Tetesi za soka Ulaya Jumanne tarehe 26.04.2022 Rudiger, Rice, Mbappe, De Jong, Messi, Origi

Iliyochapishwa

United inaweza kuwapa Barcelona mshambuliaji wake wa kimataifa wa England Marcus Rashford na mlinzi wa kushoto Mbrazil Alex Telles, 29 kubadilishana na De Jong. (Fichajes)

Mshambuliaji wa Paris St-Germain Kylian Mbappe, 23, amekuwa akihusishwa nkutaka kuhamia Real Madrid katika majira ya kiangazi, lakini nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa hatatangaza rasmi kuhusu hatma yake mpaka baada ya mchezo wa mwisho wa klabu hiyo msimu huu dhidi ya Metz, Mei 21. (Marca)

Norwich City imeingia katika mbio za kumsaka kiungo muingereza wa Bristol City Alex Scott, huku Tottenham na Leeds tayari zinamfuatilia kinda hilo la miaka 18. (Football League World)

Barcelona wanaweza kukubali kumuachia Frenkie de Jong, 24, kuondoka kwa ada ya £58m, huku Manchester United ikionyesha nia ya kumtaka kiungo huyo wa Uholanzi. (El Chiringuito)

Real Madrid inakaribia kufikia makubaliano ya uhamisho kwa ajili ya mlinzi wa Chelsea Antonio Rudiger, huku Mjerumani huyo mwenye umri wa miaka 29 akiwa tayari kuhamia Bernabeu kwa mkataba wenye mshahara wa angalau £200,000 kwa wiki. (Guardian)

Manchester City wanafikiria kumnasa kiungo wa West Ham na England Declan Rice, 23, ambaye amekuwa akisakwa kwa muda mrefu pia na mahasimu wao Manchester United na Chelsea. (Telegraph, subscription required)

Meneja mpya wa Manchester United Erik ten Hag atafanya mkutano wa mtandao na mchezaji mmoja mmoja kutathmini nani atasalia au kuondoka kabla ya kushika mikoba mwezi Juni. (Mirror)

Mchezaji ambaye ni wazi anaondoka Old Trafford ni Paul Pogba, 29, na tayari kiungo huyo mfaransa ameshajiondoa kwenye kundi la WhatsApp la timu hiyo baada ya kupata ofa kutoka Real Madrid na PSG. (Mirror)

PSG itambakiza mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi, 34, kwa msimu mmoja zaidi lakini iko tayari kuruhusu mshambuliaji wa Brazil Neymar, 30, leave. (Sky Sports News)

AC Milan inakaribia kufikia makubaliano na mshanbuliaji wa Liverpool mbelgiji Divock Origi, 27. (Calciomercato)

Juventus iko kwenye mazungumzo ya kumsajili winga wa Argentina Angel di Maria, 34 kwa uhamisho huru mwishoni mwa msimu baada ya kuamua kutoongeza mkataba wake. (Goal)

West Ham itaanzisha mazungumzo na Hull City kwa ajili ya kumsajili mshambiliaji muingereza Keane Lewis-Potter. Hull imekataa ofa ya £12m kutoka Brentford, ikisema thamani ya kinda hilo lenye miaka 21 inafikia £18m. (Athletic, subscription required)

Stade Reims itamruhusu mshambuliaji mfaransa mwenye miaka 19 Hugo Ekitike kuondoka klabuni hapi kwa ada ya £30m msimu wa kiangazi na Newcastle wanatarajia kurejesha nia yao ya kumsajili baada ya kufanya mazungumzo na kinda huyo mwezi Januari. (Shields Gazette)

Ekitike alikua akisakwa pia na Liverpool, Chelsea na Manchester United. (Goal)

Ilkay Gundogan, 31, anasema angefurahi kumaliza soka lake Manchester City, lakini kiungo huyo wa Ujerumani angetamani kutimkia ligi ya Uturuki Turkish au MLS ya Marekani mkataba wake utakapomalizika mwaka 2023. (Sport 1, in German)

Neco Williams anasema hajua atacheza klabu gani msimu ujao. Mlinzi huyo wa kulia wa Wales mwenye miaka 21 kwa sasa anacheza kwa mkopo Fulham akitokea Liverpool. (Wales Online)

Udinese inataka kumsajili mlinzi wa Arsenal, mhispania Pablo Mari, 28, kwa mkataba wa kudumu atakapomaliza mkataba wake wa mkopo. (Football London)

Newcastle inamfuatilia mlinzi mfaransa wa Eintracht Frankfurt Evan Ndicka, 22. (Bild - in German