Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Watumishi wa afya Kenya waonywa kupoteza ajira zao
Waziri wa Afya nchini Kenya bwana Mutahi Kagwe ametoa angalizo kwa wafanyakazi wa afya nchini humo kuwa watafukuzwa kazi endapo wataendelea na mpango wao wa kugoma.
Kagwe amewaambia manesi na maofisa wa afya kusitisha mgomo na kurejea kazini kama wanataka kuendelea kuwa na ajira zao.
Aidha bwana Kagwe ametaka ajira zianze kutangazwa katika kaunti mbalimbali kuchukua nafasi za kazi za waliogoma.
"Taifa linabidi lianze kuajiri watumishi wa afya wapya ili kuchukua nafasi za wanaogoma ," alisema.
Aliongeza kusema kuwa sasa Kenya ina manesi 8,000 ambao hawana ajira na wapo nyumbani tu.
"Kama wafanyakazi wataendelea kugoma basi watumishi walio nyumbani waajiriwe ," alisisitiza.
Madaktari wa Kenya wamekuwa wakilalamikia malipo duni , ukosefu wa vifaa vya kujikinga pamoja na huduma ya bima.
Madaktari walikuwa mapema mwezi huu lakini waliamua kuipa serikali muda wa wiki mbili kufanyia kazi madai yao.
Ingawa wahudumu wengine wapatao 30,000 wakiwemo manesi walianza mgomo wao.