Watu kadhaa wafariki baada ya mashambulizi ya ndege zisizo na rubani na makombora kote Ukraine

Ndege hizo zisizo na rubani, zinazoripotiwa kutumwa kwa Urusi na Iran, zinaweza kuruka kwa saa kadhaa kabla ya kuzama kwenye shabaha na kulipuka.

Moja kwa moja

  1. Mpaka hapa tumefika mwisho wa matangazo ya moja kwa moja BBC Swahili

  2. Jengo lashika moto katika mji wa Yeysk, Urusi baada ya ndege ya kijeshi kuanguka

    TH

    Ndege ya kijeshi imeanguka katika eneo la makazi ya watu katika mji wa Yeysk kusini mwa Urusi.

    Picha ambazo hazijathibitishwa za tukio hilo zilionyesha moto mkubwa ukiteketeza jengo kubwa la ghorofa .

    Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema ndege hiyo aina ya Su-34, ilikuwa kwenye safari ya mafunzo wakati injini yake moja iliposhika moto.

    Bado hakuna habari kuhusu majeruhi, lakini ambulensi na vyombo vya moto vilionekana kwenye eneo la tukio.

  3. Ushindi wa Tanzania katika kombe la dunia kubadilisha taswira ya soka la wanawake

    mm

    Kocha wa Tanzania, Bakari Shime anaamini kuwa mafanikio katika Kombe la Dunia la Wanawake wenye umri wa chini ya miaka 17 nchini India unaweza kuleta "mabadiliko" katika nchi ambayo mchezo wa wanawake bado haujakubalika na watu wengi.

    Serengeti Girls, timu ya kwanza kutoka Tanzania kuwahi kushiriki michuano ya kimataifa, ilizinduka baada ya Japan kuifunga mabao 4-0 na baadae kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya mabingwa wa zamani Ufaransa Jumamosi.

    Wachezaji wa kwanza wanaweza kufuzu kihistoria kwa awamu ya muondoano ya shindano hilo watakapokabiliana na timu ya mwisho ya Kundi D ya Canada siku ya Jumanne. "Kufika robo fainali itakuwa mafanikio makubwa katika historia yetu na katika nchi yetu," Shime aliambia BBC Sport Africa.

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

    "Tukushinda Jumanne itakuwa hatua ya mabadiliko kwa soka la wanawake nchini Tanzania. "Shirikisho na serikali wanasukuma mpira wa miguu wa wanawake kwa sababu wameona timu za wanawake zinaweza kufanya vizuri zaidi kuliko wanaume, tunatarajia mashindano haya yataongeza morali ya watu kuwaunga mkono nchini Tanzania.

    " Mwaka jana, Rais wa kwanza mwanamke wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alikosolewa vikali kwa kusema wanasoka wa kike wa nchi hiyo hawakuwa na mvuto.

    wasichana

    Katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki, ambapo 63% ya wakazi wanajitambulisha kuwa Wakristo na 34% ni Waislamu, mitazamo dhidi ya wasichana wanaocheza mpira mara nyingi inabaki kuwa ya wasiwasi.

    "Katika baadhi ya maeneo ya nchi yetu, wazazi hawaruhusu wasichana kucheza soka," Shime alisema.

    "Lazima uwashawishi wazazi kwa sababu Uislamu hauruhusu wasichana kucheza na kaptula.

    Timu yetu mara nyingi huvaa suruali ndefu katika mazoezi na lazima uwahakikishie wazazi kwamba wasichana watafunika viungo vyao vya mwili kulingana na dini zao."

    Taifa moja la Afrika tayari limefuzu kwa robo-fainali, baada ya Nigeria kuwafunga Chile 2-1 Jumatatu na kufuzu kama washindi wa pili wa Kundi B.

  4. Kenya imezipa kampuni za simu siku 60 kusajili kadi zote za simu

    th

    Mamlaka ya Mawasiliano nchini Kenya imezipa kampuni za simu za mkononi siku 60 kuhakikisha wateja wote wamesajili kadi za simu zao.

    Haya yanajiri baada ya watoa huduma hao kuwazimia huduma wateja ambao hawajasajiliwa siku mbili zilizopita huku makataa ya kujisajili yakiisha.

    Mamlaka ya Mawasiliano inatahadharisha kuwa muda wa siku 60 sio nyongeza nyingine kwa wale ambao bado hawajasajili kadi zao za simu.

    Inasema katika kipindi hiki kadi zote ambazo hazijasajiliwa zinapaswa kuzimwa hadi wamiliki wao watakapothibitisha maelezo ya umiliki wao, huku kampuni zikitarajiwa kuhakikisha uzingatiaji wa sheria hiyo kwa 100%.

    Mamlaka imesema kuwa kampuni yoyote ya simu itakayoshindwa kutekeleza agizo hilo itatozwa faini ya 0.5% ya mauzo yake yote kwa mwaka.Mnamo Aprili, Mamlaka iliongeza muda wa usajili kwa miezi 6 iliyoisha wikendi iliyopita.

    Zikiwa zimesalia siku mbili tu kabla ya tarehe hii ya mwisho, watumiaji milioni 53 walikuwa wamethibitisha maelezo yao ya usajili, na kuwaacha zaidi ya milioni 10 kwenye hatari ya kuzimiwa simu zao

  5. Unyanyasaji waua mabinti 85 wa Kenya Uarabuni

      • Author, Grace Kuria
      • Nafasi, BBC News
    kenya

    Wasichana 85 wa Kenya wamepoteza maisha katika muda wa siku 90 zilizopita, na takriban 1,000 kurejeshwa makwao, hasa kutoka Saudi Arabia.

    Haya yalibainishwa na mteule wa Kenya katika nafasi ya Waziri wa Masuala ya Kigeni Dkt. Alfred Mutua, ambaye alisema wasichana hao walinyanyaswa walipokuwa wakitafuta kazi.

    Dkt. Mutua alikuwa akijibu swali wakati alipokuwa akipigiwa kura Bungeni, kuhusu hatua ambazo angeweka kuhakikisha wafanyakazi hao wahamiaji wamepewa mikataba katika ajira, wanalindwa, na wanafurahia kikamilifu haki wanazopewa.

    "Nimeangalia suala hili, na nimeona kushindwa kwa utaratibu katika mifumo, kutoka kwa jinsi wanavyoajiriwa hapa .... na jinsi wanavyoruhusiwa kufanya kazi wanapofika Saudi Arabia na nchi nyingine."

    Mteule huyo aliahidi kuwa iwapo ataidhinishwa, atashirikiana na mamlaka husika, kuruhusu Kurugenzi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai kusafiri naye hadi Saudi Arabia, kuchunguza kila kifo kilichotokea.

    "Ili kila mtu aliyehusika katika vifo hivyo ashtakiwe."

    Mnamo 2021, Wizara ya Mambo ya Nje ya Kenya ilisema Wakenya 89, wengi wao wakiwa wafanyakazi wa nyumbani walifariki nchini Saudi Arabia katika miaka miwili iliyopita. Hata hivyo vilihusishwa na mshtuko wa moyo.

    • Dhuluma wanazopitia uarabuni wafanyakazi wa nyumbani kutoka Tanzania
    • Madaktari Uganda wathibitisha Judith kutolewa figo akiwa kwa mwajiri wake Saudi Arabia
    • WARIDI WA BBC:‘Najuta kwenda Saudia Arabia kufanya kazi za nyumbani’
  6. Lutfunisa Kwandwalla: Mwili wa mwanachama wa dhehebu la siri kufukuliwa na kuchunguzwa Kenya

    v
    Maelezo ya picha, Lutfunisa Kwandwalla mwenye umri wa miaka arobaini na nne alikuwa kutoka Leicester

    Familia ya mwanamke wa Uingereza ambaye anadaiwa alifariki baada ya kujiunga na dhehebu moja nchini Kenya imepata haki ya kuufukua mwili wake.

    Wakati Lutfunisa Kwandwalla alifariki mwaka wa 2020 katika nyumba ya kiongozi wa kiroho huko Mombasa, maafisa walilaumu "sababu za asili" na hakuna mtu aliyekamatwa.

    Lakini familia yake inaamini kuwa aliuawa na wameshinda ombi la mahakama la uchunguzi wa maiti, kwa matumaini ya kuthibitisha hilo."Amri ya mahakama ni ushindi kwa haki’ - kaka yake Imran Admani aliambia BBC."Ilikuwa wakati wa hisia na wakati wa furaha.

    "Bi Kwandwalla, 44, alikuwa kutoka Leicester nchini Uingereza na alifika Kenya kama mtalii mnamo Agosti 2019 kutembelea watu wa familia ya mumewe, kaka yake anasema.

    th
    Maelezo ya picha, Kaka yake Imran Admani anasema familia inahitaji majibu

    Alitarajiwa kurejea Uingereza miezi kadhaa baadaye, lakini vikwazo vya usafiri vya janga la Corona vilimzuia kuondoka Kenya.Wakati huo alijiunga na dhehebu lenye utata katika mji wa pwani wa Mombasa, kulingana na familia yake.Wanadai aliuawa na mwili wake kuzikwa haraka ili kuficha ushahidi.

    Kufuatia uamuzi wa wiki jana katika mahakama moja mjini Mombasa, mamlaka ya Kenya sasa lazima ifukue mwili wa Bi Kwandwalla na kufanya uchunguzi wa maiti ili kuthibitisha sababu ya kifo chake.Hakuna mtu aliyekamatwa kuhusiana na kifo hicho na rekodi za polisi zinaonyesha kuwa kwa sasa hakuna uchunguzi unaoendelea.

    Lakini familia ya Bi Kwandwalla iliambia BBC kwamba uchunguzi huo wa maiti ulikuwa hatua ya kwanza ya kuwafanya watamatishe hali ya majonzi.

    "Hatua inayofuata ya kubaini kama ilikuwa hila ni kufika kwenye mwili. Tunatumai hivi karibuni tutajua kilichompata," Bw Admani alisema.

  7. Mataifa ya EU kutoa mafunzo kwa wanajeshi wa Ukraine

    nn

    Mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya wamekubali kutoa mafunzo ya kijeshi kwa hadi wanajeshi 15,000 wa Ukraine.

    Misheni ya Usaidizi wa Kijeshi imetiwa saini katika mkutano huko Luxembourg leo, kwa gharama ya zaidi ya €100m ($97.5m, £86m).

    Mpango huo utafanyika katika eneo la Umoja wa Ulaya kwa muda wa miaka miwili ya awali - kutoa "mafunzo ya mtu binafsi, ya pamoja na maalum" kwa vikosi vya kijeshi vya Ukraine.

    Mwanadiplomasia mmoja alipendekeza itachukua "wiki chache zaidi" kabla ya misheni hiyo kutumwa.

    Walisema hiyo ni kwa sababu ilikuwa "ya kipekee" na kwamba maelezo ya uendeshaji bado yalihitaji kufanyiwa kazi.

    Mkuu wa Masuala ya Kigeni wa Umoja wa Ulaya, Josep Borrell, alisema uamuzi huo ni "uthibitisho wa wazi" kwamba EU itasimama na Ukraine "kwa muda mrefu kama inahitajika".

    Poland inatarajiwa kuwa mwenyeji wa mafunzo hayo mengi huku makao makuu ya uendeshaji yatakuwa Brussels.

  8. Tazama: Polisi wa Ukraine waiangusha ndege isiyo na rubani ya Kamikaze

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

    Picha za video sasa zimeibuka zikionyesha maafisa wa polisi wa Ukraine wakitumia bunduki zao za kivita kuiangusha ndege ya Urusi isiyo na rubani.

    Katika video hiyo, mmoja wa maofisa anasikika akisema kwa Kiukreni: "Piga risasi, ikiwa [droni] zinakuja."

    Maafisa wengine kisha wanapiga kelele: "Hapa, hapa, hapo juu!" kabla ya risasi nyingi kufyatuliwa.

    Kelele kubwa zinasikika, kabla ya kile kinachoonekana kama dronikuanguka karibu na kulipuka.

    Video hiyo ina alama ya "polisi wa doria" wa Ukraine, na mshauri wa wizara ya mambo ya ndani ya Ukraine Anton Herashchenko anasema "ndege hiyo isiyo na rubani ya Iran" ilidunguliwa.

    Mahali halisi ya kile kinachoonekana kama eneo kuu la miji haikujulikana mara moja, na picha hiyo haijathibitishwa kwa njia huru .

  9. Baba ataka kumpiga mshukiwa wa mauaji ya binti yake, Mahakamani

    Mwanaume mmoja nchini Afrika Kusini amerekodiwa akijaribu kumshambulia mshukiwa anayetuhumiwa kumuua binti yake wa miaka minne.

    Binti huyo, Bokgabo Poo, alitoweka wiki iliyopita kabla ya kuthibitishwa kufariki.

    Ntokozo Zikhali mwenye umri wa miaka 30 ameshtakiwa kwa utekaji nyara, ubakaji na mauaji ya mtoto huyo, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya ndani.

    Haijulikani ikiwa amepata dhamana. Alifika mahakamani leo,Jumatatu, na kesi ilipokuwa karibu kukamilizika kusikilizwa, baba yake msichana huyo aliruka kutoka kwenye kiti chake na kujaribu kumshika.

    Baba huyo alisikika akipiga kelele "umemuua binti yangu", kulingana na tovuti ya habari ya Times Live.

    Bw Zikhali atarudi mahakamani wiki ijayo kwa ajili ya kusikilizwa kwa dhamana. Vyombo vya habari vimesambaza picha za vurugu zilizotokea katika chumba cha mahakama huku mshukiwa akiongozwa kwa amri:

    Ruka YouTube ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje Mitandao ya kijamii inaweza beba matangazo

    Mwisho wa YouTube ujumbe

  10. EU yaangalia usambazaji wa Iran wa ndege zisizo na rubani kwa Urusi

    th

    Mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya wanaokutana leo mjini Luxembourg watajadili kuhusu uhamisho wa ndege zisizo na rubani za Iran kwenda Russia na vikwazo vipya pia vinaweza kuwa mezani.

    Mazungumzo hayo yatahusisha waziri wa mambo ya nje wa Ukraine na yanakuja wakati Umoja wa Ulaya ukijiandaa kuidhinisha vikwazo dhidi ya Iran kutokana na ukandamizaji wake wa ghasia dhidi ya maandamano yaliyochochewa na kifo cha Mahsa Amini mwenye umri wa miaka 22.

    Mwanadiplomasia mkuu wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell anasema umoja huo unatafuta "ushahidi halisi" wa kuhusika kwa Iran katika vita vya Urusi dhidi ya Ukraine. Lakini mawaziri kadhaa wa mambo ya nje tayari wameonyesha wana uhakika Iran imekuwa ikiipatia Urusi ndege zisizo na rubani.

    Waziri wa mashauri ya kigeni wa Denmark Jeppe Kofod alisema: "Tunachoweza kuona sasa: Ndege zisizo na rubani za Iran zinatumika kushambulia katikati ya Kyiv, huu ni ukatili."

    Wiki iliyopita, Rais Zelensky alisema Urusi ilitumia "ndege zisizo na rubani" zilizotengenezwa na Iran kama sehemu ya mfululizo wa mashambulizi ya nchi nzima ambayo yalisababisha vifo vya watu 19. Na siku ya Jumapili, gazeti la The Washington Post lilinukuu vyanzo vilisema Iran inapanga kusambaza makombora ya balestiki ya Fateh-110 na Zolfaghar kwa Urusi.

    Vyombo vya habari vya Urusi bado havijatoa maoni yoyote kuhusu ripoti hiyo, na Tehran imekanusha kuhusika kwa vyovyote vile.

    Lakini waziri mmoja wa Israel alisema hatua hiyo inamaanisha Israel ilipaswa kushiriki katika kuunga mkono Ukraine.

    "Hakuna tena shaka yoyote ambapo Israeli inapaswa kusimama katika mzozo huu wa umwagaji damu," Waziri wa Masuala ya wageni wa Israeli Nachman Shai aliandika kwenye Twitter.

  11. Chanjo za majaribio za Ebola zinaweza kuongezwa Uganda - ripoti

    ebola

    Zaidi ya dozi 20,000 za chanjo za majaribio dhidi ya Ebola ya aina ya Sudan zinaweza kutengenezwa na Taasisi ya Serum ya India na kutumika katika majaribio kuona kama zinaweza kukabiliana na mlipuko wa sasa nchini Uganda, shirika la habari la Reuters limeripoti.

    Chanjo zimetumwa dhidi ya aina ya virusi vya Zaire katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, lakini hakuna chanjo iliyothibitishwa yenye ufanisi dhidi ya aina ya Sudan.

    Watu 19 wamefariki mpaka sasa na kumekuwa na visa 54 vilivyorekodiwa tangu mlipuko huo uanze mwezi uliopita.

    Mwishoni mwa wiki, Rais Yoweri Museveni aliweka kizuizi katika wilaya mbili ambako mlipuko huo umeenea zaidi.

    "Hizi ni hatua za muda za kudhibiti kuenea kwa Ebola," alisema katika hotuba yake kwenye televisheni.

    Watafiti katika Chuo Kikuu cha Oxford wanaofanya kazi na Taasisi ya Serum - mtengenezaji mkubwa zaidi wa chanjo ulimwenguni - umeona chanjo yao ya majaribio, ambayo inaonekana kufanya kazi katika majaribio ya mapema, sasa inaweza kutengenezwa, Reuters inaripoti.

    Kumekuwa na kufadhaika juu ya uhaba wa fedha kwa ajili ya maendeleo ya chanjo, shirika hilo la habari linaongeza kueleza.

    • Mpelelezi wa virusi ambaye aligundua Ebola mwaka 1976
    • Mlipuko wa Ebola Uganda: Kwa nini hali ni mbaya?
  12. Cocaine iliyosukumwa na maji hadi ufukweni Uingereza yenye thamani ya £42m

    th

    Mabunda ya dawa za kulevya ambayo yalisogeshwa ufukweni yana thamani ya takriban £42m, polisi wamesema.

    Idadi kubwa ya mifuko nyeusi iliyofungwa kwenye beseni za plastiki ilipatikana na wapita njia kwenye ufukwe wa Tan-y-Bwlch karibu na Aberystwyth, Ceredigion, tarehe 1 Oktoba.

    Vifurushi zaidi vilipatikana baadaye na vyote vinakisiwa kuwa na kokeini.

    Polisi wa Dyfed-Powys walisema kuwa shehena hiyo na uzito wa kilo 1,200 na kuwaonya wananchi kutogusa tena wawasiliane na jeshi.

    Taarifa ilisema: "Kazi ya uchunguzi inaendelea kuhusu shehena iliyopatikana kwenye mifuko, lakini tunaamini kuwa kokeini yenye uzito wa takriban kilo 1,200. Kiasi hiki kingekuwa na thamani ya jumla ya takriban pauni milioni 42.

    "Uchunguzi wetu unaendelea na tunasisitiza kwa umma kwamba ikiwa watapata chochote cha kutilia shaka kwenye fukwe, yaliyomo yasiguswe na polisi wanapaswa kufahamishwa mara moja."

  13. Japan kuchunguza kikundi cha kidini kilichohusishwa na mauaji ya Abe

    Fumio Kishida ameagiza uchunguzi ufanyike katika kanisa hilo licha ya kwamba awali, hilo lililonekana kusitasita
    Maelezo ya picha, Fumio Kishida ameagiza uchunguzi ufanyike katika kanisa hilo licha ya kwamba awali, hilo lililonekana kusitasita

    Waziri mkuu wa Japan ameagiza uchunguzi ufanyike kuhusu kanisa la Muungano, kundi la kidini ambalo limeangaziwa baada ya kuuawa kwa kiongozi wa zamani Shinzo Abe.

    Mshukiwa wake aliyemuua alisema kanisa lilimfilisi mamake na kumlaumu Abe kwa madai ya kulikuza.

    Uchunguzi wa dhehebu hilo la kidini katika wiki zilizofuata ulibaini kuwa lilikuwa na uhusiano na wabunge wengi wa serikali.

    Kashfa hiyo ilimlazimu kiongozi Fumio Kishida kuomba radhi.

    Siku ya Jumatatu alikubali kufanya uchunguzi wa serikali kuhusu kanisa hilo - baada ya hapo awali kupinga wito wa uchunguzi kama huo.

    Alisema "anachukulia kwa uzito" shutuma kwamba kanisa hilo limeharibu familia na kuwanyonya wafuasi wake kwa pesa.

    Kanisa hilo hapo awali lilisema limekashifiwa isivyo juu ya mauaji ya Abe, ambalo lililaani kitendo hicho.

    Kesi kadhaa zimeletwa dhidi kanisa hilo na wafuasi wake wa awali.

    Bw Kishida alikiri "waathiriwa ni wengi" wa kanisa hilo na kusema "juhudi za kuwasaidia bado hazitoshi".

    Wachambuzi wa masuala ya kisiasa nchini walitaja tangazo la Bw Kishida kama nia ya kurejesha imani ya umma.

    Kiwango chake cha kuungwa mkono kilishuka katika miezi iliyopita, huku habari zikiibuka kuhusu uhusiano wa chama chake na Kanisa.

    Chama cha Liberal Democratic Party - ambacho Bw Kishida ni mkuu wake - uchunguzi uligundua wabunge 179 kati ya 379 walishirikiana na Kanisa hilo la Muungano.

    Kufuatia ripoti hiyo, Bw Kishida aliomba msamaha na kusema amewataka wabunge wa chama chake kukata uhusiano wote na dhehebu hilo.

    Pia alisisitiza kuwa hakuwa na uhusiano wa kibinafsi na kikundi hicho.

    Kanisa hilo la Muungano, lilianzia Korea Kusini, na kuingia Japani katika miaka ya 1960 ambapo lilikuza uhusiano na wanasiasa ili kukuza msingi na sifa ya wafuasi wake, watafiti wanasema.

    Soma zaidi:

  14. Jeshi la Ukraine latungua makombora 26 ya Urusi

    w

    Jeshi la Ukraine limeharibu ndege 26 za Urusi zisizo na rubani eneo la kusini usiku kucha, Hii ilitangazwa leo kwenye anga ya telethon ya kitaifa na msemaji wa vikosi vya anga vya Ukraine Yuriy Ignat.

    Tunazungumza juu ya drones za Irani za Shahed-136 (baada ya kununuliwa na jeshi la Urusi, zilipewa jina la Geran). Kulingana na Ignat, haya yote yalitokea "katika eneo la uwajibikaji la Amri ya Anga Kusini" - bila kutaja mikoa.

    Mapema leo, mitandao kadhaa ya telegram ya Ukraine iliripoti kuwa wanajeshi wa Urusi walishambulia maeneo ya Zaporozhye na Odessa kwa kutumia ndege zisizo na rubani.

    Hakuna data kamili juu ya matokeo ya shambulio hili, pamoja na matokeo ya shambulio la ndege isiyo na rubani huko Kyiv mapema asubuhi ya leo.

    Soma zaidi:

  15. Kiongozi wa CDC Afrika 'abaguliwa' uwanja wa ndege Ujerumani

    w

    Kaimu mkuu wa Vituo vya Afrika vya Kudhibiti Magonjwa (CDC), Ahmed Ogwell Ouma, amerejea Kenya baada ya kudaiwa kubaguliwa mwishoni mwa juma na maafisa wa uhamiaji katika uwanja wa ndege wa Frankfurt nchini Ujerumani.

    Alisema maafisa wa uhamiaji "walijua nataka kusalia kinyume cha sheria".

    Dk Ogwell alipaswa kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa Afya Duniani ambao ulifanyika Jumamosi na Jumapili katika mji mkuu wa Ujerumani, Berlin.

    Kufuatia tukio hilo, alisema "mahudhurio yake yalikuwa ya shaka" licha ya kuwa na visa na mwaliko wa mkutano huo.

    Siku ya Jumatatu alituma ujumbe kwenye Twitter: "Nimerejea salama barani Afrika nyumbani kwa wanadamu wanaostahimili zaidi ninaowajua."

    Aliongeza: "Viza mara nyingi haina maana unapokuwa umebeba pasipoti ya Kiafrika - ya kawaida au ya kidiplomasia."

    Uwanja wa ndege wa Frankfurt uliomba radhi kwa tukio la Jumamosi.

    "Kama uwanja wa ndege wa kimataifa, tunakaribisha abiria wote na hatuvumilii aina yoyote ya ubaguzi. Tungependa kuwa na taarifa zaidi kuhusu tukio hili," iliandika kwenye Twitter baada ya Dkt Ogwell kushiriki masaibu yake katika uwanja wa ndege.

  16. Mbappe: Taarifa ya kuondoka PSG hata mimi nimeshtuka

    w

    Mshambulizi Kylian Mbappe anasema "hakuwahi kuomba kuondoka" Paris St-Germain huku kukiwa na ripoti kwamba alitaka kuhama mji mkuu wa Ufaransa mwezi Januari. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 23 alitia saini mkataba mpya wa miaka mitatu na klabu hiyo mwezi Mei. Mbappe, mshindi wa Kombe la Dunia 2018, hapo awali alikuwa akihusishwa pakubwa na kuhamia Real Madrid. "Nina furaha sana," Mbappe alisema baada ya kutengeneza bao la ushindi la Neymar katika ushindi wa 1-0 dhidi ya Marseille Jumapili.

    "Sijawahi kuomba kuondoka Januari." anasema Mbappe Ripoti kwamba Mbappe alitaka kuondoka katika klabu hiyo ziliibuka kabla ya mechi ya PSG ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Benfica siku ya Jumanne.

    "Sikuelewa kwa nini taarifa hiyo ilitoka siku ya mchezo. Nilishtuka kama kila mtu," Mbappe alidai. "Watu wanaweza kufikiri nilihusika lakini sikuhusika kabisa."

    Soma zaidi:

  17. Vita vya Ukraine: Milipuko yasikika Kyiv huku Ukraine ikiripoti mashambulio ya ndege zisizo na rubani za kamikaze

    w

    Mji mkuu wa Ukraine, Kyiv, umekumbwa na milipuko takriban minne - huku mshauri wa rais akilaumu ndege zisizo na rubani za Kamikaze zilizotumwa na Urusi.

    "Inaonyesha kukata tamaa kwao, alisema Andriy Yermak, mkuu wa wafanyakazi wa Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky".

    Na katika mji wa bandari wa Mykolaiv, matangi ya mafuta ya alizeti yalichomwa moto na ndege zisizo na rubani kama hizo hizo, alisema meya wa jiji hilo.

    Meya Vitalii Klitschko alisema majengo ya makazi katikati mwa eneo la Shevchenkivskiy yameharibiwa.

    Andriy Yermak, mkuu wa ofisi ya Rais Zelensky, alisema mashambulizi hayo yalitokana na kile kinachoitwa ndege zisizo na rubani za kamikaze.

    Hatua hii inakuja wiki moja baada ya mji mkuu kupigwa na makombora kadhaa ya Urusi katika saa ya haraka, katika shambulio la kitaifa ambalo lilisababisha vifo vya watu 19. Milipuko hiyo siku ya Jumatatu ilitokea mwendo wa saa 07:00 kwa saa za huko (04:00 GMT), alisema mwandishi wa BBC Paul Adams, ambaye yuko mjini humo.

    Akiandika kwenye mtandao wa kijamii wa Telegram, Bw Klitschko alisema walikuwa katika wilaya ya Shevchenkivskiy, ambayo ilikumbwa na mashambulio kadhaa wiki iliyopita.

    Alisema waokoaji walikuwa kwenye tovuti, na aliwaambia wakazi kukaa katika makazi ya mashambulizi ya anga. Bw Yermak alisema kwenye Telegram kwamba shambulio hilo lilitokana na ndege zisizo na rubani za kamikaze, na kwamba Ukraine inahitaji mifumo zaidi ya ulinzi wa anga "haraka iwezekanavyo".

    Ndege hizo zisizo na rubani, zinazoripotiwa kutumwa kwa Urusi na Iran, zinaweza kuruka kwa saa kadhaa kabla ya kuzama kwenye shabaha na kulipuka. Ukraine inasema Urusi iliwahi kuzitumia hapo awali.

    Iran inakanusha kuzisambaza kwa Urusi, na Urusi haijatoa maoni yoyote. Rais wa Urusi Vladimir Putin alisema mashamulizi ya wiki iliyopita ilikuwa ya kulipiza kisasi kwa kulipuliwa kwa daraja muhimu linalounganisha Urusi na Crimea inayokaliwa kwa mabavu, ambayo aliilaumu Ukraine.

    Ilikuwa ni mara ya kwanza wakati wa vita kituo cha Kyiv kililengwa moja kwa moja. Mapema wiki hii, Bw Putin alisema hakuna haja ya mashambulizi mikubwa zaidi dhidi ya Ukraine. Malengo mengi yaliyowekwa yamefikiwa, alisema, akiongeza kuwa haikuwa lengo lake kuharibu nchi.

    Soma zaidi:

  18. Mafuriko Nigeria: Maafa yasababisha vifo vya zaidi ya watu 600

    w

    Mafuriko ya hivi majuzi nchini Nigeria yamekuwa "janga" kubwa, na majimbo mengi hayakuwa tayari kuyakabili licha ya onyo, waziri wa usimamizi wa majanga amesema.

    Zaidi ya watu 600 wamefariki katika mafuriko mabaya zaidi kuwahi kutokea katika taifa hilo la Afrika Magharibi katika muongo mmoja uliopita.

    Watu wapatao milioni 1.3 wamekimbia makazi yao, na zaidi ya nyumba 200,000 zimeharibiwa. Mafuriko yanatarajiwa kuendelea hadi mwisho wa Novemba. Nigeria imezoea mafuriko ya msimu, lakini mwaka huu imekuwa mbaya zaidi kuliko kawaida.

    Serikali imesema mvua kubwa isiyo ya kawaida na mabadiliko ya hali ya hewa ndio ya kulaumiwa. Wataalamu pia wanasema mipango duni na miundombinu imezidisha uharibifu huo.

    Mitumbwi na majirani wanaojali walikabiliana na mafuriko ya Nigeria Tangu mafuriko yaanze mwanzoni mwa msimu wa joto, maeneo makubwa ya mashamba yameharibiwa. Kuna wasiwasi kuhusu kuongezeka kwa magonjwa, na usambazaji wa chakula na mafuta pia umetatizwa. Katika mkutano na waandishi wa habari siku ya Jumapili, waziri wa masuala ya kibinadamu na usimamizi wa majanga wa Nigeria, Sadiya Umar Farouk, alitoa wito kwa mamlaka za mitaa kuwahamisha watu wanaoishi katika maeneo hatarishi zaidi.

    Mamlaka tayari zinatoa chakula na msaada mwingine kwa wale walioathirika, alisema. Aliongeza kuwa licha ya ''juhudi za pamoja'' na maonyo ya mapema, serikali nyingi za majimbo "hazikujiandaa" kwa mafuriko. Maafa hayo yameathiri majimbo 27 kati ya 36 ya Nigeria.

    Sehemu ya tatizo ni kwamba watu hurudi makwao kwenye nyanda za mafuriko kila mwaka baada ya maji kupungua. Wengi hawana njia za kuhama. Uchumi wa Nigeria umedorora katika mwaka uliopita, huku mfumuko wa bei ukiwa juu sana na jamii nyingi zikijitahidi kustahimili.

    Shirika la Mpango wa Chakula Duniani na Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo lilisema mwezi uliopita kuwa Nigeria ni miongoni mwa nchi sita zinazokabiliwa na hatari kubwa ya janga la njaa. Shirika la hali ya hewa la Nigeria limeonya kuwa mafuriko yanaweza kuendelea hadi mwisho wa Novemba katika baadhi ya majimbo ya kusini mwa nchi hiyo, yakiwemo Anambra, Delta, Rivers, Cross River na Bayelsa.

  19. NATO na Urusi zote kufanya mazoezi ya vikosi vyao vya nyuklia.

    w

    Pentagon na jumuiya ya kijasusi ya Marekani wanafuatilia harakati zozote za silaha za nyuklia nchini Urusi wakati wa mazoezi ambayo maafisa wa Marekani wanasema yanapaswa kufanyika kabla ya mwisho wa mwezi.

    Afisa mkuu wa Pentagon aliiambia CNN kwamba matamshi ya nyuklia ya Urusi na uamuzi wa kufanya mazoezi katikati ya vita na Ukraine ni kutowajibika.

    Kwa mujibu wa Marekani, mazoezi hayo ya Kirusi hufanyika kila mwaka na, kwa mujibu wa John Kirby, mratibu wa mawasiliano wa kimkakati wa Baraza la Usalama la Taifa la Marekani, yatajumuisha kurusha makombora ya moja kwa moja na kupelekwa kwa vifaa vya kimkakati.

    Kwa upande wake, NATO itaanza Jumatatu mazoezi yake ya kila mwaka ya nyuklia, ambayo yatahudhuriwa na nchi 14, pamoja na Marekani.

    Zitahusisha ndege zenye uwezo wa kubeba vichwa vya nyuklia, ingawa hakutakuwa na silaha za kijeshi ndani ya ndege hiyo. Kwa jumla, hadi ndege 60 zitashiriki katika mazoezi hayo, ikijumuisha wapiganaji wa kisasa, ndege za upelelezi na ndege za mafuta.

    Safari za ndege zitafanyika Ubelgiji, Uingereza na Bahari ya Kaskazini.

    Lengo la zoezi hilo ni kuhakikisha kuwa kizuwizi cha nyuklia cha NATO kinasalia "kinachoaminika, kinafaa, salama na cha kutegemewa," msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Marekani alisema.