Tetesi za soka Ulaya Alhamisi tarehe 28.04.2022: Haller, Phillips, Lewandowski, Rice, Rodriguez, Pepe

Chanzo cha picha, Getty Images
Borussia Dortmund itachuana na Manchester United kusaka saini ya mshambuliaji wa Ajax na Ivory Coast Sebastien Haller, 27. (Sun)
Arsenal itafanya mazungumzo na nyota wake anayeshikilia rekodi ya uhamisho klabuni hapo Nicolas Pepe, 26, mwishoni mwa msimu kuhusu hatma ya winga huko wa Ivory Coast. (Standard)

Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester United wanataka kutoa £50m kwa ajili ya kiungo wa Leeds United na England Kalvin Phillips, 26, msimu ujao. (The Athletic - subscription required)
Barcelona inapambana kumsajili mshambuliaji wa Bayern Munich Robert Lewandowski, 33, lakini bado hawajapeleka ofa kwa ajili ya nyota huyo wa kimataifa wa Poland. (Fabrizio Romano)
Mshambuliaji wa Everton na England Dominic Calvert-Lewin, 25, angetamani kutua Arsenal kuliko Newcastle. (Football Insider)

Chanzo cha picha, Getty Images
Mshambuliaji wa zamani wa Everton James Rodriguez, 30, anataka kurejea Ulaya ambapo Mcolombia huyo itamlazimu kushusha mshahara wake kufanikisha hilo. (Star)
Manchester United wanajua kwamba msimu huu ni nafasi nzuri kwao kumsajili kiungo wa kimataifa wa England Declan Rice, kwa sababu washindani wao wanaomsaka kiungo huyo wa West Ham mwenye miaka 23 wamejielekeza zaidi kuboresha nafasi zingine kwenye vikosi vyao kama vipaumbele vyao. (Standard)
Roma inaitolea macho ligi kuu England msimu huu. Klabu hiyo ya Serie A inamtaka kiungo wa Arsenal na Switzerland Granit Xhaka, 29, kiungo wa Aston Villa Mbrazil Douglas Luiz, 23, na kiungo wa Manchester United Mserbia Nemanja Matic, 33. (Calciomercato - in Italian)
Kiungo wa Liverpool na Hispania Thiago Alcantara, 31, awali alitakiwa na Manchester United kabla ya kutua Anfield, anasema Rio Ferdinand. (Vibe with Five podcast)

Chanzo cha picha, Getty Images
Mlinzi mfaransa wa Arsenal 21 William Saliba, 21 - ambaye kwa sasa anacheza kwa mkopo Marseille - anapanga kurejea 'the Gunners' mwishoni mwa msimu kupambania namba kwenye kikosi cha Mikel Arteta. (Teamtalk)
Unai Emery anataka kumsajili mshambuliaji wa Watford Mnigeria Emmanuel Dennis, 24, kumpeleka Villareal katika dirisha la kiangazi. (Standard)
Wolves inataka kumsajili mshambuliaji wa Valencia mreno Goncalo Guedes, 25. (Telegraph)
Kiungo wa Oxford United muingereza Cameron Brannagan, 25, anavivutia vilabu vya Sheffield United, QPR, Stoke, Preston na Blackpool. (Sun)
































