Kurunzi ya Qatar 2022: Taarifa 5 kubwa jioni hii kuhusu kombe la dunia

world cup
Iliyochapishwa

1. Ghana yatuma salamu Qatar

Katika kujiandaa na mashindano ya kombe la dunia, Ghana leo imetuma salamu kwa kuichapa Switzerland 2-0 katika mchezo wa maandalizi ya mashindano hayo.

Ghana wako kundi H wakianza kufungua dimba na Ureno Alhamisi ijayo huku Switzerland walio kundi G watakipiga na wawakilishi wengine wa Afrika, Cameroon siku hiyo hiyo.

Ruka X ujumbe, 1
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

Mwisho wa X ujumbe, 1

2. Maddison akosa mazoezi ya England

g

Kiungo James Maddison hakufanya mazoezi na wenzake wa England kushughulikia jeraha lake la goti.

Maddison alitolewa katika mchezo wa mwisho wa Leicester kabla yamapumziko ya kombe la dunia, kwa sababu ya majeruhi, ikiwa ni siku mbili baada ya kutajwa kwenye kikosi cha England kinachoshiriki kombe la dunia huko Qatar.

Alipoulizwa kama ataweza kucheza mechi ya kwanza ya England Jumatatu dhidi ya Iran. alisema: "mambo yatakuwa mazuri. Nadhani hivyo."

3. Joto kali lailazimisha Wales kuhama uwanja wa mazoezi

world cup

Wales imelazimika kubadilisha mipango yake ya mnazoezi na uwanja kutokana na joto kali huko Doha, Qatar.

Kikosi cha Robert Page kilikuwa kianze mazoezi kila siku saa 7:30 mchana kila siku kwa saa za huko kujiandaa na mchezo wao wa ufunguzi dhidi yaMarekani siku ya Jumatatu.

Pamoja na kuiweka michuano ya mwaka huu wakati huu, bado joto ni kali, na sasa wanafanya saa 10:00 jioni kuanzia leo.

5. Ronaldo 'kuwakosa' Wanigeria

world cup

Cristiano Ronaldoa ataukosa mchezo wa leo wa kirafiki wa Ureno dhidi ya Nigeria, kujiandaa na kombe la dunia kutokana na kusumbuliwa na tumbo.

Mshambuliaji huyo wa Manchester United hakuwepo kwenye mazoezi jana.

Ronaldo kwa sasa ametapakaa kwenye vichwa vyahabari kufuatia mahojiano yake na Talk TV, kwamba United imemsaliti.

Kocha wa Ureno Fernando Santos alipoulizwa kama Ronaldo amewaambia lolote alisema: "Hapana, sidhani kama Cristiano analazimika kufanya hivyo".

4. Conor Cody - anaeleza namna England inavyopambana na joto

Ruka X ujumbe, 2
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

Mwisho wa X ujumbe, 2