ECOWAS yapanga tena kukutana na viongozi wa mapinduzi Niger

Chanzo cha picha, EPA
Jumuiya ya ECOWAS ya Afrika Magharibi inalenga kutuma kamati ya bunge nchini Niger kukutana na viongozi wa mapinduzi walionyakua mamlaka mwezi uliopita, msemaji alisema Jumamosi, sehemu ya jitihada za mwisho za kikanda za kurejesha utawala wa kiraia unaojumuisha viongozi wa kidini.
Wanajeshi wa Niger mwezi uliopita walimshikilia Rais Mohamed Bazoum na kuvunja serikali iliyochaguliwa, na kulaaniwa na mataifa yenye nguvu ya kikanda ambayo yameanzisha kikosi cha kijeshi ambacho kinasema kitatumwa kama suluhu la mwisho iwapo mazungumzo yatashindwa.
Lakini viongozi wa mapinduzi, wakiongozwa na Jenerali Abdourahamane Tchiani, wamepinga juhudi za kidiplomasia za Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS), Marekani na mataifa mengine, na hivyo kuibua hali ya mzozo zaidi katika eneo maskini la Sahel la Afrika Magharibi, linakabiliwa na uasi mbaya wa Kiislamu.





