Ukraine yataka wakazi waondolewe katika mji uliokombolewa

Ukraine imewaamuru baadhi ya wakazi kuondoka Kupiansk, wakati Urusi ikijaribu kuutwaa tena mji uliiouacha mwaka jana.

Moja kwa moja

  1. Ukraine yataka wakazi waondolewe katika mji uliokombolewa

    m

    Ukraine imewaamuru baadhi ya wakazi kuondoka Kupiansk, wakati Urusi ikijaribu kuutwaa tena mji uliiouacha mwaka jana.

    Mamlaka ya eneo la Kharkiv ilisema familia zilizo na watoto na watu "wenye uwezo wa kuhama" lazima waondoke kutokana na mashambulizi ya "mara kwa mara" ya vikosi vya Urusi.

    Urusi iliuteka mji wa kaskazini-mashariki awali katika uvamizi kamili, na Ukraine iliupata tena mwezi Septemba.

    Wakati huohuo, mamluki wa Urusi wanasema "wameuzingira" mji muhimu wa Bakhmut mashariki mwa Ukraine.

    Maelezo hayo yalitolewa na Yevgeniy Prigozhin, ambaye anaongoza kikundi cha kijeshi cha Wagner.

    Katika taarifa yake ya hivi karibuni, jeshi la Ukraine lilisema wanajeshi wa Urusi waliendelea na mashambulizi yao dhidi ya Bakhmut - lakini mashambulizi hayo "yalizuiwa".

    Mapema wiki hii, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alikiri hali ilivyo Bakhmut - takriban kilomita 130 (maili 80) kusini-mashariki mwa Kupiansk - inazidi kuwa "ngumu zaidi na zaidi".

    Huko Kupiansk, utawala wa kijeshi wa mkoa wa Kharkiv ulisema siku ya Alhamisi kuwa amri ya kuwahamisha ilitokana na "hali isiyo thabiti ya usalama" iliyosababishwa na makombora ya Urusi.

    Ilisema waliohamishwa watapewa msaada, ikiwa ni pamoja na malazi, chakula, misaada ya kibinadamu na msaada wa matibabu.

    Raia wengine pia waliruhusiwa kuondoka katika mkoa huo, iliongeza.

    Kabla ya vita, Jiji lilikuwa na idadi ya watu karibu 25,000. Jeshi lilisema watoto 812 kwa sasa wamesajiliwa Kupiansk na wilaya inayozunguka, pamoja na walemavu 724.

    Soma zaidi:

    • Vita vya Ukraine: Jinsi Urusi ilivyochukua eneo la kusini na kisha kukwama
    • Jinsi wakinamama walivyowanasua watoto wao kutoka kwenye uwanja wa vita
  2. Muuza chips ahukumiwa miaka miwili jela kwa kupikia mafuta ya transfoma

    mm

    Mwanaume mmoja ambaye alikuwa anauza chips zilizopikwa kwa mafuta machafu kutoka kwenye transfoma ya umeme amehukumiwa na mahakama nchini Kenya.

    Elijah Mwangi Muthoga alikamatwa zaidi ya mwaka mmoja uliopita akiwa na lita 11 za mafuta hayo katika hoteli anayoendesha katika Kaunti ya Nyandarua.

    Sasa anatakiwa kutumikia kifungo cha miaka miwili jela au kulipa faini ya shilingi 200,000 za Kenya ambazo ni sawa na ($1,570; £1,300).

    Adhabu kali zaidi ya miaka 10 jela au faini ya shilingi milioni 10 ilitolewa kwa Zachary Mwangi Gitau, mwanaume aliyepatikana na hatia ya kumuuzia Muthoga mafuta hayo na kuharibu transfoma ya umeme.

  3. Ubalozi wa Urusi nchini Kenya walaani uungwaji mkono dhidi ya wapenzi wa jinsia moja

    lgbt

    Ubalozi wa Urusi nchini Kenya umekuwa ukionesha kuunga mkono msukumo wa viongozi wa eneo hilo kulaani kile wanachodai ni kukuza utamaduni wa LGBT.

    Hii inafuatia uamuzi wa wiki iliyopita wa Mahakama ya Juu ambao unaruhusu jumuiya ya wapenzi wa jinsia moja kusajili vikundi vya kushawishi nchini Kenya.

    Wafuasi hao wanasema majaji hao waliamini kuwa wanadai haki ya kujumuika kama inavyopewa raia wote, lakini uamuzi huo ulipata upinzani mkubwawapinzani, akiwemo Rais William Ruto na kiongozi wa upinzani Raila Odinga, waliwashutumu majaji hao kwa kuendeleza maadili "yasiyo ya Kiafrika".

    Wengi walitafsiri tofauti hukumu hiyo na kuona ni kama kuipa jumuiya ya LGBT uhuru wa kufunga ndoa nchini Kenya.

    Moja ya ujumbe wa ubalozi huo ulisema: "Vladimir#Putin: "Kadri nitakavyokuwa rais, tutakuwa na ''baba'' na ''mama''".

    Mwingine akasema: "Magharibi taikuja kwa zaidi. Maadili ya kimapokeo yatalindwa, vinginevyo ubinadamu utaangamia."

    Soma zaidi:

    • Ruto: ''Kenya kamwe haiwezi kuruhusu ndoa za wapenzi wa jinsia moja''
  4. Mlinzi wa PSG Achraf Hakimi ashtakiwa kwa madai ya ubakaji

    mm

    Mchezaji wa Paris Saint-Germain Achraf Hakimi amefunguliwa mashtaka ya ubakaji.

    Mwanamke mwenye umri wa miaka 24 amemshutumu Hakimi, ambaye pia ana umri wa miaka 24, kwa kumbaka nyumbani kwake mjini Paris siku ya Jumamosi, Februari 25.

    Wakili wa kimataifa wa Morocco, Fanny Colin, mwanzoni alisisitiza kuwa madai hayo ni "uongo".

    Katika taarifa iliyotolewa mwanzoni mwa mwezi Machi, mwakilishi wa Hakimi pia alithibitisha kuwa mwanasoka huyo "anajitolea kwa mamlaka" kwa uchunguzi.

    Waendesha mashtaka sasa wameithibitishia AFP kwamba amefunguliwa mashtaka.

    Ripoti za awali nchini Ufaransa zilidai Hakimi alifahamishwa tu kuhusu uchunguzi huo takriban dakika 90 kabla ya hafla ya Jumatatu jioni ya ya tuzo za FIFA za The Best Best.

    Beki huyo alitajwa kwenye orodha ya 'FiFPro Men's World11' kwa mafanikio yake uwanjani.

    Kama ilivyo kwa Le Parisien, mshukiwa huyo aliripoti tukio hilo katika kituo cha polisi Jumapili jioni lakini hakutaka kushtaki dhidi ya mwanasoka huyo.

    Hata hivyo ofisi ya mwendesha mashtaka wa umma huko Nanterre, kitongoji cha Paris, ilithibitisha kuwa uchunguzi ulianza.

    PSG ilitoa taarifa kabla ya mashtaka kufunguliwa. Ilisomeka: "Klabu inamuunga mkono mchezaji huyo, ambaye amekanusha vikali shutuma hizo na ana amini mfumo wa haki. Paris St-Germain ni taasisi inayokuza heshima ndani na nje ya uwanja."

    Soma zaidi:

    • Wafahamu wachezaji wa Morocco wanaoweka historia Qatar
    • Waafrika, Waarabu au Amazigh? Mgogoro wa utambulisho wa Morocco
  5. Ales Bialiatski: Mwanaharakati aliyeshinda tuzo ya Nobel ahukumiwa miaka 10 jela

    mm

    Mahakama ya nchini Belarus imemhukumu mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel Ales Bialiatski kifungo cha miaka 10 jela.

    Alikutwa na hatia ya kusafirisha vitu kintume na sheria na kufadhili "vitendo vinavyokiuka sana utaratibu wa umma", shirika la haki za binadamu la Viasna lilisema.

    Wafuasi wa Bw Bialiatski mwenye umri wa miaka 60, wanasema utawala wa kimabavu wa kiongozi wa Belarus Alexander Lukashenko unajaribu kumnyamazisha.

    Bw Bialiatski alikuwa mmoja wa washindi watatu wa Tuzo ya Amani ya Nobel ya 2022.

    Alikamatwa mwaka wa 2021 kufuatia maandamano makubwa dhidi ya uchaguzi uliobishaniwa mwaka uliopita, na kushutumiwa kwa kusafirisha pesa taslimu hadi Belarus ili kufadhili shughuli za upinzani.

    Waandamanaji walikutana na ukatili wa polisi na wakosoaji wa Lukasjenko walikamatwa mara kwa mara na kufungwa jela wakati wa maandamano, ambayo yalianza mnamo 2020.

    Bw Bialiatski alikuwa mahakamani pamoja na wanaharakati wenzake wawili, Valentin Stefanovich na Vladimir Labkovich. Bw Stefanovich alihukumiwa kifungo cha miaka tisa jela, huku Bw Labkovich akipokea miaka saba, kulingana na Viasna, kikundi cha Bw Bialiatski kilichoanzishwa mwaka wa 1996.

    Wote watatu hapo awali walikana mashtaka.

    Soma zaidi:

    • Belarus inaweza kujiunga na vita vya Urusi huko Ukraine?
  6. Manusura wa shambulio la fisi auliwa na ndovu

    f
    Maelezo ya picha, Tsavo ni mbuga kubwa zaidi ya wanyamapori nchini Kenya

    Mwanaume mmoja ambaye alinusurika na shambulio la fisi miaka miwili iliyopita ameuliwa na ndovu katika Kaunti ya Machakos mashariki mwa Kenya, vimeripoti vyombo vya habari nchini humo.

    Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 72, Musili Musembi anasemekana kuwa alikanyagwa na ndovu alipokuwa akitembea kwenda nyumbani kwake Jumatano usiku.

    Mizozo wa binadamu na wanyamapori ni ya kawaida katika maeneo yanayopakana na mbuga ya Wanyama ya Tsavo Mashariki , ambapo wakazi wamekuwa wakilalamika kushambuliwa na kuharibiwa kwa mimea yao na wanyamapori .

    Mwaka 20202, marehemu Musembi alisemekana kupigana na fisi aliyekuwa ameshambulia mifugo wake, ambapo alipata majeraha kwenye mkono wake wa kushoto.

    Alhamisi, wakazi wenye hasira walidai kufanya mkutano na waziri anayehusika na wanyamapori. Pia walitaka Huduma ya Wanyamapori nchini Kenya kumuondosha ndovu huyo.

    Inasemekana polisi walifyatua risasi angani ili kuuchukua mwili wa Bw Musembi, ambao baadaye ulipelekwa katika hifadhi ya maiti ya hospitali ya mji wa Kibwezi.

  7. Uingereza: Wenza kufikishwa mahakamani baada ya mabaki ya mwili wa mtoto mchanga kupatikana

    g

    Constance Marten na Mark Gordon wanatarajiwa kufika mahakamani baada ya mabaki ya mwili wa mtot mchanga kupatikana.

    Mwili wa mtoto mchanga aliyezaliwa kupatikana katika eneo la woodland Brighton nchini Uingereza, baada ya msako mkali siku ya Jumatano.

    Bi Marten, 35 na Gordon, 48, walishitakiwa kwa mauaji ya uzembe mkubwa, pamoja na kuficha kuzaliwa kwa mtoto na kuweka pingamizi kwa mahakama.

    Wanatarajiwa kufikishwa katika mahakama ya hakimu wa mahakama ya Crawley Magistrates Ijumaa.

    Wenza hao walikamatwa kwa mara ya kwanza Jumatatu na kushikiliwa mahabusu kwa ajili ya kuhojiwa, kabla ya kushitakiwa na waendesha mashitaka Alhamisi jioni.

    Awali polisi ilisema Alhamisi kuwa ni "mapema sana" kusema ni lini mtoto alifariki au kutambua alikuwa na jinsia gani.

  8. ISW: Urusi inatumia Nyuklia kama tisho kwa Magharibi

    g

    mkataba wa START na itatumia tisho la nyuklia ili kuzorotesha kasi ya usaidizi wa kijeshi wa Magharibi kwa Ukraine, wataalamu katika taasisi ya stadi za vita (ISW) wameandika katika ripoti yao ya kawaida.

    ISW ilikuwa ikizungumzia mazungumzo baina ya waziri wa mambo ya kigeni wa MarekaniAnthony Blinken na Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov yaliyofanyika katika kikao cha G20 cha mawaziri kilichofanyika mjini Delhi nchini India.

    Blinken alimtaka Lavrov kuondoa marufuku iliyowekewa Marekani ya ushiriki katika mkataba wa START na akaelezea utayari wa kushirikiana na Urusi katika mkakati wa kudhibiti silaha za nyuklia,bila kujali vita vya Ukraine au uhusiano kati ya Marekani na Urusi.

    Kando , Blinken aliitolea wito Urusi kuacha vita nchini Ukraine, kukaa chini katika meza ya mazungumzo na akaitaka imwachilie Mmarekani Paul Whelan aliyefungwa nchini Urusi.

    Hatahivyo, maafisa wa Urusi huenda wasiwe na mazungumzo ya maana kuhusu kufufufliwa kwa ushiriki wa mkataba wa START, wataalamu wameandika.

    "Hakuna uwezekano kwamba Kremlin inatumia hofu ya nyuklia na kufutwa kwa ushiriki wa Urusi katika mkataba wa START kwa matumaini ya kupunguza usaidizi wa Magharibi kwa Ukraine na kupunguza kasi ya usaidizi wa msaada wa kijeshi ," ISW iliandika.

    Urusi na Ukraine: Mengi zaidi:

    • YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
    • UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
    • UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
    • KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
    • ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
    • PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
  9. Wakili wa Marekani apatikana na hatia ya kumuua mke na mwanawe

    B

    Mwanasheria wa South Carolina nchini Marekani amepatikana na hatia ya kumuua mkewe na mtoto wake wa kiume ili kujitenga na uhalifu wake wa kifedha wa mamilioni ya dola.

    Mahakama ilijadili kwa chini ya saa tatu kabla ya kumtia hatiani Alex Murdaugh, 54, kwa makosa mawili ya mauaji mwishoni mwa kesi ya wiki sita.

    Anakabiliwa na kifungo cha miaka 30 jela bila msamaha kwa kila shtaka la mauaji.

    Maggie na Paul Murdaugh walipigwa risasi karibu karibu na banda la mbwa kwenye mali ya familia yao mnamo 7 Juni 2021.

    Alex Murdaugh alisimama bila kusita alipojua hatima yake wakati wa kusikilizwa kwa kesi dhidi yake Alhamisi jioni huko Walterboro.

    "Ushahidi wa hatia ni mwingi," Jaji wa Mahakama ya South Carolina, Clifton Newman alisema alipokuwa akikataa ombi la utetezi la kushtakiwa. Alipanga hukumu yake Ijumaa asubuhi.

    Murdaugh wakati mmoja alikuwa wakili mashuhuri wa kibinafsi katika jimbo hilo, na kwa miongo kadhaa hadi 2006 wanafamilia wake walikuwa wamehudumu kama waendesha mashtaka wakuu katika eneo hilo.

    Lakini mahakama ilifahamishwa kwamba kwa miaka mingi alikuwa akiwaibia washirika wake wa sheria na wateja ili kfadhili uraibu wa dawa za kutuliza maumivu na maisha ya anasa.

    Murdaugh alikana mashtaka ya kumuua mkewe na mwanawe mdogo katika jaribio la kuficha ufisadi wa miaka mingi wa kifedha - udanganyifu ambao yeye mwenyewe alikiri mahakamani.

  10. Marekani kutoa zawadi ya $5m kumpata kiongozi wa wanamgambo wa DR Congo

    Marekani

    Marekani imetangaza zawadi ya hadi dola milioni tano kwa mtu atakayetoa taarifa itakayosaidia kukamatwa kwa Seka Musa Baluku, kiongozi wa wanamgambo wa kundi la Islamic State ADF katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

    Kiongozi anayesakwa wa ADF ni raia wa Uganda ambaye huenda ana umri wa miaka 40 hivi, kulingana na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani.

    "Chini ya uongozi wa Seka Musa Baluku, kikundi hicho kinalenga, kuua, kulemaza, kubaka, na kufanya ukatili mwingine wa kingono na kushiriki katika utekaji nyara wa raia, wakiwemo watoto," mpango wa Idara ya Tuzo kwa Haki ulisema katika taarifa.

    Ilisema "kundi hilo pia huajiri na kuwatumia watoto wakati wa mashambulizi na kazi ya kulazimishwa" katika eneo la Beni mashariki mwa DR Congo.

    Kundi hilo linatuhumiwa kuwaua maelfu ya raia wa Kongo na kutekeleza mashambulizi ya mabomu nchini Uganda.

    Mwaka 2020 pekee, kundi hilo linasemekana kuwaua zaidi ya raia 849, kulingana na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

  11. Nusu ya wakazi wa Dunia kuwa na uzani wa juu zaidi wa mwili mwaka 2035

    g
    Maelezo ya picha, mwanamke akifanya mazoezi nchini Uchina

    Zaidi ya nusu ya watu duniani watakuwa na uzito wa mwili kufikia mwaka 2035 iwapo hatua hazitachukuliwa, limetahadharisha shirikisho la kupambana na unene wa mwili wa kupindukiaduniani, (World Obesity Federation ), limetahadharisha.

    Watu zaidi ya bilioni nne wataathiriwa, huku viwango vikitarajiwa kuongezeka kwa kasi zaidi miongoni mwa watoto, imesema ripoti.

    Nchi zenye kipato cha chini na cha kati barani Afrika na Asia zinatarajiwa kushuhudia ongezeko kubwa zaidi la watu weney uzito wa mwili wa kupindukia.

    Ripoti inabashiri kuwa garama ya unene wa mwili wa kupindukia itapanda na kufikiza zaidi yad ola trilioni 4 za Kimarekani (£3.3tn) kila mwaka ifikapo 2035.

    Ripoti hiyo imeelezea hasa kuongezeka kwa viwango vya uzito wa mwili wa kupindukia miongoni mwa watoto na vijana wadogo wenye umri wa kubalehe, huku viwango vyao vikitarajiwa kuongezeka mara dufu ikilinganishwa na viwango vya mwaka 2020 miongoni mwa wavulana na wasichana.

    Unaweza pia kusoma:

    • Kuna hatari gani kwa mtoto kuzaliwa na uzito mkubwa?
    • Mambo 5 ya kushangaza yanaokusababisha kuongeza kilo
  12. Marekani haiwapi wanajeshi wa Ukraine data kuhusu shabaha nchini Urusi- Pentagon

    Askari

    Msemaji wa Pentagon Jenerali Pat Ryder amesema kuwa Marekani haiwapi wanajeshi wa Ukraine data kuhusu shabaha zinazowezekana kushambuliwa nchini Urusi.

    Akijibu swali la mwandishi wa habari kuhusu shambulio la ndege zisizo na rubani la Februari 28, Ryder alisema ameona ripoti za vyombo vya habari kutoka kwa maafisa wa Urusi kwamba Marekani inaweza kutoa taarifa za kufanya mashambulizi hayo.

    Lakini, kulingana na Ryder, Marekani haitoi habari kama hizo.

    P

    "Kama tulivyosema hapo awali, tunashauriana mara kwa mara na Waukraine kuhusu matumizi sahihi ya vifaa ambavyo tunawapa. Tunaona kwamba bado wanalenga kulinda nchi yao na mapigano ndani ya Ukraine. Hiyo ndiyo tu ninaweza kusema," - alisema jenerali.

    Huku hayo yakijiri baadaye leo Marekani inatarajiwa kutatangaza mpango mpya wa msaada wa kijeshi kwa Ukraine, msemaji wa Baraza la Usalama la Taifa John Kirby alisema.

    Msaada wa kijeshi kwa Ukraine utakuwa mada ya mazungumzo kati ya Rais wa Marekani Joe Biden na Kansela Olaf Scholz wa Ujerumani wakati viongozi hao wawili watakapokutana katika Ikulu ya White House, Kirby alisema.

    Urusi na Ukraine: Mengi zaidi:

    • YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
    • UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
    • UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
    • KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
    • ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
    • PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
  13. Hujambo na Karibu.