Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Chelsea mabingwa wa kombe la dunia kwa vilabu
Miamba ya soka ya England klabu ya Chelsea hapo jana ilitwaa ubingwa wa kombe la dunia kwa vilabu kwa kuifunga Palmeiras ya nchini Brazil kwa magoli 2-1.
Chelsea imekuwa timu ya tatu kutoka England kuchukua ubingwa wa Dunia wakiungana Liverpool na Manchester United.
Beki wa Chelsea Thiago Silva alishinda tuzo ya mchezaji bora wa michuano ya hiyo ya kombe la dunia kwa ngazi ya vilabu michuano ambayo mwaka huu lilifanyika katika nchi za Falme za kiarabu katika jiji la Abu Dhabi.
Meneja wa Chelsea Thomas Tuchel amepata mafanikio makubwa akiwa na The Blues toka ajiunge na timu hiyo akitokea Psg ya Ufaransa.
Tuchel Ametwaa mataji matatu makubwa
-Kombe la dunia la Vilabu
-Kombe la ligi ya mabingwa ulaya
-Kombe la UEFA Super Cup
Pia umekuwa ni mwaka mzuri kwa golikipa namba moja wa kikosi cha Chelsea Edouard Mendy ambae Mwezi huu wa Ferbuary ametwaa taji la ubingwa wa Africa ( Afcon) akiwa na timu ya taifa ya Senegal.
Katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu wawakilishi wa Bara la Africa Al Ahly kutoka nchini Mirsi walimaliza katika nafasi ya tatu kwa ushindi wa magoli 4-1 Al Hilal ya Saudia Arabia.