Tetesi za soka Ulaya Jumamosi 14.01.2023

mm
Iliyochapishwa

Newcastle wana nia ya kumsajili kiungo wa kati wa Ureno mwenye umri wa miaka 25 Ruben Neves, ambaye amebakiza miezi 18 kwenye mkataba wake na Wolves. (Mail)

Uongozi wa Chelsea upo nyuma ya meneja Graham Potter na wanapanga kuwaondoa wachezaji wengi ikiwa matokeo hayataimarika.(Telegraph - subscription required)

Arsenal wana uhakika wa kukamilisha usajili wa pauni milioni 80 wa Mykhailo Mudryk, 22, kutoka Shakhtar Donetsk kwa wakati ili winga huyo wa Ukraine acheze mechi yake ya kwanza dhidi ya Manchester United wikendi ijayo. (Times - subscription required)

mm

Chelsea wanaweza kumsajili fowadi wa Ufaransa Marcus Thuram kwa kitita cha €10m (£8.86m) mwezi huu huku kandarasi ya Borussia Monchengladbach mwenye umri wa miaka 25 ikikamilika mwishoni mwa msimu. (Caught Offside)

Liverpool walikutana na wawakilishi wa Sofyan Amrabat kujaribu kumshawishi kiungo huyo wa Fiorentina kuhamia Anfield, lakini mchezaji huyo wa kimataifa wa Morocco, 26, anapendelea kuhamia Atletico Madrid. (Mirror)

Chelsea na Tottenham wanatazamia kumnunua Leandro Trossard baada ya wakala wa winga huyo wa Ubelgiji kutoa taarifa akisema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 anataka kuondoka Brighton. (Football.London)

Manchester United imepokea nia ya kunyakua kutoka Mashariki ya Kati, Asia na Amerika na wako tayari kukaribisha zabuni rasmi kutoka kwao kufikia tarehe ya mwisho ya mwezi ujao. Bilionea wa Uingereza Sir Jim Ratcliffe pia anatarajiwa kutoa zabuni kwa klabu hiyo. (Telegraph - subscription required)

mm

Chelsea wako kwenye mazungumzo na PSV Eindhoven kuhusu kutaka kumnunua winga wa chini ya miaka 21 wa Uingereza Noni Madueke, 20. (Football.London)

Aston Villa wameanza mazungumzo ya kumsajili kiungo wa kati wa Marseille na Ufaransa Matteo Guendouzi, 23, na wamejadili kumpa mchezaji katika mkataba wa kubadilishana. (Football Insider)

Everton na Wolves wanavutiwa na beki wa Brazil Felipe Monteiro, 33, ambaye amebakiza miezi sita kwenye mkataba wake Atletico Madrid.(Mail)

The Toffees pia wametoa ofa ya euro 20m (£17.7m) kumnunua fowadi wa Lorient na Burkina Faso Dango Ouattara, 20. (Ouest-France - in French)

mm

Wolves wamekubali mkataba wa kumsaini kiungo wa kati wa Brazil Joao Gomes, 21, kutoka Flamengo.(Fabrizio Romano)

Timu hiyo ya Black Country pia inakaribia kufikia makubaliano ya kumsajili kiungo wa kati wa Uhispania Pablo Sarabia, 30, kutoka Paris St-Germain. (Talksport)

Club Bruges imekubali dili la kumsajili kipa wa England Josef Bursik, 22, kutoka Stoke. (Telegraph)

Nice wamekubaliana na Lorient kwa ajili ya kumnunua fowadi wa Nigeria Terem Moffi, 23, ambaye pia amekuwa akihusishwa na ofa kutoka Southampton. (Footmercato - in French)

Tottenham inasalia kuwa na hamu ya kumsajili mchezaji wa kimataifa wa Uhispania Pedro Porro, 23, kutoka Sporting Lisbon lakini wanahitaji kumuuza beki wao wa kulia - Mchezaji wa kimataifa wa Jamhuri ya Ireland Matt Doherty, 30, au Mbrazil Emerson Royal mwenye umri wa miaka 23 - kwanza. (Standard)

mmm

Newcastle United na Tottenham zinaweza kushindana kuwania saini ya kiungo wa kati wa Roma na Itlay Nicolo Zaniolo, 23.(Calciomercato - in Italian

Burnley wana nia ya kumsajili beki Mholanzi mwenye umri wa miaka 19 Jenson Seelt kutoka PSV Eindhoven na mlinzi wa Uswidi Hjalmar Ekdal, 23, kutoka Djurgardens. (Mail)

Kiungo wa kati wa Manchester United Scott McTominay, 26, hauzwi mwezi huu licha ya Everton, Southampton, Leeds, West Ham na Leicester zote kuonesha nia ya kutaka kumnunua mchezaji huyo wa kimataifa wa Scotland. (90Min)

Beki wa pembeni wa Aston Villa Mfaransa Frederic Guilbert, 28, anatazamiwa kusaini mkataba wa kudumu na Strasbourg, ambapo alitumia kipindi cha pili cha msimu uliopita kwa mkopo.(L'Equipe - in French)