EU yaondoa vikwazo dhidi ya Grace Mugabe

Chanzo cha picha, Getty Images
Serikali ya Zimbabwe imekaribisha uamuzi ya Muungano wa Ulaya (EU) wa kuondoa vikwazo vya usafiri na uchumi dhidi ya Makamu wa Rais Constantino Chiwenga, mama taifa wa zamani Grace Mugabe na mkuu wa majeshi Valerio Sibanda.
EU ilichukua uamuzi huo licha ya kukiri kwamba rekodi ya haki za binadamu ya Zimbabwe haijaboreka na inaweza kuwa mbaya zaidi.
Vikwazo hivyo viliwekwa kwa mara ya kwanza miaka minne 20 iliyopita, lakini vilisitishwa miaka miwili iliyopita. Sasa vimeondolewa kabisa.
Vikwazo dhidi ya sekta ya ulinzi ya Zimbabwe bado vipo.
Msemaji wa serikali ya Zimbabwe Nick Mangwana aliiambia BBC kwamba uamuzi huo ni ishara chanya na unaonyesha mafanikio ya kujiunga tena na EU.
Serikali itaendelea kushinikiza vikwazo vyote kuondolewa bila masharti, aliongeza.
Rais Emmerson Mnangagwa amekuwa akijaribu kuboresha uhusiano na mataifa ya Magharibi tangu kumwondoa madarakani mtawala wa muda mrefu Robert Mugabe mwaka 2017.
Serikali iliyoongozwa na Mugabe ilikuwa na mzozo mkubwa na EU baada ya kunyakua mashamba yanayomilikiwa na wazungu, na kuanza kukandamiza upinzani.










