Ukraine yadai kuhusika na shambulio la makao makuu ya meli za bahari nyeusi za Urusi

Makao makuu ya meli ya Urusi ya Bahari Nyeusi huko Crimea yamepigwa kombora, gavana aliyewekwa na Urusi wa Sevastopol anasema.

Moja kwa moja

  1. Huenda kombora lililotumika kupiga makao makuu ya meli za Bahari nyeusi za Urusi ni la Uingereza au Ukraine

    Shambulio la kombora kwenye Makao Makuu ya meli za Bahari Nyeusi linaonyesha mtindo unaojulikana sasa wa mashambulizi dhidi ya mali za kijeshi za Urusi katika eneo linalokaliwa la Crimea.

    Mojawapo ni kombora la cruise la Storm Shadow la Uingereza, lililorushwa kutoka kwenye ndege ya Ukraine ya Su-24 "Fencer" ya mashambulizi ya ardhini.

    Makombora haya yanaweza kusafiri kwa zaidi ya maili 150 (241km) na yana vifaa vya mlipuko au kichwa cha kivita kinachopenya.

    Kombora jingine linaloshukiwa kutumika ni lile la R-360 Neptune lililoendelezwa na Ukraine kama silaha ya kupambana na meli, imebadilishwa kwa kina na kuboreshwa kwa matukio ya mashambulizi ya ardhini.

    Aprili iliyopita, wakati wa wiki za mwanzo za vita, kombora hilo lilitumiwa kushambulia na kuzamish Meli ya Bahari Nyeusi, Moskva.

    Urusi ilidai kuwa meli hiyo ilizama katika dhoruba baada ya moto.

    Hivi majuzi, Neptune ilitambuliwa kuwa ilitumiwa kuharibu moja ya mifumo ya juu zaidi ya Urusi ya kombora kutoka ardhini hadi angani - S-400 - huko Crimea.

  2. Rais wa zamani wa CAR aliyetoroka ahukumiwa kifungo cha maisha jela

    .
    Maelezo ya picha, Fracois Bozize anaisha nchini Guinea Bissau

    Rais wa zamani wa Jamhuri ya Afrika ya Kati aliye uhamishoni, Francois Bozizé, amehukumiwa kifungo cha maisha jela na mahakama katika mji mkuu wa nchi hiyo, Bangui.

    Mzee huyo mwenye umri wa miaka 76, ambaye sasa anaongoza muungano wa waasi, alipatikana na hatia akiwa ugenini kwa mashtaka yakiwemo uasi na kudhoofisha usalama.

    Ukitolewa siku ya Alhamisi, hukumu hiyo haikutoa maelezo yoyote juu ya muda au uhalifu unaohusika.Zaidi ya wengine 20, wakiwemo wana wawili wa Bw Bozizé, pia walipatikana na hatia bila kuwapo.

    Bw Bozizé alinyakua mamlaka nchini CAR mwaka 2003.

    Alipinduliwa muongo mmoja baadaye, na kusababisha vita vya mwisho vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vimeua maelfu ya watu.Sasa anaishi Guinea-Bissau.

  3. Timbuktu Yazingirwa: Watu 2 wauawa katika shambulio la kombora Mali

    .
    Maelezo ya picha, Kumekuwa na ongezeko la mashambulizi ya wanamgambo kaskazini mwa Mali (picha ya faili)

    Watu wawili wameuawa na wengine watano kujeruhiwa baada ya makombora kurushwa kwenye mji wa kihistoria wa Timbuktu kaskazini mwa Mali, jeshi linasema.

    Wanajeshi walilaumu kile walichokiita "magaidi" kwa shambulio hilo.

    Timbuktu, eneo lililoteuliwa na Umoja wa Mataifa la Urithi wa Dunia, limezingirwa katika wiki za hivi karibuni na wanajihadi, na kuripotiwa kusababisha uhaba mkubwa wa chakula.

    Mwaka wa 2012, eneo hilo lilitekwa na wapiganaji wa Kiislamu na Tuareg, ambao hatimaye walitimuliwa na vikosi vya Ufaransa.

    Hata hivyo, wanajihadi waliendelea kufanya mashambulizi kutoka kambi zao kaskazini zaidi katika Jangwa la Sahara.

    Uasi huo ndio sababu kuu ya jeshi la Mali kunyakua mamlaka mnamo 2020, wakiishutumu serikali ya kiraia kwa kushindwa kutoa usalama.Iliahidi kukomesha mashambulizi ya wanamgambo lakini katika miezi ya hivi karibuni inaonekana yamekuwa yakiongezeka.

    Katika moja ya matukio ya umwagaji damu zaidi, watu 49 walikufa wakati mashua moja kaskazini-mashariki mwa nchi ilipovamiwa wiki mbili zilizopita.

  4. 'Sijaoga kwa siku nyingi, nitafundishaje wanafunzi?'

    .
    Maelezo ya picha, Mwalimu

    Mwalimu mmoja nchini Morocco ameiambia BBC kuwa anahisi hawezi kuwasaidia wanafunzi waliopata kiwewe kutokana na tetemeko kubwa la ardhi lililotokea hivi majuzi.

    Abdelali Mahfodi alizungumza na Newsday kutoka mji wa Amizmiz, wiki mbili baada ya tetemeko kubwa zaidi kuikumba nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika katika zaidi ya miaka 60.

    Kwa vile sehemu kubwa za Amizmiz zimeharibiwa na kuwa vifusi, wengi katika mji huo hawawezi kuoga au kubadilisha nguo zao, Bw Mahfodi aliambia kipindi cha redio cha Newsday.

    Mwalimu huyo wa somo la Kiingereza alisema wanafunzi wake wanahitaji "msaada wa kisaikolojia", lakini "sijabadilisha nguo kwa siku nne, unatarajiaje mtu katika hali hii kujitahidi ili kuwarudisha wanafunzi katika halki yao ya kawaida?

    "Zaidi ya watu 2,900 waliuawa na tetemeko la ardhi la kipimo cha 6.8, lililoikumba Morocco tarehe 8 Septemba.

    Mamlaka ya Morocco imesema dirham 120bn ($11.6bn; £9.4bn) zitatumika kujenga upya maeneo yaliyoathiriwa na kwamba waathiriwa watapokea msaada wa kifedha.Hata hivyo, hakuna muda maalum uliotolewa kwa ajili ya mipango hii.

    Morocco pia imekuwa ikichagua sana kupokea misaada kutoka nje, ikikubali tu kupokea msaada kutoka nchi nne - Qatar, Uhispania, Falme za Kiarabu na Uingereza.

  5. Habari za hivi punde, Askari 'amepotea' hajafa - imesema Wizara ya Ulinzi ya Urusi

    Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema kwamba askari mmoja amepotea, hajafa baada ya shambulio la Ukraine kwenye makao makuu ya jeshi la wanamaji huko Sevastopol.

  6. Habari za hivi punde, Ukraine yadai kuhusika na shambulio la makao makuu ya meli za bahari nyeusi za Urusi

    ..

    Ukraine imedai kuhusika na shambulizi la leo la kombora kwenye makao makuu ya meli ya Urusi ya Bahari Nyeusi huko Crimea.

    Jeshi la Ukraine linasema "limefanikiwa" kupiga kambi ya wanamaji huko Sevastopol, lakini halikutoa maelezo zaidi ya shambulio hilo.

    Makao hayo makuu yaliopo huko Crimea yalipigwa kombora, gavana aliyewekwa na Urusi wa Sevastopol anasema.

    Mwanajeshi mmoja ameuawa katika shambulizi hilo , Wizara ya Ulinzi ya Urusi imethibitisha.

    Katika chapisho lake kwenye mtandao wa Telegraph, Mikhail Razvozhayev anasema kipande kimoja kilianguka karibu na ukumbi wa michezo wa Lunacharsky katika mji mkubwahuko Crimea inayokaliwa na Urusi.

    Anasema huduma za dharura ziko eneo la tukio na taarifa kuhusu waathiriwa zinafafanuliwa.

    Makao hayo yamekuwa yakilengwa na Ukraine kwa sababu za kiutendaji.

    Urusi imerusha makombora kwa Ukraine kutoka kwa meli zake katika Bahari Nyeusi, na kusababisha uharibifu mkubwa.

    Pia imekuwa ikitishia kuziba njia za meli za Bahari Nyeusi ambazo Ukraine imekuwa ikitumia kusafirisha nafaka nje ya nchi.

    Pia kumekuwa na hofu - haswa katika wiki za mwanzo za uvamizi kamili - kwamba Urusi inaweza kutumia meli za kutua kushambulia mikoa ya Odesa ya kusini mwa Ukraine na Mykolayiv kutoka baharini.

    Lakini meli za Bahari Nyeusi pia ni ishara kuu ya uwepo wa kijeshi wa karne nyingi za Urusi katika eneo hilo.

    Urusi imetumia mara kwa mara uwepo wa meli hizo huko Crimea ili kuhalalisha utekaji wake wa mfereji Ukraine, na Vladimir Putin amesema kuwa Urusi ilibidi kuchukua udhibiti wa Crimea mwaka wa 2014 ili kuizuia kuanguka katika mikono ya Magharibi.

    Licha ya madai hayo, meli za Urusi za Bahari Nyeusi na makao yake makuu hazikukabili tishio lolote la kweli wakati huo.

    Lakini sasa, karibu mwaka mmoja na miezi saba katika "operesheni maalum ya kijeshi" ya Putin, jeshi la Ukraine limeweza kushambulia moja kwa moja katikati mwa jeshi la Urusi huko Crimea inayokaliwa.

  7. Martin Odegaard: Arsenal yakubali mkataba mpya wa miaka mitano na nahodha wake

    .

    Nahodha wa Arsenal Martin Odegaard amesaini mkataba mpya wa miaka mitano.Kiungo huyo wa kati wa Norway, 24, amefunga mabao 27 na kutoa asisti 15 katika mechi 112 alizoichezea The Gunners.

    Odegaard alijiunga na klabu hiyo kutoka Real Madrid kwa mkataba wa kudumu Agosti 2021 kwa takriban £30m kufuatia mkopo wa awali.

    Alishiriki katika mechi zote isipokuwa moja kati ya mechi 38 za Ligi Kuu ya Uingereza msimu uliopita huku kikosi cha Mikel Arteta kikimaliza katika nafasi ya pili nyuma ya Manchester City na kumaliza miaka sita ya kutoshiriki Ligi ya Mabingwa.

    "Kusaini mkataba mpya ulikuwa uamuzi rahisi kwangu kwa sababu nyingi," Odegaard alisema.

    "Hasa kile tunachofanya hivi sasa kama klabu ni maalum, na ninataka kuwepo ndani ya mpango huu."Nimefurahishwa sana na kile kitakachokuja hapa. Nimepata mahali ambapo ninaweza kukaa na kupiga simu nyumbani kwangu.

    "Odegaard, ambaye pia ni nahodha wa Norway na amecheza mechi 53, amejitolea kuitumikia Arsenal hadi mwisho wa msimu wa 2027-28.Amefunga mabao matatu katika mechi saba alizoichezea Arsenal msimu huu - ikiwa ni pamoja na bao zuri siku ya Jumatano wakati klabu hiyo ikirejea kwenye michuano ya klabu bingwa barani Ulaya kwa ushindi wa 4-0 dhidi ya PSV Eindhoven.

  8. Habari za hivi punde, Julian Nagelsmann: Kocha wa zamani wa Bayern Munich ateuliwa kuwa meneja wa Ujerumani

    Ujerumani imemteua Julian Nagelsmann kama meneja wa gtimu ya taifa hilo kwa mkataba hadi Julai 2024.

    Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 36 anarithi mikoba ya Hansi Flick, ambaye alifutwa kazi baada ya matokeo duni, na hivyo kupelekea kushindwa kwa mabao 4-1 na Japan katika mechi ya kirafiki mapema mwezi huu.

    Nagelsmann amekuwa nje ya kazi tangu alipofutwa kazi na Bayern Munich mwezi Machi baada ya kuifunza kwa chini ya miaka miwili.

    Mechi yake ya kwanza itakuwa ya kirafiki dhidi ya Marekani mjini Connecticut mwezi ujao.

  9. Mkandarasi wa Marekani ashtakiwa kwa kuipelelezea Ethiopia

    .
    Maelezo ya picha, Idara ya haki nchini Marekani

    Mkandarasi wa Marekani mzaliwa wa Ethiopia ambaye alifanya kazi katika idara ya haki amekamatwa na kushtakiwa kwa kutuma taarifa za siri nchini Ethiopia.

    Abraham Teklu Lemma, 50, anatuhumiwa kuwasilisha taarifa za siri kwa afisa anayehusishwa na idara ya ujasusi ya Ethiopia tangu Agosti mwaka jana, Idara ya Sheria ilisema.

    Idara hiyo haikutaja nchi ya Kiafrika anayodaiwa kuifanyia ujasusi, lakini ilitambuliwa na gazeti la New York Times na vyombo vingine vya habari vya Marekani kuwa ni Ethiopia.

    Anakabiliwa na mashtaka matatu, ikiwa ni pamoja na kukusanya au kutoa taarifa za utetezi kusaidia serikali ya kigeni na kumiliki bila kibali taarifa za ulinzi wa taifa na kuzihifadhi kwa makusudi.

    Bw Abraham, ambaye alikamatwa mwezi uliopita hadi Alhamisi, ni raia wa Marekani mwenye asili ya Ethiopia anayeishi Silver Spring, Maryland.

    Alifanya kazi kama msimamizi wa TEHAMA katika Idara ya Nchi, na kama mchambuzi wa usimamizi wa Idara ya Haki.

    Mshukiwa alikuwa amepewa kibali cha juu cha usalama cha siri na ufikiaji wa mifumo iliyoainishwa ya Marekani.

    Huenda akakabiliwa na hukumu ya kifo iwapo atapatikana na hatia ya ujasusi.

  10. Mwili wa mwanamuziki MohBad wafukuliwa Nigeria

    .
    Maelezo ya picha, Hashtag Justice for Mohbad imekjuwa ikivuma mitandaoni

    Mwili wa nyota wa Afrobeats wa Nigeria MohBad umefukuliwa, polisi katika jiji la Lagos walisema.

    Mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 27, ambaye jina lake halisi lilikuwa Ilerioluwa Aloba, alifariki Jumanne Septemba 12 katika hospitali ya Lagos.

    Mazingira kamili ya kifo chake hayajawekwa wazi na kumekuwa na swito kutoka kwa mashabiki wake kwa uchunguzi.

    “Ufukuaji umekamilika. Uchunguzi wa maiti utaanza," msemaji wa polisi wa jimbo la Lagos Benjamin Hundeyin alitweet.

    Tangu kifo cha mwanamuziki huyo kumekuwa na mikutano katika miji ya kusini mwa Nigeria na huzuni nyingi ikitanda huku watu wakitaka majibu. Hashtag #justiceformohbad imekuwa ikivuma kwenye mitandao ya kijamii.

    Mwimbaji marehemu alikuwa maarufu kwa sauti yake ya baritone na nyimbo zake zikiangazia masuala ya mitaani , wakati mwingine masuala machafu.

  11. Urusi imepiga marufuku kwa muda mauzo ya mafuta kwa nchi nyingi kukabili uhaba

    .

    Urusi imepiga marufuku kwa muda mauzo ya petroli na dizeli kwa nchi zote za nje ya mzunguko wa mataifa manne ya zamani ya Soviet na athari ya haraka ili kuleta utulivu wa soko la ndani, serikali ilisema siku ya Alhamisi.

    Ilisema marufuku hiyo haitumiki kwa mafuta yanayotolewa chini ya makubaliano ya kiserikali kwa wanachama wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Eurasia inayoongozwa na Moscow, ambayo inajumuisha Belarus, Kazakhstan, Armenia na Kyrgyzstan.

    "Vikwazo vya muda vitasaidia kueneza soko la mafuta, ambalo litapunguza bei kwa watumiaji," ilisema taarifa ya serikali.

    Wizara ya nishati ilisema hatua hiyo itazuia usafirishaji usioidhinishwa wa mafuta ya gari.

    Marufuku hiyo ni ya muda usiojulikana na hatua zaidi zitategemea soko, kulingana na Naibu Waziri wa Nishati wa Kwanza wa Urusi Pavel Sorokin.

    "Tunatarajia kuwa soko litakuwa na mabadiliko haraka na ya kutosha. Lakini itategemea soko na matokeo," Sorokin alisema.

    Urusi katika miezi ya hivi karibuni imekumbwa na uhaba wa petroli na dizeli.

    Bei za jumla za mafuta zimepanda, ingawa bei za rejareja zimepunguzwa ili kujaribu kuzipunguza kulingana na mfumuko wa bei rasmi.

    Ugumu huo umekuwa chungu sana katika baadhi ya sehemu za kikapu cha chakula cha kusini mwa Urusi, ambapo mafuta ni muhimu kwa kukusanya mavuno.

    Mgogoro mkubwa unaweza kuwa mbaya kwa Kremlin kama uchaguzi wa rais unakaribia Machi.

  12. Idadi ya vifaru weupe yaongezeka kwa mara ya kwanza kwa miaka 10

    ,

    Idadi ya vifaru weupe wa kusini imeongezeka kwa mara ya kwanza tangu 2012, kikundi kikuu cha uhifadhi kimesema huku kikifichua matokeo ya utafiti wake wa kila mwaka.

    Muungano wa Kimataifa wa Uhifadhi wa Asili na Maliasili (IUCN) ulitangaza Alhamisi kwamba "faru weupe sasa ni takriban 16,803, ongezeko la 5.6%" kutoka mwaka uliopita.

    "Inawezekana, hili ni ongezeko la kwanza la idadi ya faru weupe tangu 2012," iliongeza.

    Idadi ya vifaru weusi pia iliongezeka na kufikia karibu 6,500 mwishoni mwa mwaka jana.

    Hata hivyo, Mwenyekiti wa Kikundi cha Wataalamu wa Vifaru wa Afrika IUCN, Michael Knight alisema licha ya ongezeko la idadi ya faru barani Afrika, uhifadhi bado ni muhimu kwani ujangili unaendelea kuwa mkubwa.

    Mwaka 2022, Afrika ilipoteza faru 561 kutokana na uwindaji haramu, 448 kati yao waliuawa nchini Afrika Kusini.

    Hasara za uwindaji haramu ziliongezeka karibu maradufu nchini Namibia, na kuongezeka kutoka faru 47 waliouawa mwaka 2021 hadi 93 mwaka 2022.

    Nchini Kenya, faru mmoja alikufa kutokana na ujangili, kutoka sita mwaka 2021.

    Mapema mwezi huu kikundi cha uhifadhi cha African Parks kilisema kinapanga kuwaachilia vifaru weupe 2,000 wa kusini baada ya kununua eneo kubwa zaidi duniani uhifadhi wa faru nchini Afrika Kusini.

    Kuna vifaru wawili tu waliosalia wa spishi ndogo nyingine, vifaru weupe wa kaskazini - wote wa kike na wote wapo nchini Kenya.

    Inadhaniwa kuwa uwindaji haramu wa pembe za vifaru ulisababisha kutoweka kwao karibu.

    Pia unaweza kusoma:

    • Shirika lisilo la kiserikali kuwaachilia huru vifaru 2000 waliozuiliwa
    • Jinsi faru wanavyokuzwa kwenye maabara, sayansi inayoweza kuokoa viumbe vilivyo hatarini kutoweka
  13. Tazama: ‘Nilipigwa risasi mguuni katika shambulio la Westgate’

    Maelezo ya video, ‘Nilipigwa risasi mguuni katika shambulio la Westgate’ - Fatima Abdul

    Fatima Abdulrahman ni mmoja kati ya walioathirika na shambulizi la duka kubwa la Westgate jijini Nairobi lililotokea takribani miaka kumi iliyopita.

    Anamsimulia Mwandishi wa BBC @roncliffeodit jinsi anavyoikumbuka siku hiyo na jinsi anavyohisi usalama wake akiwa angali bado anafanya kazi katika jego hilo la kibiashara.

    Video: @frankmavura

  14. Wanafunzi 90 wapewa 'Keki za bangi' Afrika Kusini

    .

    Takriban watoto tisini wa shule ya msingi nchini Afrika Kusini walipelekwa hospitalini baada ya kula keki zinazodhaniwa kutiwa bangi.

    Maafisa walisema wanafunzi walinunua keki hizo kutoka kwa mchuuzi wa barabarani walipokuwa wakielekea Shule ya Msingi ya Pulamadibogo, kaskazini-magharibi mwa Pretoria.

    Walipata kichefuchefu, maumivu ya tumbo na kutapika - na wasichana watatu bado wako hospitalini.

    Watu wawili wamekamatwa na wanakabiliwa na mashtaka ya kujaribu kuua.

    Washukiwa hao, wenye umri wa miaka 21 na 19, watafikishwa mbele ya Mahakama ya Soshanguve siku ya Ijumaa, polisi walisema.

    Idara ya elimu ya mkoa wa Gauteng ilisema walimu waliita gari la wagonjwa baada ya kuona "tabia ya ajabu" kutoka kwa watoto darasani.

    Ilisema tukio hilo limesababisha masikitiko makubwa kwa wazazi ambao walikuwa na wasiwasi juu ya usalama wa watoto wao.

    Polisi, ambao wanaendesha ripoti ya sumu ili kuthibitisha kama bangi ilitumiwa, wanasema zaidi ya wanafunzi 90 walipokea keki hizo na walipata "maumivu makali".

    Wote walitumwa katika vituo vya matibabu vilivyo karibu, na "karibu 87" wameruhusiwa kwenda nyumbani, idara ya elimu ilisema katika taarifa.

    "Ni wanafunzi wasichana watatu pekee ndio wamesalia hospitalini, na bado wanapokea matibabu muhimu ili kurejea katika afya zao," ilisema.

    Pia unaweza kusoma:

  15. Komeni kutufundisha kiongozi wa kijeshi wa Guinea aziambia nchi za magharibi

    ,
    Maelezo ya picha, Kanali Mamady Doumbouya alitetea uingiliaji kati wa kijeshi katika siasa za Afrika

    Kiongozi wa kijeshi wa Guinea, Kanali Mamady Doumbouya, amesema mtindo wa Magharibi wa demokrasia haufanyi kazi barani Afrika, kutetea hatua ya kuingilia kijeshi.

    Aliliambia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York kwamba bara hilo lilikuwa likiteseka kutokana na "mfano wa utawala uliotwikwa juu yetu" na ambao "hauendani na hali halisi ya mambo".

    "Wakati umewadia muache kutusomea na kutufanya kama watoto," aliongeza.

    Kanali Doumbouya alichukua mamlaka katika mapinduzi mwaka wa 2021, na kumuondoa madarakani Rais Alpha Condé.

    Alitetea hatua hiyo katika kikao cha Umoja wa Mataifa akisema ni "kuokoa nchi yetu kutokana na machafuko kamili".

    Wakati huo, habari za mapinduzi zilipokelewa kwa furaha na umati wa watu katika mji mkuu, Conakry, kwani wengi walikuwa wamefarijika kwamba Rais Condé alikuwa ameondolewa.

    Lakini nchi hiyo iliondolewa katika jumuiya ya kikanda, Ecowas, baada ya jeshi kuchukua hatamu, huku viongozi wa kikanda wakitaka kurejeshwa kwa utawala wa kiraia.

    Mwaka jana, Kanali Doumbouya alitoa ratiba ya mpito kwa serikali iliyochaguliwa baada ya mazungumzo na Ecowas lakini hakuna hatua ya haja iliyopigwa katika kuandaa kura, shirika la habari la Reuters linaripoti.

    Guinea ni miongoni mwa nchi kadhaa za magharibi na kati mwa Afrika ambazo zimeshuhudia mapinduzi katika miaka ya hivi karibuni zikiwemo Mali, Burkina Faso, Niger na Gabon.

    Mapinduzi hayo yamelaaniwa vikali na Ecowas, Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa.

  16. 'Sijali kuhusu tuhuma za kujitakasa kimichezo'

    Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman
    Maelezo ya picha, Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman

    Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman anasema hajali shutuma za 'kijitakasa kimichezo'.

    Taifa hilo la Ghuba limeshutumiwa kwa kuwekeza katika michezo na kutumia matukio ya hali ya juu ili kuboresha sifa yake ya kimataifa.

    Mfuko wa Uwekezaji wa Umma wa Saudi Arabia (PIF) uliongoza kuinunua klabu ya Newcastle United mwaka jana na kuzindua LIV Golf.

    "Ikiwa kujitakasa kimishezo kutaongeza Pato la Taifa langu kwa 1%, basi tutaendelea kufanya hivo," Bin Salman alisema.

    Aliiambia Fox News: "Sijali [kuhusu muda]. Nina ukuaji wa 1% katika Pato la Taifa kutokana na michezo na ninalenga 1.5% nyingine.

    Saudi Arabia imekosolewa kwa ukiukaji wake wa haki za binadamu - wanaume 81 walinyongwa siku moja mwaka jana - ukiukwaji wa haki za wanawake, kuharamisha ushoga, kizuizi cha uhuru wa kujieleza na vita nchini Yemen.

    Msimamo wake wa kimataifa uliharibiwa vibaya na mauaji ya 2018 ya Jamal Khashoggi, mwandishi wa habari wa Saudi anayeishi Marekani ambaye alikuwa mkosoaji maarufu wa serikali.

  17. Dawa za kulevya zapatikana chini ya mlango wa shule wa chekechea

    .

    Polisi wamepata "kiasi kikubwa" cha fentanyl, madawa ya kulevya na vifaa vingine vilivyofichwa chini ya mlango wa shule ya chekechea ya New York City ambapo mvulana alipatikana amefariki kutokana na kuathiriwa na dawa ya kulevya aina ya opioidi.

    Picha zilizotolewa na Idara ya Polisi ya Jiji la New York zinaonyesha zaidi ya mifuko kumi na mbili ya plastiki iliyojaa ungaunga wa rangi ya kahawia na nyeupe.

    Uchunguzi unaendelea, polisi walisema.

    Mtoto wa mwaka mmoja alifariki kwa kushukiwa kuwa ametumia dawa za kulevya kupita kiasi katika kituo cha kuangalia watoto siku ya Ijumaa iliyopita.

    Nicholas Dominici alikuwa katika kitalu cha Divino Niño kwa wiki moja tu. Fentanyl alikuwa amefichwa kwenye chumba cha kulala chini ya mkeka alipokuwa akilala, polisi walisema.

    Nicholas Dominici alikuwa katika shule ya chekechea ya Divino Niño kwa wiki moja tu. Dawa ya kulevya ya Fentanyl ilikuwa imefichwa kwenye chumba cha kulala chini ya mkeka alipokuwa akilala, polisi walisema.

    Watoto wengine watatu walilazwa hospitalini baada ya kuathiriwa na dawa hiyo ya kulevya katika kituo hicho.

    Uchunguzi wa mkojo kutoka kwa mmoja wa waathiriwa ulithibitisha uwepo wa dawa hiyo.

    Mmiliki wa shule hiyo, Grei Mendez, 36, na mpangaji wake, Carlisto Acevedo Brito, 41, wanakabiliwa na mashtaka ya serikali ya kumiliki dawa za kulevya kwa nia ya kusambaza na kusababisha kifo, na mashtaka ya kula njama, kulingana na waendesha mashtaka.

    "Tunadai washtakiwa waliwapa sumu watoto wanne, na kumuua mmoja wao, kwa sababu walikuwa wakiendesha biashara ya madawa ya dawa kulevya katika kituo cha kuangalia watoto wadogo," Manhattan Wakili wa Marekani Damien Williams alisema wiki hii.

    Soma zaidi:

  18. Kiongozi wa Sudan aonya vita vinaweza kusambaa hadi kwa mataifa jirani

    .

    Kiongozi wa Sudan ameonya Umoja wa Mataifa kwamba vita vya nchi yake vinaweza kusambaa katika mataifa jirani ya Afrika.

    Katika hotuba yake, Jenerali Abdel Fattah al-Burhan pia aliitaka jumuiya ya kimataifa kuwatambua wapinzani wake, kundi la Rapid Support Forces (RSF), kama kundi la kigaidi.

    Wakati huo huo, kiongozi wa RSF Hamdan Dagalo alisema yuko tayari kwa usitishaji mapigano.

    Tangu Aprili, Sudan imekumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyosababisha vifo vya maelfu ya watu.

    Mnamo 2021, majenerali hao wawili walifanya mapinduzi, lakini katika miezi ya hivi karibuni mzozo wa kuwania madaraka kati yao umesababisha wafuasi wao kuchukua silaha na kukabiliana.

    Akizungumza na Umoja wa Mataifa siku ya Alhamisi, Jenerali Burhan alisema chama chake kiko tayari kwa mazungumzo ya amani, na alitaka "kukomesha vita hivi na kupunguza mateso ya watu wetu", lakini akasema RSF ilikataa.

    Hata hivyo, katika ujumbe adimu wa video kwa Umoja wa Mataifa, mpinzani wake, Jenerali Dagalo - anayejulikana pia kama Hemedti - alisema yuko tayari kushiriki mazungumzo.

    Maelezo zaidi:

  19. Hujambo na karibu katika matangazo ya moja kwa moja leo Ijumaa 22.09.2023.