Tetesi za soka Ulaya Jumanne 10.11.2020: Eriksen, Bale, Romero, Henderson, Giroud, Dembele

Chanzo cha picha, Getty Images
Tottenham wamepewa nafasi ya kumsajili tena kiungo wa kati wa Denmark Christian Eriksen, 28, kutoka Inter Milan. (Football Insider)
Tottenham huenda wakapewa nafasi ya kumsajili mshambuliaji wa Wales Gareth Bale, 31, kwa mkataba wa kudumu kutoka Real Madrid kwa kiwango cha chini cha hela cha hadi euro milioni 15 (£13.4m) (Mundo Deportivo - in Spanish)
Manchester United wamesitisha uamuzi kuhusu hatima ya baadae ya kipa Muargentina Sergio Romero,33 hadi pale mpango wa kumuuza Dean Henderson utakapokamilika, huku Muingereza huyo akiwa katika oradya ya uhamisho wa mkopo mwezi Januari. (ESPN)

Olivier Giroud anatafakari kuhusu maisha ya baadae katika klabu ya Chelsea. Mshambuliaji huyo aliye na umri wa miaka 34, aliyewahi kuhusishwa na klabu ya Inter Milan, huenda akahamia mahali ambapo patamhakikishia kujiunga na kikosi cha Ufaransa msimu ujao. (Football London)
Manchester United huenda wakamkosa Ousmane Dembele mwezi Januari, huku Barcelona ikijiandaa kumpatia mshambuliaji huyo wa Ufaransa jukumu kubwa baada ya Ansu Fati kuumia (Sport - in Spanish)
Jaribio la Chelsea la kumsajili mlinzi wa zamani wa Nottingham Forest Anel Ahmedhodzic kutoka Malmo zinazibwa kwa mujibu wa baba yake kiungo huyo raia wa Bosnia .

Chanzo cha picha, Twitter/BBC
Manchester United imemzuia mlinzi wao Victor Lindelof, 26, kujiunga na kikosi cha Sweden kwa mechi ya kirafiki na Denmark kutokana na masharti ya usafiri ya Covid-19 yanayotekelezwa kwa sasa na Uingereza. (Goal)
Manchester United inatafakari kuwapa uhamisho wa mkopo wachezaji wake watatu - kiungo wa kati wa Ireland Kaskazini Ethan Galbraith, kiungo wa kati wa Mhispania Arnau Puigmal na beki Ethan Laird -dirisha la uhamisho litakapofunguliwa mwezi Januari. (Manchester Evening News)
Liverpool imefunga kambi yao ya mazoezi ambayo wamekuwa wakitumia kwa zaidi ya miaka 60, Melwood. (Liverpool Echo)































