Putin aionya Finland kujiunga na Nato itakuwa 'kosa'
Rais wa Urusi Vladimir Putin amemuonya mwenzake wa Finland kwamba kujiunga na NATO na kuacha msimamo wa kutoegemea upande wowote wa Finland itakuwa "kosa".
Moja kwa moja
Finland yathibitisha ombi la kujiunga na Nato licha ya onyo la Putin
Chanzo cha picha, Reuters
Finland imethibitisha kwamba itaomba uanachama wa Nato, licha ya onyo kutoka kwa Rais wa Urusi Vladimir Putin kwamba kuacha kutoegemea upande wowote itakuwa "kosa".
Rais Sauli Niinisto aliiita "siku ya kihistoria". Anasema kubadilika kwa sera ni kukabiliana na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.
Mawaziri wa mambo ya nje wa Nato wanasema wanataka mchakato wa kujiunga na Finland haraka. Uswidi pia inaweza kutangaza nia yake ya kujiunga mara tu ifikapo Jumatatu.
Ufini inashiriki mpaka wa kilomita 1,300 (maili 810) na Urusi. Hadi sasa, imesalia nje ya Nato ili kuzuia kuchukiza jirani yake wa mashariki.
Makombora ya Urusi 'yaharibu' kituo cha jeshi la Ukraine magharibi
Chanzo cha picha, Reuters
Kituo cha kijeshi katika eneo la Lviv nchini Ukraine "kimeharibiwa " na shambulio la kombora la Urusi, gavana wa eneo hilo Maksym Kozytskyy anasema kwenye Telegram.
Katika wiki za hivi karibuni Urusi imekuwa ikilenga mashambulizi yake mashariki mwa Ukraine lakini mashambulizi ya hapa na pale yameendelea katika maeneo ya magharibi kama vile Lviv.
"Makombora manne ya adui yalipiga kituo cha miundombinu ya kijeshi katika Mkoa wa Lviv.
Kituo hicho kimeharibiwa kikamilifu. Kulingana na taarifa za awali, hakukuwa na majeruhi," Kozytskyy anasema.
Ameongeza kuwa mifumo ya ulinzi wa anga ya Ukraine imedungua makombora mawili.
Mapema siku hiyo Kozytskyy alisema makombora hayo yalipiga kituo hicho saa 04:30 kwa saa za huko (01:30 GMT).
Putin aionya Finland kujiunga na Nato itakuwa 'kosa'
Chanzo cha picha, Getty Images
Rais wa Urusi Vladimir Putin amemuonya mwenzake wa Finland kwamba kujiunga na NATO na kuacha msimamo wa kutoegemea upande wowote wa Finland itakuwa "kosa".
Alimwambia Sauli Niinistö hakuna tishio kwa usalama wa Finland.
Mazungumzo hayo yalikuja wakati wa simu iliyopigwa na rais wa Ufini, kabla ya ombi rasmi ambalo Ufini inatarajiwa kutangaza hivi karibuni.
Uswidi pia imeonesha nia yake ya kujiunga na muungano wa Magharibi, kufuatia uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine.
Ufini inashiriki mpaka wa kilomita 1,300 (maili 810) na Urusi.
Hadi sasa, imesalia nje ya Nato ili kuzuia kumchukiza jirani yake wa mashariki.
Bw Putin hakutoa tishio mahususi la kulipiza kisasi hatua hiyo ya Finland, lakini wizara ya mambo ya nje ya Urusi imedokeza kuwa kutakuwa na kulipiza kisasi.
Watu kumi wauawa katika shambulizi linaloshukiwa kuchochewa na ubaguzi wa rangi Marekani
Chanzo cha picha, CBS
Mwanaume mmoja mwenye asili ya weupe amewapiga risasi watu 10 katika kitongoji cha watu weusi katika jimbo la New York katika kile mamlaka inaita shambulizi lililochochewa na ubaguzi wa rangi.
Mwanaume huyo, mwenye miaka 18 aliyetajwa kwa jina la Payton Gendron katika nyaraka za mahakama, alikamatwa baada ya mvutano katika eneo la tukio - duka kubwa katika jiji la Buffalo.
Mshukiwa aliingia katika duka hilo Jumamosi mchana kabla ya kufyatua risasi. Akilirusha shambulio hilo mtandaoni.
Rais wa Marekani Joe Biden alilaani kile alichokiita kitendo cha "chukizo".
"Tunachunguza tukio hili kama uhalifu wa chuki na kesi ya itikadi kali za kikabila," alisema Stephen Belongia, kutoka ofisi ya FBI ya Buffalo, akiongeza kuwa kuna ushahidi wa "uadui wa rangi."
Habari za CBS ziliripoti kwamba mshambuliaji alipiga kelele za kibaguzi wakati wa ufyatuaji risasi na kusema kuwa alikuwa na maneno ya kikabila yaliyoandikwa kwenye silaha yake.
Pia inaonekana alichapisha manifesto mtandaoni iliyojumuisha lugha na mawazo ya ubaguzi wa rangi.
Mshukiwa anaaminika kuwa aliendesha gari kwa takriban maili 200 kufika eneo lenye watu weusi wengi jijini humo.
Watu 13 walipigwa risasi kwa jumla na wengi wa waathiriwa walikuwa weusi, Kamishna wa Polisi wa Buffalo Joseph Gramaglia alisema.
"Alitoka kwenye gari lake.
Alikuwa na silaha nyingi sana. Alikuwa na vifaa vya mbinu. Alikuwa amevaa kofia ya chuma. Alikuwa na kamera ambayo alikuwa akirusha moja kwa moja alichokuwa akifanya," Bw Gramaglia aliwaambia wanahabari.
Alisema mtuhumiwa alisalimisha silaha yake baada ya hali ya wasiwasi na kupelekwa mahabusu. Baadaye alifikishwa mahakamani akishtakiwa kwa mauaji ya kiwango cha kwanza.
Waathiriwa watatu waliojeruhiwa - ambao wote walifanya kazi katika duka kubwa - hawajapata majeraha ya kutishia maisha.
Afisa wa polisi aliyestaafu ambaye alikuwa akifanya kazi kama mlinzi alijaribu kumpiga risasi mshukiwa lakini alikuwa miongoni mwa waliouawa, polisi walisema.
Habari za asubuhi na karibu katika taarifa zetu za moja kwa moja