Virusi vya corona: Serikali zimeanza kulegeza masharti ya kukabiliana maambukizi, Je kulegeza masharti ni hatari kiasi gani?

Market stall
Maelezo ya picha, Soko la wanunuzi wa bidhaa mbali mbali la Kirkgate lililoko Leeds
Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 3

Nchini Uingereza watu wameanza kurejelelea shughuli zao za kawaida, watu kukutana, baadhi ya watoto wanarejea shuleni, maeneo ya kuonyeshwa magari yanafunguliwa, na masoko kufunguliwa tena.

Lakini baadhi ya wanasayansi hata wanaoshauri serikali wamekuwa na mitazamo tofauti na kusema kwamba serikali imechukua hatua za haraka.

Na kulegezwa kwa masharti kumeelezwa kama wakati hatari hata na naibu afisa mkuu wa matibabu Uingereza.

Sasa je tuko hatarini kiasi gani?

Kwa sasa hivi mambo yamekuwa mazuri kuliko hali ilivyokuwa wakati hatua ya kusalia ndani inaanza kutekelezwa.

Kulikadiriwa maambukizi mapya kila siku kufika 100,000 kote nchini Uingereza Machi 23, siku ambayo Boris Johson alitangaza hatua kali za kukabiliana na ugonjwa huo katika maisha ya kila siku.

Hiyo ni sawa na maambukizi mapya 8,000 kila siku kwa sasa.

"Ni karibia mara kumi zaidi kwa siku lakini idadi hiyo ni kubwa," Dkt. Adam Kurcharski kutoka London School of Hygiene and Tropical Medicine ameiambia BBC.

Kiwango cha usambaaji wa virusi ni cha chini mno.

Wastani wa watu wanaoambukizwa na kusambaza virusi kwa wengine ilikuwa karibu watu watatu kupindi cha kusalia ndani.

Hiyo ilimaanisha kwamba watu 10 walikuwa wanasambaza virusi vya corona kwa watu 30 kila siku.

Hata hivyo, ulinganisho wa chuo kikuu cha Oxford unapendekeza kwamba Uingereza iko katika hatari zaidi linapokuja suala la kulegeza masharti.

Virusi vya corona

Hatari iko vipi

Mshauri mkuu wa sayansi, Sir Patrick Vallance, ametahadharisha kwamba hakuna muda wa kupoteza.

Kulegeza masharti kunamaanisha kwamba watu watatangamana sana na kuongeza uwezekano wa kusambaa kwa virusi.

Masharti yakilegezwa kunatarajiwa kuchangia kidogo katika kusambaa kwa virusi lakini athari yake haijulikani.

Hasa kuna hali ya wasiwasi mashuleni.

Pengine haifahamike watu watachukuliaje hatua ya kufunguliwa tena shughuli na kulegezwa kwa masharti ingawa wanasanyansi wanashauri serikali kufikiria kwamba nusu tu watu ndio wanaojitenga kwa siku saba.

Kwanini wanasayansi wana wasiwasi?

Katika kipindi chote cha janga la corona, wanasayansi na wanasiasa wamekuwa na maono sawa.

Lakini kwa sasa hivi serikali iko wazi na imegawanyika kati ya wanaoshauri serikali na wanaofuata sayansi.

Zaidi ya watu kadhaa wa kamati inayoshauri serikali, wanasema tunastahili kusibiri hadi kupima na kutafuta waathirika kutafanikiwa na idadi ya wanaoambukizwa inapungua.

"Ni sawa na kufungua mfuniko juu ya sufuria inayotokota, na bila shaka tutarukiwa," amesema Profesa Calum Semple.

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe

Kulegeza masharti kipindi hiki kuna athari zake - kunaweza kuongeza idadi hiyo vibaya. Ikiwa masharti yatalegezwa na watu waendelee kukaribiana, bila shaka idadi ya wanaoambukizwa itaendelea kuwa karibu 8,000 kwa siku.

Kusubiri hadi idadi hiyo ipunge kabisa kutafaya iwe rahisi kudhiti virusi na kupata muda wa kuchukua hatua iwapo mlipuko wa pili wa maambukizi utatokea. Hata hiyvo, hilo litamaanisha kuongeza hatua ya kusalia ndani.

Maelezo ya video, Coronavirus: Utajuaje kuwa umeathirika na virusi?

Vipi kuhusu kutafuta wanaoambukizwa?

Pia kuna hali ya sintofahamu kuhusu ufanisi wa kutafuta walioambukizwa virusi nchini Uingereza.

Lengo ni kubaini na kutenga yeyote aliyetangamaa na mtu aliyepata maambukizi.

Mkakati huu unaonekana kama moja ya sababu kuu baadhi ya nchi za Asia zimefanikiwa kudhibiti virusi vya corona (Korea Kusini ikiwa na karibu vifo 270 ikilinganishwa na vifo zaidi ya 39,000 nchini Uingereza

Ukadiriaji wa ufanisi wa kupima na kutafuta waliopata maambukizi kunatofautiana sana kuanzia kupungua kwa maambukizi kwa asilimia 5 hadi asilimia 30.

Je tutapata wimbi la pili la maambukizi?

Idadi ya watu ambao wameambukizwa iko chini, kwa hiyo kinga ya mwili pia iko chini.

Hiyo ina maanisha kuna uwezekano wa kutokea kwa wimbi la pili la maambukizi lakini ikiwa hilo litatokea au la itategemea na maamuzi ya serikali na hatua itakazochukua.

Mpango unalenga kuanzisha hatua taratibu na kufuatilia kitakachotokea.

Kuongezeka kwa maammbukizi ni jambo ambao lina uwezekano mkubwa wa kutokea.

Dkt. Kucharski amesema: "Sidhani kama idadi ya maambukizi itaongezeka sana vile.

"Itachukuwa muda kwa hilo kutokea ikiwa mabadaliko yanafanyika kwa awamu; kulingana na kile kitakachotokea. Lakini pia huenda ikawa safari bado ni ndefu."