Zuckerberg kutoa utajiri wake ‘kwa maskini’

Chanzo cha picha, Getty
Mwasisi wa Facebook Mark Zuckerberg na mkewe Priscilla Chan wamesema watatoa asilimia 99 ya hisa zao kwenye kampuni hiyo zitumiwe kwa hisani kuwasaidia binadamu.
Bw Zuckerberg ametoa tangazo hilo baada ya kuzaliwa kwa mwanawe wa kwanza, binti aliyepewa jina Max.
Tangazo hilo amelitoa kwa njia ya barua kwa Max ambayo ameiweka kwenye ukurasa wake wa Facebook.
Wawili hao wataweka hisa hizo kwenye wakfu wao wa Chan Zuckerberg Initiative kwa sababu wanataka ulimwengu uwe pahala pazuri pa Max kuishi.
Bw Zuckerberg amesema pesa hizo kwa sasa zinafikia $45bn (£30bn).

Chanzo cha picha, AP
Max alizaliwa wiki iliyopita, lakini wawili hao walitangaza hadharani kuzaliwa kwake Jumanne.
Mwekezaji bilionea Warren Buffet amewapongeza Zuckerberg na Chan, na kusema kwamba katika kutoa mali kusaidia maskini, “umri wa miaka 30 sasa umekuwa ndio miaka 70”.
Amesema matajiri hawafai kusubiri hadi wafe ndipo watoe pesa zao kwa watu wengine.































