Guinea-Sierra Leone ‘zakubaliana’

Guinea na Sierra Leone zakubaliana kumaliza mgogoro wa Mpaka
Maelezo ya picha, Guinea na Sierra Leone zakubaliana kumaliza mgogoro wa Mpaka
Iliyochapishwa

Guinea na Sierra Leone zimekubaliana kuondoa vikosi vyao kutoka kwenye mpaka unaozozaniwa, waziri wa mambo ya nje wa Guinea Edouard Nyankoi Lamah amesema.

Pande hizo mbili ziliahidi kutatua mzozo juu ya udhibiti wa mji wa Yenga kwa mazungumzo, alisema.

Vikosi vya Guinea viliingia Yenga zaidi ya muongo kusaidia jeshi la Sierra Leone kuapambana na waasi.

Zimekataa kurejesha mji kwa serikali ya Sierra Leone baada ya kuzima ghasia za kisiasa.

Bw Lamah, akizungumza baada ya ziara yake Freetown, alisema serikali hizo mbili zimekubaliana kuondoa majeshi yao kwenye eneo lao.

Msaada kutoa nje

"Jambo la kwanza ni kuondoa majeshi katika eneo hilo, hiyo ndio kusema jeshi la Sierra Leone litarejea kwenye mipak yake na vikosi vya Guinea navyo hivyo hivyo," alisema.

“Ni muhimu kuweka vitu vingine vyote pembeni na kutatua suala hiili kidilomasia.” Alisema Adikali Suma Sierra mwanadiplomasia kutoka Leone.

"Suala la pili ni kwa majeshi yote kufanya kazi pamoja na namna ya kuweka eneo huru mpakani."

Alisema Sierra Leone na Guinea zitaunda kamati zitakazosaidiwa na waatalam kutoka Uingereza na Ufaransa, makozloni ya zamani kusaidia kupata makubaliano.

"Kamati hizi zitatusaidia kuweka mpaka na kuonyesha kila nchi mpaka wake," alisema Bwm Lamah.

Balozi wa Sierra Leone nchini Guinea, Adikali Suma, alisema nchi zote zilikuwa na malengo kuepuka mgogoro.

"Ni muhimu kuweka pembeni vitu vingine vyote na kutatua suala hili kidiplomasia," alisema.

Mwaka 2005, Sierra Leone na Guinea zilisaini makubaliano kuhakiki Yenga – mji mdogo katika ukingo wa wa mto Makona ulio upande wa Guinea.

Hata hivyo vikosi vya Guinea vimebakia mjini humo.