Ukraine yapiga hatua moja zaidi karibu na kujiunga na muungano wa bara Ulaya

Rais wa Tume ya Ulaya Ursula von der Leyen amekuwa akitoa taarifa kuhusu maombi ya uanachama wa Umoja wa Ulaya na Ukraine, pamoja na Moldova na Georgia.

Moja kwa moja

  1. Na mpaka hapo ndio tunafikia mwisho wa matangazo yetu ya moja kwa moja kwa leo, tukutane tena hapo kesho majaaliwa

  2. Mahakama yawaruhusu wanafunzi wa kike wavae hijab shuleni Nigeria

    Hijab

    Mahakama ya juu zaidi nchini Nigeria imeamua kuwa wanafunzi wa kike wanafunzi wavae vilemba vinavyofunika vichwa vyao -vinavyofahamika kama Hijab bila kusumbuliwa au kubaguliwa.

    Katika uamuzi mkubwa uliotolewa Ijumaa, mahakama ya juu zaidi nchini Nigeria imepitisha uamuzi wa Mahakama ya rufaa kwamba hijab ni ubaguzi dhidi ya wanafunzi Waislamu katika jimbo hilo.

    Serikali ya jimbo la Lagos ilikuwa imepiga marufuku matumizi ya hijab , ikidai kuwa sio sehemu ya sare za shule zilizoidhinishwa za wanafunzi. Marufuku hiyo ilipingwa na wanafunzi Waislamu mwaka 2015, waliosema kuwa marufuku hiyo inakiuka haki zao za mawazo, za kidini na za elimu . Makabiliano ya kisheria kuhusiana na marufuku hiyo yamedumu kwa mud awa miaka saba.

    Uamuzi wa Mahakama hiyo ya juu zaidi nchini Nigeria hatimaye unaweza kumaliza utata unaozingira uvaaji wa hijab wa wanafunzi katika shule zisizo za kiduni nchini Nigeria.

    Wanafunzi wa shule kadhaa za kusini mwa Nigeria wamekuwa katika mzozo uliofuatia upinzani wa uvaaji wa hijab katika baadhi shule unaoshuhudiwa katika shule za umma.

    Unaweza pia kusoma:

    • Mwanafunzi aliyevaa hijab azuiwa kufuzu chuoni Nigeria
    • Wasichana waliojifanya Waislamu wakamatwa Nigeria
    • Msichana aliyevaa hijab ashambuliwa na mtu aliyetaka kukata vazi hilo Canada
  3. Urusi na Ukraine: Urusi 'ililazimishwa' kuanzisha 'operesheni maalumu’ katika Ukraine - Putin

    Putin

    Katika hotuba anayoendelea kuitoa katika mkutano wa kimataifa wa Uchumi mjini St Petersburg, Rais wa Urusi anasema uamuzi wa Urusi wa kuanzisha kile alichokiia ‘operesheni maalumu’ ulikuwa mgumu- lakini ‘tulilazimishwa’ .

    Putin anasema ililenga kuwalinda "watu wetu" watu wa Donbas – mashariki mwa Ukaraine, huku akiendelea kurejelea madai kwambawalikuwa "wanakabiliwa na mauaji ya kimbari".

    Ameongeza kuwa ‘’nchi za Magharibi zinaendelea kuisukumia Ukraine silaha’’ akisema kuwa ‘’malengo yote ya operesheni maalumu yatafikiwa bila wasi wasi".

    Vita vya Ukraine: Mengi zaidi

    • MOJA KWA MOJA:Biden amuonya Putin: ''Madikteta watagharamika
    • YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
    • UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
    • UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
    • KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
    • ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
    • PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
  4. Habari za hivi punde, Urusi na Ukraine: Putin anasema vikwazo vina madhara kwa wale walioviweka

    Putin

    Rais Vradmir Putin anasema vikwazo vina madhara zaidi kwa wale walioviweka.

    Akizungumza mjini St Petersburg, katika Mkutano wa kimataifa wa wa Uchumi , Bw Putin amesema Muungano wa Ulaya unaweza kupoteza dola bilioni 400 (£326bn) kwasababu ya vikwazo dhidi ya Urusi.

    Putin ameongeza kuwa EU imepoteza "hadhi yake ya kisiasa" katika kuvijibu vita vya Ukraine.

    Anasema hasara ya kiuchumi inaongezeka katika nchi za Ulaya na kuongeza kuwa ukosefu wa usawa utaongezeka tu kutokana na vikwazo.

    Putin anasema maslahi halisi ya watu katika Ulaya yanawekwa kando.

    Vita vya Ukraine: Mengi zaidi

    • MOJA KWA MOJA:Biden amuonya Putin: ''Madikteta watagharamika
    • YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
    • UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
    • UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
    • KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
    • ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
    • PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
  5. Rwanda: Askari wa DRC auawa baada ya kuwashambulia maafisa wa usalama wa Rwanda

    FLICKR.COM/PAULKAGAME

    Wizara ya ulinzi ya Rwanda imesema kuwa mwanajeshi wa DRC amepigwa risasi na kufa baada ya kuwashambulia maafisa wa usalama wa Rwanda na wananchi waliokuwa wakivuka mpaka.

    Mwanajeshi huyo wa DRC alipigwa risasi na kufariki kilomita 25 ndani ya eneo la Rwanda. Imesema Wizara ya ulinzi ya Rwanda.

    Taarifa ya Wizara ya Ulinzi ya Rwanda imesema wanajeshi wawili wa DRC waliokuwa na silaha aina ya AK 47 wamevuka eneo la kizuwizi kidogo ‘’Petite Barriere’’ lililopo kwenye mpaka wa Rubavu baina ya nchi hizo mbili na kuwapiga risasimaafisa wa usalama wa Rwandana raia waliokuwa wakivuka mpaka.

    Taarifa hiyo iliyotumwa kwenye mtandao wa Twitter imesema tukio hilo lilitokea majira ya saa mbili na dakika 45 kwa saa za eneo.

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

    Rwanda inasema imeanzisha uchunguzi kuhusiana na tukio hilo na imekwishaifahamisha DRC.

    Kulingana na Wizara ya ulinzi ya Rwanda afisa wa polisi wa Rwanda aliyekuwa kwenye ulinzi alifyatua risasi kujilinda, na kuwalinda raia waliokuwa wakivuka mpaka.

    Akizungumza na Televisheni ta taifa mjini Kigali, kuhusiana na tukio hili Meya wa mji wa Rubavu Ildephonse Kambogo amesema:

    ‘’Kilichopo sasa tuko hapa mpakani tunasubiri timu ya uchunguzi ya jeshi la kikanda (EJVM) ili kuanzisha upelelezina kutoa taarifa yake.shughuli zote za mpakani zinasimamishwa kwa muda-raia wanaofanya biashara kutoka Goma ama kutoka upande wetu wamekuwa na wasi wasi safari zimesitishwa ili kuruhusu uchunguzi… hali ya usalamahapa mpakani ipo na kiongozi wa mji wa Goma yuko hapa tuko pamoja ametuma ujumbe akiomba msamaha na kubainisha kwambahuenda askari huyo alikuwa na matatizo binafsi ‘’

    Ameongeza kwamba Rwanda imewataka raia wake kuwa makini sana wanapofanya safari mjini Goma:‘’Tunawataka raia wetu kutoa kipaumbele kwa swala la usalama wao …tumekuwa na mikutano ya kuwahamasisha kuepuka safari zisizo la lazima katika nchi ya DRC ‘’

    Haya yanajiri huku hali ya wasi wasi ikiendelea kutanda katika eneo la Mashariki mwa DRC, kutokana na ghasia za mapigano ya makundi hasimu katika eneo hilo.

    Jumanne mamia ya Wacongo walifanya maandamano hadi kwenye mpaka wa Rwanda kuilaumu Rwanda kwa kile walichosema inayumbisha usalama wa nchi yao.

    Rais wa DRC Felix Tchisekedi hivi karibuni aliilaumu Rwanda kwa kuwaunga mkono wapiganaji wa M23 katika makabiliano yao na serikali, shutuma ambazo Rwanda imezipinga.

    Rwanda inaishutumu DRC kwa kushindwa kudhibiti kundi la waasi wa FDLR , (wanamgambo wanaoshukiwa kutekeleza mauaji ya kimbari ya Rwanda) linaloendesha uasi Mashariki mwa Congo na ambalo Rwanda inasema linahatarisha usalama wake.

    Unaweza pia kusoma:

    • Mzozo wa Rwanda na DRC: Waasi wa M23 waondoka maeneo walioteka huku Kagame na Tshisekedi wakizungumza
    • Mzozo wa DRC na Rwanda : M23, majirani na bahati mbaya ya DRC
    • Tshisekedi amesema 'hakuna tashwishi' kwamba Rwanda inasaidia M23
    • Mzozo wa DRC: Je inawezekana kuyamaliza makundi ya wapiganaji Mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo?
  6. Julian Assange anaweza kukabidhiwa kwa Marekani - Uingeza

    asange
    Maelezo ya picha, Idhini ya kumkabidhi kwa Marekani, muasisi wa mtandao wa Wikileaks Julian imetolewa na Waziri wa mambo ya ndani wa Uingereza Priti Patel.

    Bw Assange ana siku 14 za kukata rufaa juu ya uamuzi huu, Wizara ya mambo ya ndani imesema.

    Ilisema kuwa mahakama zimebaini kuwa kukabidhiwa kwa Bw Assange hakutakuwa; kinyume na haki za binadamu’’ na kwamba nchini Marekani’’atashugulikiwa ipasavyo’’.

    Bw Assange anasakwa na mamlaka za Marekani kuhusu nyaraka zlizovuja katia mwaka 2010 na 2011.

    Amekuwa gerezani tangu alipoondolewa kwenye ubalozi mjini London katika mwaka 2019 na kukamatwa na polisi wa Uingereza, baada ya Ecuador kumuondolea hadi ya uhamiaji.

    Muaustralia huyo anashikiliwa katika gereza la Belmarsh lililoko London baada ya makabiliano ya muda mrefu ya kisheria ya kutaka asikabidhiwe kwa Marekani.

    Ukijibu kuhusu agizo hilo la Waziri wa mambo ya ndani, Mtandao wa Wikileaks ulithibitisha kuwa utakata rufaa juu ya uamuzi huo.

    Mke wa Assange, Stella, amesema kuwa bwana yake ‘’hakufanya lolote baya’’ na hajatekeleza uhalifu wowote’’.

    "Ni mwandishi wa habari na mchapishaji, na anaadhibiwa kwa kufanya kazi yake."

    Mwezi mei 2019, wakati alipokuwa akitumikia kifungo cha jela nchini Uingereza kwa kukiuka dhamana, wizara ya sheria ya Marekani iliwasilisha mashitaka 17 dhidi ya Bw Assange kwa kukiuka sheria ya upelelezi - ikidai kuwa nyaraka hizo zilizochukuliwa na Wikileaks zinahatarisha maisha ya watu.

    Bw Assange anatafutwa na Marekani kuhusiana na uchapishwaji wa maelfu ya nyaraka za siri zinazohusiana na vita vya Afghanistan na Iraq. Binafsi anakana kufanya kosa lolote.

    Unaweza pia kusoma:

    • Jopo la UN 'lakubali ombi la Julian Assange’
    • WikiLeaks: Julian Assange kuhojiwa na maafisa wa Sweden
    • Virusi vya corona: Mwanamke aliyezaa watoto wawili na Assange kwa siri ubalozini aeleza hofu yake
    • Jopo la UN 'lakubali ombi la Julian Assange’
  7. Ukraine yapiga hatua moja zaidi karibu na kujiunga na muungano wa bara Ulaya

    th

    Tume ya Ulaya inapendekeza kwamba Ukraine iteuliwe kuwa mgombea wa uanachama wa Umoja wa Ulaya - na kuleta matumaini yake ya kujiunga na muungano huo hatua moja karibu..

    Rais wa Tume ya Ulaya Ursula von der Leyen amekuwa akitoa taarifa kuhusu maombi ya uanachama wa Umoja wa Ulaya na Ukraine, pamoja na Moldova na Georgia.

    Anasema:

    ‘Tuna ujumbe mmoja wazi - na hiyo ni, ndiyo, Ukraine inastahili mtazamo wa Ulaya, ndiyo, Ukraine inapaswa kukaribishwa kama nchi ya mgombea. Hii ni kwa kuelewa kwamba kazi nzuri imefanywa - lakini kazi muhimu inabaki kufanywa. Mchakato wote unategemea sifa, kwa hivyo huenda kwa kitabu na maendeleo inategemea kabisa Ukraine. Kwa hivyo ni Ukraine ambayo iko mikononi mwake."

    Tume ya Ulaya inakaribisha Ukraine na Moldova kama wagombeaji wa uanachama.

    Lakini Georgia, jamhuri nyingine ya zamani ya Soviet, inaombwa kutimiza masharti fulani kabla ya kupewa hadhi sawa.

    "[Moldova] iko kwenye njia ya kweli ya kuunga mkono mageuzi, kupambana na rushwa na njia ya Ulaya," Ursula von der Leyen anasema.

    "Georgia lazima sasa ije pamoja kisiasa ili kubuni njia wazi kuelekea mageuzi ya kimuundo na EU."

  8. Kombe la Dunia 2026: Uwanja wa Azteca na SoFi kati ya kumbi 16 zinatakazoandaa mechi

    th

    Uwanja wa Azteca wa Jiji la Mexico na Uwanja wa SoFi wa Rams ni miongoni mwa viwanja 16 vya kuandaa michuano ya Kombe la Dunia la 2026.

    Kombe la Dunia la kwanza la timu 48 litafanyika katika viwanja 16 katika miji 11 ya Amerika, pamoja na kumbi tatu huko Mexico na mbili nchini Canada.

    Hii ni mara ya kwanza kwa nchi tatu kuandaa michuano hiyo.

    Uwanja wa Azteca pia utakuwa uwanja wa kwanza kushiriki michuano mitatu tofauti ya Kombe la Dunia.

    Pasadena Rose Bowl ya Los Angeles, ambayo ilikuwa mwenyeji wa fainali ya Kombe la Dunia ya 1994, haijajumuishwa.

    Eneo jingine kubwa ambalo halipo ni mji mkuu wa Marekani, Washington DC, ambao ulikuwa mmoja wa miji tisa iliyoandaa mara ya mwisho Marekani ilipoandaa mashindano hayo.

    Zabuni ya pamoja kutoka Washington DC na Baltimore, Maryland, ilikuwa mojawapo ya sita ambazo hazikuchaguliwa pamoja na Cincinnati, Denver, Nashville, Orlando na Edmonton.

    "Umekuwa mchakato wa ushindani wa ajabu. Miji yote imekuwa ya kushangaza. Hili lilikuwa chaguo gumu sana," alisema afisa mkuu wa mashindano na matukio wa Fifa Colin Smith.

    "Huwezi kufikiria Kombe la Dunia likija Marekani. na mji mkuu bila kuchukua jukumu kubwa pia."

    Orodha kamili ya Viwanja

    Atlanta - Mercedes-Benz Stadium

    Boston - Gillette Stadium

    Dallas - AT&T Stadium

    Guadalajara - Estadio Akron

    Houston - NRG Stadium

    Kansas City - Arrowhead Stadium

    Los Angeles - SoFi Stadium

    Mexico City - Estadio Azteca

    Miami - Hard Rock Stadium

    Monterrey - Estadio BBVA

    New York/New Jersey - MetLife Stadium

    Philadelphia - Lincoln Financial Field

    San Francisco Bay Area - Levi's Stadium

    Seattle - Lumen Field

    Toronto - BMO Field

    Vancouver - BC Place

  9. Rwanda yasema ukosoaji wa mpango wa Uingereza wa kupata hifadhi 'ni matusi'

    Ukosoaji wa kimataifa juu ya mpango wa Rwanda wa kupokea waomba hifadhi kutoka Uingereza ni "matusi", kulingana na msemaji wa serikali Yolande Makolo.

    Alisema wakosoaji wanapaswa kusafiri hadi katika nchi hiyo ya Afrika mashariki kuona maendeleo ambayo imepiga.

    "Madai kwamba kuishi Afrika ni adhabu ni matusi kwa wanaoishi hapa na wanafanya kazi kwa bidii kujenga nchi zetu. Tunataka Afrika ifanikiwe.

    Rwanda imepiga hatua kubwa sana. Watu waje waone," Bi Makolo alitweet.Aliambatanisha kipande cha video cha mcheshi wa Afrika Kusini Trevor Noah akikosoa mwitikio wa mpango wa hifadhi

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

  10. Mbappe ‘alibadilisha ndoto yake’ – Rais wa Real Madrid

    Kylian Mbappe
    Maelezo ya picha, Kylian Mbappe

    Rais wa Real Madrid Florentino Perez anasema Kylian Mbappe "alibadilisha ndoto yake " baada ya mshambuliaji huyo wa Ufaransa kukataa kuhamia klabu hiyo ya Uhispania.

    Mbappe, 23, alitia saini mkataba mpya wa miaka mitatu na Paris St-Germain badala ya kuhamia klabu hiyo ya La Liga."Ndoto yake ilikuwa kucheza Real Madrid," Perez aliambia El Chiringuito.

    "Tulitaka kufanya hivyo Agosti iliyopita na hawakumruhusu kuondoka, aliendelea kusema anataka kucheza Madrid na siku 15 kabla alibadilisha hali hiyo.

    "Kulingana na mtaalam wa soka wa Uhispania Guillem Balague, Mbappe alikubali kifurushi cha fedha na Real miezi kadhaa iliyopita kwa ajili ya kuhamia Uhispania kabla ya kuamua kusalia PSG.

  11. 'Wazungu wanaopenda vyura, maini na pasta wanapenda kuja Kiev' - Medvedev

    .
    Maelezo ya picha, Viongozi wa Ulaya Kyiv

    Rais wa zamani wa Urusi, Waziri Mkuu na sasa Naibu Mwenyekiti wa Baraza la Usalama la Urusi Dmitry Medvedev alikosoa ziara hiyo kwenye Twitter.

    Alitoa maoni kwa kutumia dhana mbaya kuhusu vyakula vya Ulaya.

    "Wazungu wanaopenda vyura, maini na pasta wanapenda kuja Kiev," alisema. Faida ni sifuri. Tena, uanachama wa Umoja wa Ulaya na mipira ya zamani iliahidiwa, walikunywa vodka na kurudi kwenye gari moshi kama miaka mia moja iliyopita. Yote ni sawa. Lakini hii haileti amani karibu na Ukraine. Na muda unakwenda,” alisema.

    Mkutano na waandishi wa habari ulifanyika kama sehemu ya ziara hiyo ya viongozi wa Ulaya huko Kiev.

    Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alisema viongozi wanaozuru Kiev wataunga mkono ombi la Ukraine la mgombea wa uanachama wa EU.

    Macron aliahidi Ufaransa itaipatia Ukraine silaha 6 za ziada za masafa marefu za Kaisari.

  12. NATO itaendelea kusambaza silaha nzito kwa Ukraine

    Kabla ya mkutano wa kilele wa muungano huo mjini Brussels, Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg alisema Ukraine inahitaji "uungwaji mkono wa haraka" kwa sababu iko katika hali ngumu.

    Stoltenberg amesema nchi wanachama wa NATO zitaendelea kuipatia Ukraine silaha nzito na mifumo ya makombora ya masafa marefu.

    Anasubiri kifurushi kipya cha msaada kukuafikiwa na Kiev wakati wa mkutano huo."Tunalenga katika kuimarisha misaada," alisema.

    Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg
    Maelezo ya picha, Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg
  13. Gazprom: Tutauza bidhaa zetu kwa masharti yetu - Mkuu wa kampuni ya gesi Urusi

    Alexei Miller
    Maelezo ya picha, Mkuu wa kampuni ya gazprom nchini Urusi Alexei Miller

    Gazprom: Tutauza bidhaa zetu kwa masharti yetu - Mkuu wa kampuni ya gesi Urusi

    Mkuu wa kampuni kubwa ya gesi inayodhibitiwa na serikali ya Urusi ya Gazprom amesema ni kesi ya "bidhaa zetu, sheria zetu" baada ya kampuni hiyo kupunguza nusu ya usambazaji wake wa bidhaa hiyo kwa Ujerumani.

    Waziri wa Uchumi wa Ujerumani ameishutumu Gazprom kwa kujaribu kupandisha bei ya nishati kwa kupunguza usambazaji.

    Lakini Gazprom ilisema hatua hiyo inatokana na kuchelewa kurejesha vifaa vinavyohudumiwa na kampuni ya Ujerumani ya Siemens Energy nchini Canada.

    Italia na Austria pia zimeripoti maporomoko makubwa ya usambazaji wa gesi ya Urusi. Kremlin ilisema hali hiyo haikutarajiwa.

    Mtendaji mkuu wa Gazprom Alexei Miller alisema Urusi itafuata sheria zake baada ya kuweka kiwango cha gesi kwa Ujerumani hadi chini ya mita za ujazo 70m kwa siku - chini ya nusu ya kiwango cha sasa."Bidhaa zetu, sheria zetu.

    Hatuchezi na sheria ambazo hatukuunda," Bw Miller alisema wakati wa mjadala katika Kongamano la Kiuchumi la Kimataifa la St Petersburg.

  14. Rais Samia amuhamisha Mtendaji Mkuu wa Wizara inayosimamia Loliondo na Ngorongoro

    Uhurumedia

    Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amemuhamisha Katibu mkuu wa Wizara ya Utalii na Maliasili, Dkt. Francis Michael kwenda wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia kuchukua nafasi ya Eliamani Sedoyeka aliyehamishiwa wizara ya Utalii na Maliasili.

    Ingawa, taarifa ya Ikulu, kuhusu mabadiliko hayo haijasema sababu za mabadiliko ni nini, baadhi ya maoni ya watu yanahusisha na kile kinachoendelea huko Loliondo na Ngorongoro.

    Michael alikuwa mtendaji mkuu wa wizara ya maliasili na Utalii, inayosimamia masuala ya hifadhi za nchi hiyo ikiwemo ya Ngorongoro na Pori Tengefu Loliondo, kaskazini mwa Tanzania, zilizoibua wasiwasi wa kiusalama hivi karibuni.

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

    Mzozo kati ya wakazi wa Loliondo na mamlaka za Serikali umedumu kwa miaka karibu 30, na hivi karibuni ulisababisha kifo cha Polisi mmoja, kufuatia zoezi la kuweka mipaka karibu na mpaka wa pori Tengefu Loliondo kutenganisha hifadhi na maeneo ya makazi.

    Kwa mujibu wa Serikali zoezi hilo linaloendeshwa kwa kufuata sheria, linalenga kunusuru uhifadhi ndani ya hifadhi, ndani ya Pori Tengefu Loliondo, na ndani ya mfumo ikolojia wa Serengeti na pia kunusuru utalii katika mfumo ikolojia huo.

    Kundi la kwanza la familia 27 za jamii ya kimasai waliokuwa wanaishi ndani yahifadhi ya Ngorongoro limewasili jana mkoani Tanga kuanza maisha mapya ili kunusuru hifadhi hiyo dhidi ya kuongezeka kwa shughuli za binadamu.

    Serikali ya Tanzania inasema inaendelea kuhamasisha mamia ya familia zingine kuondoka kwa hiyari katika eneo hilo la Ngorongoro, zoezi lililowahi kukutana na ukinzani mara kadhaa.

  15. Wapiganaji watatu wa Marekani waripotiwa kutoweka Ukraine

    Wapiganaji watatu wa Marekani
    Maelezo ya picha, Wapiganaji watatu wa Marekani

    Wapiganaji watatu wa Marekani waripotiwa kutoweka UkraineWizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imesema inafahamu kuhusu ripoti kwamba wapiganaji watatu wa Kimarekani wametoweka nchini Ukraine, huku wawili kati yao wakihofiwa kukamatwa.

    Maveterani wawili wa kijeshi waliokuwa wakipigania Ukraine walitajwa katika ripoti za wiki hii kuwa walichukuliwa mateka.Idara ya serikali ilisema Alhamisi: "Kuna ripoti za Mmarekani mmoja wa ziada ambaye hajulikani aliko.

    "Wiki iliyopita, wafungwa watatu wa kigeni walihukumiwa kifo kwa kuisaidia Ukraine.Wanaume hao wawili wa Uingereza na mwanamume mmoja wa

    Morocco walihukumiwa na mahakama ya kujitenga inayoungwa mkono na Urusi huko Donetsk kunyongwa kwa kupigwa risasi na askari.

    Ikulu ya White House ilisema Alhamisi "inafanya bidii sana kujifunza zaidi" kuhusu ripoti ambazo hazijathibitishwa za Wamarekani waliopotea au waliotekwa nchini Ukraine.

    Kundi la wanajeshi wa zamani wa Marekani na Ufaransa walituma ujumbe katika tweeter Jumatano kwamba Wamarekani wawili waliokuwa nao walikamatwa wiki moja iliyopita.

    Iwapo ripoti hiyo itathibitishwa, hawa watakuwa Wamarekani wa kwanza kupigania Ukraine kutekwa tangu vita kuanza mwezi Februari.

  16. Natumai hujambo