Mamluki wa Wagner wawasili nchini Belarus-Ukraine

Walinzi wa mpakani mwa Ukraine wamethibitiha kwamba mamluki wa kundi la Wagner wamewasili nchini Belarus kutoka taifa Jirani la Urusi.

Moja kwa moja

  1. Mamluki wa Wagner wawasili nchini Belarus-Ukraine

    Picha zimeibuka zinazodaiwa kuwaonesha wapiganaji wa Wagner wakiwafunza wanajeshi wa Belarusi katika kambi ya kusini-mashariki mwa Minsk.

    Walinzi wa mpakani mwa Ukraine wamethibitiha kwamba mamluki wa kundi la Wagner wamewasili nchini Belarus kutoka taifa Jirani la Urusi.

    Walinzi hao wa DPSU wanasema kwamba wanachunguza kuna wapiganaji wangapi nchini Belarus ambayo pia inapakana na Ukraine pamoja na maeneo walipo na malengo yao .

    Ripoti moja iliyothibitishwa inasema kwamba msafara wa magari 60 ya kundi la Wagner yalipita mpakani na kuingia Belarus mapema siku ya Jumamosi.

    Mnamo mwezi Juni, Wagner walifanya uasi dhidi ya seriiali ya rais Putin. Hatahivyo makubaliano yalisitisha uasi huo uliofanyika katika kipindi cha saa 24, ambapo vikosi hivyo viliuteka mji mmoja na kuanza kuelekea mjini Moscow kabla ya kusitisha hatua hiyo yapata kilomita 200 kutoka mji mkuu huo.

    Chini ya makubaliano hayo wapiganaji wa Wagner waliagizwa kujiunga na jeshi la Urusi ama kwenda Belarus, mshirika wa karibu wa Urusi, Mkuu wa Wagner Yevgheny Prighozin pia alitakiwa kwenda Belarus , hatahivyo hajulikani alipo.

    Soma zaidi;

  2. Declan Rice: Arsenal yakamilisha uhamisho kutoka West Ham kwa dau la £105m

    Rice (katikati) amekuwa uhamisho wa rekodi ya Arsenal baada ya kuhama kutoka West Ham

    Arsenal imethibitisha usajili wa kiungo wa kati wa England Declan Rice kutoka West Ham kwa dau la £100m Pamoja na nyongeza ya £5m.

    Tangazo hilo la the Gunners linajiri baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 kuandikia barua mashabiki wa West Ham akisema jinsi ilivyokuwa vigumu kwake kufanya uamuzi huo mgumu wa kuondoka katika klabu hiyo.

    Rice ametia Saini kandarasi ya miaka mitano na Arsenal mkataba ambao una fursa ya mwaka mmoja Zaidi.

    Nimekuwa nikiitazama Arsenal katika misimu michache iliopita na na mwelekeo wao, alisema. Sio msimu uliopita lakini msimu kabla ya msimu uliopita , walimaza katika nafasi ya tano , lakini ungeweza kuona mbinu ya mchezo ambayo Mikel Arteta alikuwa akiidhinisha.

    “Msimu uliopita ulikuwa mzuri sana , wakifanikiwa kuzishinda timu zote isipokuwa Manchester City pekee” alisema

  3. Masharti ya Syria kuhusu utoaji misaada hayakubaliki, yasema UN

    Mamilioni ya watu katika eneo linaloshikiliwa na waasi kaskazini-magharibi mwa Syria wanategemea misaada ya Umoja wa Mataifa kuishi

    Umoja wa Mataifa umeelezea kuwa "haikubaliki" masharti yaliyowekwa na Syria katika kuruhusu msaada kuendelea kufikia maeneo yanayodhibitiwa na waasi.

    Balozi wa Syria katika Umoja wa Mataifa alisema siku ya Alhamisi serikali yake itaruhusu msaada kuendelea kuingia nchini kupitia kivuko cha Bab al-Hawa kutoka Uturuki.

    Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hapo awali walishindwa kufikia makubaliano ya kuweka wazi kivuko hicho.

    Takribani watu milioni 4.1 kaskazini-magharibi mwa Syria wanategemea misaada.

    Katika barua kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, balozi wa Syria Bassam Sabbagh alisema Damascus imefanya "uamuzi huru" kuruhusu msaada kupitia Bab al-Hawa kwa muda wa miezi sita ijayo.

    Ingeruhusu uwasilishaji kuanza tena "kwa ushirikiano kamili na uratibu na serikali ya Syria", alisema. Lakini katika waraka uliotumwa kwa Baraza la Usalama na kuonekana na mashirika ya habari ya AFP na Reuters, Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya

    Kibinadamu (OCHA) ilisema pendekezo hilo "lina masharti mawili yasiyokubalika".Ilisema kwamba, kwanza, serikali ya Syria "imesisitiza kwamba Umoja wa Mataifa haupaswi kuwasiliana na vyombo vilivyotajwa kama 'magaidi'.

    Tangu kuanza kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria mwaka 2011, Rais Bashar al-Assad mara kwa mara amekuwa akiyataja makundi yoyote ya waasi au wapinzani wa utawala wake kuwa ni magaidi.

    OCHA pia ilisema Damascus pia ilitaka usambazaji wa misaada yote kaskazini-magharibi mwa Syria usimamiwe na kuwezeshwa na Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC) na Shirika la Hilali Nyekundu la Syria (SARC).

    Ilisema hali hiyo "haiambatani na uhuru wa Umoja wa Mataifa na wala haiendani na vitendo, kwani ICRC na SARC hazipo" katika eneo hilo.

    Hata hivyo, ilisema pendekezo la serikali ya Syria linaweza kuwa "msingi kwa Umoja wa Mataifa kufanya shughuli za kibinadamu za kuvuka mpaka kupitia kivuko cha mpaka cha Bab al-Hawa".

  4. Maafisa Uganda watakiwa kuelezea walivyotumia $2.6m kufundisha unywaji kahawa

    Uganda ni mojawapo ya nchi zinazouza kahawa nje ya Afrika

    Maafisa wa Uganda kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (OPM) wamepewa jukumu la kueleza jinsi $2.6m (£2m) zilitumika kuwafunza vijana "jinsi ya kunywa kahawa" miongoni mwa mambo mengine, kwa mujibu wa waangalizi wa masuala ya bunge.

    Katika taarifa yake kwenye ukurasa wa Twitter, shirika lisilo la kiserikali la Parliament Watch lilisema kuwa mkaguzi mkuu alibaini baadhi ya maduka ya kahawa yaliyoorodheshwa kama sehemu ya kampeni hayapo.

    Mkataba uligawanywa katika sehemu nne:

    • Kutoa mafunzo kwa wakulima juu ya uzalishaji wa kahawa
    • Kufundisha vijana jinsi ya kunywa kahawa
    • Kutoa ujuzi wa kifedha
    • Usimamizi wa biashara

    Mkurugenzi katika ofisi ya Waziri Mkuu, Robert Limlim, alitetea gharama kubwa ya kampeni hiyo akisema inahusu elimu na pesa zilitumika kununua vifaa vya kahawa na kuleta vijana katika uchumi wa kahawa.

    Uganda ni mojawapo ya nchi zinazouza kahawa nje ya Afrika, ikiwa imesafirisha magunia milioni 5.7, yenye thamani ya $840m (£641m), katika kipindi cha miezi 12 kuanzia Juni 2022, kwa mujibu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Kahawa Uganda.

  5. Nchi za Ulaya hazijapokea kibali rasmi cha Marekani kuanza kuwafunza marubani wa Ukraine

    Mataifa ya Magharibi sasa yanapanga kutoa mafunzo kwa marubani wa Ukraine juu ya F16

    Nchi za Ulaya bado hazijapokea kibali rasmi cha Marekani kuanza kuwafunza marubani wa Ukraine kurusha ndege za kivita za F-16.

    Kulingana na uchapishaji huo ambao hawakutajwa majina maafisa wa Marekani na Ulaya waliohusika katika mazungumzo hayo, Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani bado haijaidhinisha uhamishaji wa nyaraka,vifaa vya ndege vya kompyuta na vifaa vingine.

    Takriban nchi 11 za Ulaya zikiongozwa na Uholanzi na Denmark zitashiriki katika mpango wa mafunzo kwa marubani wa Vikosi vya Wanajeshi vya Ukraine.

    Uamuzi wa kuanza kutoa mafunzo kwa marubani wa Ukraine ulifanywa rasmi wakati wa mkutano wa kilele wa NATO huko Vilnius, Politico inafafanua.

    Kulingana na chombo hiki cha habari, maafisa wa Ulaya wanatumai kuwa programu ya mafunzo itaanza nchini Denmark mapema mwezi wa Agosti, na kituo cha mafunzo pia kitaonekana nchini Romania.

    Politico inasema kuchelewa kunaweza kusababishwa na sababu za kiufundi, na "hakuna ushahidi kwa wakati huu kwamba Marekani haitatoa kibali chake katika siku zijazo." Hata hivyo, ombi la Ulaya la kuanza mafunzo limekuwa likizingatiwa kwa wiki kadhaa.

    Afisa wa ununuzi wa silaha nchini Marekani William Laplante aliiambia Politico katika mahojiano kwamba Idara ya Ulinzi ya Marekani inatoa idhini rasmi ya uhamisho wa nyaraka wakati kila kitu kiko tayari kwa hili, ikiwa ni pamoja na tafsiri na mipango ya msaada wa kiufundi.

  6. Habari, karibu katika taarifa zetu za moja kwa moja