoka Ireland ameweka rekodi ya dunia ya kupika bila kukoma, na kuvunja rekodi ya awali kwa zaidi ya saa 24.
Alan Fisher, ambaye anaishi Japani, alipika kwa saa 119 na dakika 57 katika mgahawa wake wenye mandhari ya Kiayalandi huko Matsue, Guinness World Records (GWR) ilisema.
Rekodi mpya ya Bw Fisher ina maana kwamba mpishi wa Nigeria, Hilda Baci ameondolewa kama mshikilizi wa rekodi ya dunia.
Alishinda taji hilo mapema mwaka huu, na kusababisha hisia ya aina yake nchini Nigeria.
Jaribio lake la rekodi ya dunia lililofuatiliwa kwa karibu sana lilizua mshangao katika nchi yake huku watu wakijaribu kujiweka katika vitabu vya rekodi kwa kufanya mambo kama kulia au kuimba bila kukoma.
Rekodi ya Mnigeria huyo ilikuwa saa 93 dakika 11.
"Nilijua tu kwamba ninahitaji kufanya kitu ambacho si cha kawaida ili kuwa maarufu, kuiweka Nigeria kwenye umaarufu, kuwaweka wanawake vijana wa Kiafrika kwenye umaarufu," alisema wakati huo.
"Lata (aliyeshikilia rekodi hapo awali) na mafanikio ya Hilda yalitoa shinikizo," GWR inamnukuu Bw Fisher akisema.
Lakini sasa rekodi ya Bi Baci imebadilishwa na Bw Fisher - ambaye alimenya viazi kilo 300 kama sehemu ya harakati zake za kupikia mfululizo.
“Kadiri uchovu ulivyoanza kunishika ndivyo nilivyokuwa nikipata shida zaidi na zaidi kukaa macho kila nilipoketi kuanza kumenya viazi,” alisema.
"Hali ya kumenya viazi ungekaribia kunilaza. Nilikuwa kwenye ndoto siku ya pili hadi ya mwisho. Niligeuka kumwomba mtu anipe kitu kama ambavyo ningefanya siku yoyote ya kawaida, lakini nikagundua kuwa hakukuwa na mtu hapo. "
Cha kushangaza, Fisher kisha akavunja rekodi ya kuoka bila kukoma kwa muda wa saa 47 dakika 21, GWR ilisema.
Baada ya vipindi vyote viwili vya mapishi ya bila kukoma, Fisher alikuwa ametengeneza mkate wa soda wenye kilo 357 na sehemu 3,360 za chakula.
Bi Baci amepata heshima kubwa katika kusalimisha taji lake.
"Hongera sana Alan Fisher!" aliandika kwenye mtandao wa X, ambao zamani ulijulikana kama Twitter .
"Nimefurahi sana kushikilia rekodi ya kifahari na yenye uzito mkubwa, nitaheshimiwa milele na ninashukuru kwa upendo na usaidizi wote."
Soma zaidi:
Almasi adimu ya samawati yauzwa kwa zaidi ya $40m

Chanzo cha picha, Reuters
Almasi ya buluu adimu sana iliuzwa kwa zaidi ya $40m (£32m) katika mnada wa Christie huko Geneva, mashirika ya habari yalisema.
Almasi ya Bleu Royal yenye umbo la karati 17.61, iliyowekwa kwenye pete, ilipata dola milioni 43.8.
Ni "kito kikubwa zaidi cha ndani kisicho na dosari cha rangi ya samawati" kuwahi kuonekana kuuzwa katika historia ya mnada, kampuni ya Christie ilisema.
Katika sehemu ya mkusanyiko wa kibinafsi kwa miaka 50, ilikuwa mara ya kwanza Bleu Royal kuuzwa kwenye mnada.
"Almasi hii ni miongoni mwa adimu zaidi kupatikana," jumba la mnada lilisema katika taarifa yake.
Kampuni ya Christie ilisema ni almasi tatu tu za rangi ya samawati zaidi ya karati 10 zilizoonekana kuuzwa katika historia yake ya mnada ya miaka 250, mnamo 2010, 2014 na 2016.
Oppenheimer Blue ya karati 14.62 iliuzwa kwa zaidi ya $57 milioni mwaka wa 2016, kulingana na kampuni ya Christie.
"Tumefurahishwa sana," Max Fawcett, mkuu wa vito vya Christie huko Geneva aliiambia AFP kuhusu mauzo ya Jumanne, akiongeza kuwa ni "sehemu ya bei ya juu zaidi ya vito iliyouzwa katika 2023" na mnada wowote ule duniani kote.
Siku ya Jumatatu, Christie iliuza saa ya Rolex iliyokuwa ikivaliwa na mwigizaji wa Marekani Marlon Brando katika filamu ya Apocalypse Now kwa takriban $5m, mashirika ya habari yaliripoti. "M. Brando" ilichorwa kwa mkono nyuma ya saa, Christie ilisema.
Pia, Christie inafanya uuzaji mtandaoni wa mkufu wa lulu unaovaliwa na Audrey Hepburn katika onyesho la mwisho la filamu "Roman Holiday". Uuzaji unafanyika kati ya 3 na 16 Novemba.
Pia unaweza kusoma:
